IMF wathibitisha, Serikali imeishiwa!


Labda hujasoma haya maandishi za Zambarau. This is a warning FROM IMF kuwa matumizi ya serikali yanazidi hata makusanyo ya kodi, na misaada ya wafadhili na hilo linapelekea kukua kwa DENI LA SERIKALI!!!!!
 

Well said Mdondoaji,
Unajua the way hawa wanaendesha uchumi nikama miaka ile tukiwa watoto tunaiba gari nyumbani na kutumia mafuta yote ya mzazi na kumrudishia empty; kinachoendelea ni hayo hayo, tumia nafasi zao na kukamua kila kitu then kurudishia maskini nchi yao ikiwa empty.
 
Merekani wanakopa itakuwa Tanzania? mnanchekesha!

Merekani ndo nini? unamaanisha merereni kwenye tanzanite? au marekani? Kama ulikusudia marekani basi hujui wanamaanisha nini wanaposema marekani inakopa. Hawakopi kwa bakuli kama unavyofanya wewe na raisi wako mnunuliwa suti, unaposikia kuwa serkali ya marekani imekopa maana yake ni kwamba serkali hiyo imeiamuru federal reserve bank yao kuchapisha dola zaidi. Tofauti yao na sisi ni kwamba sisi tukiiamuru BOT kuchapisha zaidi madafu yetu basi yanashuka thamani kama yale ya Mugabe, wao hata wachapishe kwa wingi kiasi gani thamani ya pesa yao inabaki vilevile. Ila kwa kukudanganya wewe wanakuambia hiyo extra pesa waliochapisha wameikopa. Nchi za ulaya na marekani ndo wanavyofanya, hivi sasa baadhi yao wanataka kusitishwa kwa uchapishaji huo (Ukopaji) kwa madai kuwa serkali zao zimeongeza sana matumizi hasa kwenye social services, wanajadili namna ya kupunguza matumizi ya serkali zao ili wawe na budget ndogo ambazo hazitawafanya waendelee kuchapisha mihela ovyo ovyo na wanawasiwasi wakiendelea kufanya hivyo uchumi wa dunia nzima unaweza ku collapse. Kama unaswali zaidi unaweza kuni pm nitaendelea kutoa tuition bure.
 

ubarikiwe katika bwana akaaye juu mahali palipoinuka. Nadhani wengi hili hawalijui, wanaweza vilivile kufuatilia oil scam ya marekani 1972 ndiyo watatambua kuwa wenzetu hawahaingaiki kama sisi.
 
Hii nchi ilifilisika wakati wa NYERERE, wakaja kutuokoa hao hao IMF cha ajabu ni nini? leo Tanzania tuna reserve ya kututosha miezi sita na uchumi umepanda mpaka UN wametambuwa hilo na kutupandisha chart.

Nyie mnakuja na sijui nini sijui nini, IMF hata nchi za magharibi wanakwenda, tazama Ugiriki kuna nini sasa hivi? msituletee porojo za mitaani.
 
Merekani wanakopa itakuwa Tanzania? mnanchekesha!

Dada FF, kukopa sio shida. Tatizo ni pale unapokwenda kukopa ili ukanunue mashangi, au ukalipie gharama za safari za nje za rais wako, au ukalipe watu kama dowans n.k. Marekani, hata china bado wanakopa mpaka kesho, lakini matumizi ya fedha hizo za mikopo ni kwa ajili ya miraji yenye tija( kiuchumi na kijamii) kwa mataifa yao. Naomba uelewe.
 

Faizafoxy saa hizi tayari hushapata Lager ngapi!!! Loh!
 

ningependa kujua inakuwaje wao wakichapisha hela zaidi, dola haishuki thamani nasi tukichapisha inashuka.?
 

Kuna siku JK na Mkulo watakuwa wanaangaliana tu bila cha kufanya pale nchi itakapo kufa kifo cha mende....uchumi unaelekea kusimama wakuu.


Usijali. Watahalalisha ushoga wapewe £ na bwana Cameron!
 
hii serikali bana,mpaka simu imeuza imebaki na line,ili uchaguzi ujao ishinde ki-line. Nalog off
 
sas huku tunakoelekea ni kule waliko wenzetu wa Turkey!
Mungu atuepushie mbali na hili!
Eee Molah tuepushie hili balaaaa!
 

Faiza, hivi unajua kwanini Tanzania wakati wa nyerere ilifilisika? naomba mawazo yako kwanza kabla sijakujibu maana unaweza kuwa na hoja ambayo kwa sababu moja au nyingine hukuitoa; Kuhusu uchumi kupanda, je huo uchumi ume trickle down to the micro level au ni uchumi uchwara? Inasikitisha kuona kuna watu wanashangilia kukua kwa uchumi kitakwimu, basi tuwe na siku moja ndani ya mwaka ya mapumziko - siku ya kusherehekea kukua kwa uchumi Tanzania maana since mwaka 2000, tume average at very impressive rates (over 6%) yet we are in one of our darkest moments katiak historia ya nchi hii. Wewe kusema uchumi umepanda hata UN wanatusifia ni kama mwajiri kumwambia mfanyakazi mshahara wako umepada by 10% na yeye kwenda mbio nyumbani kushehereke na familia yake bila kwanza ya kuangalia, ok, mshahara mwaka huu umepanda by 10%, je inflation? kwani kama ni by lmore than 10% imekula kwako; na hivyo ndivyo uchumi huu unakula kwa wananchi - more growth - more poverty; Uchumi huu sio pro - poor na ujue kwamba kilichofanya uchumi wetu ukue sana kuanzia mwaka 2000 ni mchango wa production ya gold, tukitoa gold katika equation ya GDP, uchumi wetu utakuwa chini sana kwani for the past 15 years, productivity in the agricultural sector has stagnated; kwenye manufacturing sector hakuna any meaningfu valued added growth;

Kuhusu nchi za magharibi kama Greece wanapata matatizo, yes ni kweli lakini as a result, viongozi wanaachia ngazi kukubali wamekosea!!!
 
