Kikwete aseme ukweli, yeye in sehemu ya haya mauaji! Haiwezekani akawa na intelijensia ambayo huwa inaweza kugundua kuwa wapinzani wakiandamana kutatokea uvunjifu wa amani lakini hawawezi kugundua wauaji wa watanzania ambao yeye kama Rais amepewa dhamana ya kuwalindana Bado akakaa kimya Kimsingi, kwa kitendo tu cha watu kuendelea kufa yeye akiwa madarakani kilitosha kumlazimisha ajiuzuru kwa kushindwa kuilinda katiba inayosema wazi kuwa kila mtanzania ana Haki ya kuishi. Ni jukumu la serikali kuhakikisha kwamba hakuna mtanzania anayekosa Haki yake ya kuishi eti kwakuwa tu kuna mwanasiasa anataka kiungo chake ili ashinde uchaguzi. Kama hawezi kabisa kuzuia hali hii ajiuzuru. Hatakuwa wa kwanza kuachia ngazi Sikh chache kbla ya muda wake kuisha. Hata Mbeki alifanya hivyo. Ajenge heshima japo kwa njia hiyo. Hii ni aibu kubwa!