Tafiti kadhaa zimeshafanyika juu ya uwezo wa mti wa Mugariga anaotumia Babu wa Loliondo kutibu. Mti huo kitaalamu unaitwa Carrisa edulis umeonekana kuwa na uwezo mkubwa wa kupambana na aina tofauti ya virusi wanaomshambulia binadamu kama Herpesvirus na wengine
source Anti-viral activity of the extracts of a Kenyan me... [J Ethnopharmacol. 2006] - PubMed result
www.ku.ac.ke/.../In_vitro_anti-viral_activity_of_aqueous_extracts_of_Kenyan.pdf
Haijaripotiwa kama kuna utafiti umeshafanywa juu ya virusi vya ukimwi, au virusi vingine vinavyohusika na cancer.
Kazi kwenu watafiti...
Mti anaoutumia Babu wa Loliondo unaitwa Carissa edulis na umekuwa published na baadhi ya scientists wa Kikenya March 2006 (Journal of Ethnopharmacology, Volume 104, Issues 1-2, 8 March 2006, Pages 92-99).
Sample size, methodology iliyotumika na imefanyiwa utafiti lini? Inatakiwa matokeo ya dawa hiyo yawe published kwenye recognised journal ili yakubalike.
I gues the side effects will be less effective than on the curretive side.
Tumesikia wengi waki confess wamepona, Ila binafsi sijasikia aliyeconfess kupatwa na Madhara.
Ningeshauri serikali iwe strict kidogo kwa hawa wengine wanaojitokeza na kudai wameoteshwa na mama zao.
yaani amini msiamini, Foleni ya Mbeya kama Loliondo, Dogo anadai kaotesha na mama yake aliyekuwa mganga wa kienyeji.
Kuna watu wamepata kikombe cha mbeya na wamepata madhara makubwa sana, The Govt should act soon!!!!
Tumshikuru Mungu kwa kazi yake. Taifa lilikua linaangamia
Well done Jackbauer! Matokeo yako yanaonyesha before and after the treatment.
Ongezea sample size na hapo utaweza kujua statistically kama kuna improvement yo yote au la.
Hata hivyo Serikali inashindwa kwa sasa kutoa taarifa ya awali kwa sababu ya complications za "Hati Miliki" na pia hatma ya muendelezo wa dawa hiyo. Inasemekana kwa kuwa dawa hiyo imechukuliwa mikononi mwa Babu kwa ruhusa yake, hakuna mwenye uwezo wa kisheria wa kufanya chochote bila ridhaa ya Babu.
Kuna kazi kubwa saana Tanzania, hapa JF wachangiaji ndio hao wanaonekana kuwa wameenda shule. Hao ambao hawajasoma inakuwaje? Tunalazimisha vitu kutokana na hisia na imani zetu. Hata hiyo chroroquine iliyoitaja nayo pia ilikuja kugundulika kuwa na madhara. Wanaoumwa wana haki ya kuhangaika na tiba kwa kuwa kila ambacho hushauriwa kuwa kitawaponya wangependa kujaribu, lakini kwa hili la kuacha tiba ambazo zilishachunguzwa na kujikita kwenye tiba isiyo na uchunguzi ni kuweka maisha hatarini.
Binafsi ninawasihi wale wanaoumwa waendelea kutumia dawa za kitaalamu kama hii ya babu inaponya wasubiri majibu ya tafiti kisha ndio wataamua la kufanya. Wasiache dozi, Taifa bado linawahitaji.
1. Kisukari - 100% ACTIVE
2. Saratani - 100% ACTIVE
3. Vidonda vya Tumbo - 100% ACTIVE
4. Ukimwi - 99% ACTIVE
Hakuna dawa isiyokuwa na side effects, kinachogomba ni kuzidiana kwa hizo effects!
Binafsi naipongeza taasisi hii iliyofanya utafiti huu wa awali, angalau wameonyesha japo kwa dim-light kwamba dawa ya babu inatibu kwa percentage hizo !