Ndugu yangu, kwa huyu mtu ni bora ujaribu kutwanga maji kwenye kinu. Una possibility ya kupata unga kwa kufanya hivyo kuliko yeye kukuelewa


QUOTE=gmosha48;2777287]Dada FF, kukopa sio shida. Tatizo ni pale unapokwenda kukopa ili ukanunue mashangi, au ukalipie gharama za safari za nje za rais wako, au ukalipe watu kama dowans n.k. Marekani, hata china bado wanakopa mpaka kesho, lakini matumizi ya fedha hizo za mikopo ni kwa ajili ya miraji yenye tija( kiuchumi na kijamii) kwa mataifa yao. Naomba uelewe.[/QUOTE]
 

Tafadhali, kuna mkopo usioelezwa ni wanini siku hizi? IMF wana sheria zao za mikopo, na la kwanza inabidi wakupe masharti ambayo kama huyatimizi hawakupi, sasa wewe unaleta habari za kufikirika, mashangi sijui nini, wewe barabara alizotuwachia Nyerere hapa bila magari kama yale unafikiri kuna sehemu utazipita? wachaaa, usione sasa hivi Kikwete anajitahidi kutandaza mabarabara ukadhani ndio kote kupo hivyo.

Halafu unaongelea safari za kikwete, unafikiri anakwenda kucheza huko anakokwenda? ni nani anaetaka kusafiri kila siku? inafaa umpe sifa Kikwete kwa kufanya kazi kwa bidii usiku na mchana. Wewe hii Tanzania ya Kikwete leo ndio Tanzania ilivyokuwa hapo nyuma? maendeleo kila pembe lakini mnajidai kuyafumbia macho. Kikwete ndio Rais pekee wa Tanzania aliotangaza rasmi "hafi mtu kwa njaa hapa" na kweli, ni nani mwingine ambae hawajafa watu kwa njaa Tanzania hii.

Unaujuwa wakati wa Nyerere wewe> au unausikia tu? tulikuwa hatujui cha kukila kesho nini, unapanga foleni hjui kinachotolewa leo nini> kama ni mchele au unga au sukari. Leo unakwenda kuchaguwa untaka mchele wa wapi? Mbeya, Shinyanga, Ifakara, Mwanza, Pakistan, Thailand, India? yalikuwepo hayo wakati wa Mtakatifu? wacheni chuki binafsi tazameni ukweli.
 
Na bado kila wizara inaendelea na matumizi ya kutisha eti kusheherekea miaka 50 ya uhuru wakati wizara hizo hazikuwapo tangu uhuru. Sijui hayo mafungu ya sherehe nani anayaidhinisha maana sasa hivi imefanywa ndio uchochoro wa kupiga kila senti iliyopo wizarani.
 
FF haelimishiki, unapotezwa muda wako bure.
 

Hoja zenu ni nzuri sana sasa tufanyeje maana hata hao mataifa makubwa yakitokea matatizo kama haya wanajadili tufanyeje sio kulaumu?????
 
Aliye kuroga ni lazima alishakufa, sijui utatibiwa na nani, Lakini sikushangai kwakuwa wewe mwenzetu unafaidi makombo ya huyo shetani wako ibilisi usiye na soni.
 

Kimsingi uko sahihi- haswa kwa kuzingatia sentensi yako ya mwisho. Unachotakiwa kutambua ni kwamba, nchi/uchumi hauendeshiw tu kwa mishahara, posho na maendeleo. Lipo pia fungu la ghrama nyinginezo ( other charges): Mafuta, madawa, vitabu, chaki, kombat za police, nk. Tazama kifungi F hapo juu utaona mchanganuo. Kuna point mbili za msingi kwenye huu mjadala:
1) Tujitahidi sana kuhakikisha gharama za uendeshaji wa serikali ( recurrent expenditutures) zinatokana na makusanyo ya kodi. Na pia, matumizi kwenye fungu hili yawe ni ya lazima tu. Sii kama sasa ambapo tumekimbilia kununua mashangingi kwa killa boss serikalini. Uwezo wetu wa makusanyo ya ndani haukidhi mahitaji hayo.

2) Tunatakiwa kutenga kiasi kikubwa zaidi kwa ajili ya shughuli za maendeleo ( Capial Expenditure). Hapa nataka kutofautisha shughuli za maendeleo kweli- haswa katika uwekezaji katika miundo mbinu- barabara, nishati na mawasiliano, tofauti na mtindo wa sasa ambapo bajeti ya maendeleo bado mejaa mafungu kibao ya semina, posho, safari na marupurupu yasiyokuwa na tija kwa uchumi wetu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…