Kwanini hiyo hatimiliki isitolewa kwa jina la babu kama hatua ya awali, ili serikali iwe huru kutoa taarifa ya utafiti kwa jamii?...au kuna shida ya maslahi?
kwa kufanya utafiti ndio tunaweza kujua ukweli
Habari za uhakika kutoka moja kati ya Taasisi ya Serikali iliyopo chini ya Wizara ya Afya inayojishughulisha na utafiti wa tiba zimethibitisha kuwa "Dawa ya Babu wa Loliondo" inatibu.
Chanzo cha habari hizi kutoka kwa moja kati ya watafiti wa Taasisi hiyo nyeti ambayo pia inafadhiliwa na Wamarekani ambaye ana shahada ya Uzamifu (Ph.D) na pia ni moja katika ya Wakurugenzi katika Taasisi hiyo zinasema kuwa utafiti wa awali katika maabara kutoka katika Samples za dawa ya "Kikombe Cha Babu" inaonyesha kuwa dawa hiyo ni "ACTIVE" katika kutibu magonjwa yafuatayo:
1. Kisukari - 100% ACTIVE
2. Saratani - 100% ACTIVE
3. Vidonda vya Tumbo - 100% ACTIVE
4. Ukimwi - 99% ACTIVE
Chanzo cha habari kilisema Babu alikubali Serikali kuchukua Samples za dawa hiyo baada ya kuhakikishiwa kuwa hawaendi kuwapa watu vikombe bali ni utafiti. Baada ya kuhakikishiwa Babu alitoa baraka zake.
Hatua hiyo ilikuwa ni muhimu hasa baada ya taarifa za kuthibitika kuonyesha kuwa hata Mkuu wa Kaya alikuwa ni kati ya watu wa Mwanzo kupata kikombe cha Babu mbali ya viongozi wengine wa Juu wa Serikali pamoja na vyama vya Siasa.
Changamoto kubwa kwa sasa ni utafiti juu ya "Madhara" au Side Effects zinazotokana na dawa hiyo na hapo panahitaji umakini. Kama side effects zitakuwa mbaya na Mkuu wa Kaya na viongozi wengine wameshapata kikombe inatubidi kuwa makini katika kuchuja matokeo au findings hizo.
Chanzo hicho pia kilisema Dawa ya Babu iliwahi kufanyiwa utafiti wa Maabara na Wakenya ambao waliipa jina la "KEMRON". Hata hivyo utafiti huo wa Wakenya katika maabara haukuendelea kwa sababu ambazo hazijafahamika.
Akionyesha kuwa Dawa ya Babu inaweza kufaa, alitolea mfano kuwa Dawa ya Chloroquine ambayo iligunduliwa miaka ya 1934 kabla ya hapo ilikuwa inatolewa na "Mtumishi Wa Mungu" ambaye naye alidai pia alionyeshwa na Mungu na ilimpasa mgonjwa yeyote anywee dawa hiyo ya mitishamba akiwa Kanisani. Baadaye mtafiti moja aliichukua dawa hiyo na kuifanyia utafiti na kugundua kuwa ilikuwa inatibu Malaria. Kabla ya hapo wengi waliidharau wakidhani kuwa ilikuwa ni sumu au ina side effects nyingi.
Hata hivyo Serikali inashindwa kwa sasa kutoa taarifa ya awali kwa sababu ya complications za "Hati Miliki" na pia hatma ya muendelezo wa dawa hiyo. Inasemekana kwa kuwa dawa hiyo imechukuliwa mikononi mwa Babu kwa ruhusa yake, hakuna mwenye uwezo wa kisheria wa kufanya chochote bila ridhaa ya Babu.
Huu unaweza kuwa ni Mwanzo wa nuru mpya ya matibabu katika magonjwa haya sugu. Ingawa Babu amekuwa akibezwa na baadhi ya watu, lakini kumekuwa na ushahidi wa kutosha kutoka kwa watumijaii wa dawa yake kuwa inawasaidia na pia imewaponya. Hata hivyo wapo pia Wagonjwa wanaozidiwa njiani na kufariki na pia wapo ambao wamepata Kikombe na kufariki kwa kuwa hali zao zilikuwa mbaya au kutokana na matatizo mengine ya kitabibu.
Ingawa Babu amekuwa akitumia Kikombe maalumu ambacho anadai amepewa na Mungu lakini kwa sasa tafiti za awali za kisayansi na matokeo ya waliopona au kupata nafuu vinaonyesha kuwa dawa yake inatibu.
Ni juu ya Serikali na "Babu wa Loliondo" kukaa chini kwa pamoja na kuangalia ni nini cha kufanya. Wasiwasi mkuu uliopo kwa sasa ni juu ya "Side Effects" za dawa hiyo kama zitakuwepo.
Wadau hii imekaaje? Kazi kwenu!
ndugu zangu,
kumekuwa na misimamo mingi na kinzani kuhusu uwezo wa dawa ya babu wa loliondo kutibu magonjwa sugu. Misimamo mingine ni ya kiimani kwamba kama ni huduma hiyo inatolewa kwa imani kwa nini babu atoze hela sh. 500? Wenye msimamo huu wanarejea biblia pale yesu kristo aliposema mmepewa bure toeni bure. Kwa hiyo, wenye msimamo huu wanasema hiyo kasoro ni dalili tosha kuwa huduma ya babu haijatoka kwa mungu. Lakini vilevile, wapo wanaoipinga huduma ya babu siyo kwa imani bali kwa mtazamo tofauti kwamba hiyo ni biashara kama zilivyo biashara zingine tu. Hao wanasema babu ametumia ujanja wa kuweka gharama ndogo sana ya tiba ambayo ni sh. 500 lakini ana uhakika na msururu wa wateja utakaojaa kuitaka tiba hiyo unatosha kumfanya yeye awe tajiri pengine kuliko wote katika nchi hii. Hao wanasema hesabu za babu zimejikita katika uwingi wa watu wanaosumbuliwa na magonjwa ambayo babu ameyatangaza kuwa anatibu.
Ni jambo lililo wazi kuwa hivi sasa nchi yetu na pengine dunia nzima afya limekuwa ni suala linaloisumbua sana jamii. Magonjwa ya ukimwi, kisukari, pumu, kansa, n.k. Yanasumbua na kupoteza maisha ya watu wengi. Hali hii pengine kwa nchi yetu ni mbaya zaidi kutokana na huduma za afya kuwa duni sana. Na ndiyo maana viongozi takriban wote na wananchi wa kawaida wenye uwezo wamekuwa wakienda nchi za nje kufuata tiba bora. Sasa katikati ya hali hii anapojitokeza mtu wa aina ya babu akatibu wagonjwa na wagonjwa hao wakashuhudia hadharani kwamba wamepona tena siyo mmoja wala wawili, ni wengi, unatarajia mwitikio utakuwaje?
Ndugu zangu tusidanganyane tena tuache porojo. Inawezekana tunafanya hivyo kwa sababu tuna afya njema. Hatujui kuumwa maana yake ni nini. Kwa mtu ambaye miaka yote amekuwa akiumwa tena kuumwa haswa na amekuwa akiombewa na kupata tiba kila hospitali kubwa hapa nchini bila mafanikio, anaposikia wagonjwa wenzie wamepona unatarajia nini? Kwa nini nae asiende kujaribu kama alivyojaribu kwenye hizo hospitali na hayo maombi? Kwa nini aendelee kutegemea tiba ambazo miaka na miaka zimeshindwa kumponya?
Kuna shemeji yangu ambaye amekuwa akisumbuliwa na ukimwi kwa miaka takriban saba. Mkewe alifariki kwa ugonjwa huo. Sasa ni wikiya tatu tangu apate kikombe cha babu amecheki afya yake hospitalini yupo negative. Hospitali ya kwanza ilikuwa ni agakhan dar es salaam, ya pili ilikuwa ni regency na ya tatu ni burhan. Sehemu zote ni negative. Pia, kuna watu wameshuhudia wamepona kisukari, pumu na vidonda vya tumbo. Acheni wagonjwa waende bwana. Wanaokufa ni kutokana na uchivu wa safari ya njia ndefu na mbovu. Muhimu ni kwa ndugu kuhakikisha kuwa mgonjwa aliyezidiwa anaenda kwa babu huku akiendela na tiba.
Nadhani hii sasa ni too much manipulation ya ict! Nadhani itapelekea jammii forum kupoteza integrity yake. Wanajamii, let us post real and authentic issues