Imeniuma sana, mke wangu anatembea na baba yake mdogo

Imeniuma sana, mke wangu anatembea na baba yake mdogo

Pole sana hata kama vipi kwa kukujibu maneno hayo ni duh mbaya dana.

Muache zake aendelee na uroda, na usimpe nafasi kukuchezea maana atapigwa chini karibuni tu.

Muombe Mungu akuongoze upate mke mwema. Dah wanaume kama wewe wa kulea na familia pia sijui kwa nini wengi wenu hamnaga bahati na wake watarajiwa. Pole usirudi nyuma utakufa siku si zako
 
Unahangaika na kiporo wakati vya kupikwa vipo??!!!....
 
Izi nyingine zina jina lake haziwezi kuitwa ndoa
Ila sioni hata ushauri wa kukupa sbb jibu liko wazi hakutaki unamngangania wa nn sasa anza kusomesha mwingine ww si unajifanya baba wa mabinti wakubwa na kuchukua majukumu ya familia zao
 
Wanajamvi nimekuja na simanzi kubwa sana moyoni. Sijawahi kuumia kiasi hiki, maelezo ni marefu lakini ngoja nifupishe ili nisiwachoshe.

In short nina mke wangu nmeishi nae kwa mwaka 1 kama mke na mume. Ingawa mazingira ya kikazi yametufanya tuwe mbali kidogo lakini nmekuwa najitahid kufika kwake mara kwa mara sababu sio mbali sana(sisi ni watu wa Kanda ya Ziwa ki-makazi lakini sio kwetu).

Tatizo limekuja kuna tetesi nilipewa na dada yake kuhusu mahusiano kati ya mke wangu na mzee mmoja mwenye umri wa miaka 46. Mbaya zaidi ni baba yake mdogo na mke wangu ingawa walikwishatalakina na mkewe ambaye ni mama mdogo wa mke wangu kitambo kidogo kimepita.

Chanzo cha wao kukutana ilikua mke wangu ali carry somo moja apo UDSM ikabidi arudi kufanya hio course basi huyo mzee akamchukua aende nyumbani kwake amuangalizie wanae huku akienda chuo basi mchezo ukaanzia apo mzee kamrubuni mke wangu kuanza kutoka nae.

Kama mwanzo nilivoeleza, dada wa mke wangu aliniambia hicho kitu ila nikapuuzia sababu huwa na tabia ya uchonganishi pia huwa mahusiano yetu sio mazuri.

Nilichoamua nikafanya uchunguzi mwenyewe kwa njia zangu ninazozijua nikagundua ukweli. Mimi ni mtu wa IT basi nakaja kugundua hata baadhi ya vitu kama simu, camera, mavazi na pesa mke wangu analeta huwa vinatoka kwa huyo mzee maana nlikua napatwa shaka na spendings zake kulingana na kipato chake cha ualimu.

Basi tumeenda hivo lakini ndani kukawa na visa kikitoka hiki kinakuja kile ikafikia akaanza kuninyima sex anadai simfikishi wakati namjua vzuri na huwa namfkikisha, kwa hilo sina shaka hata tone.

Nikirudi nyuma kidogo mimi ndio nimemsomesha chuo tangu mwaka wa kwanza mpaka kamaliza na nimegharamika mambo mengi juu yake. Hapa tulipo tuna mtoto 1 wa kiume ana miaka 4 sasa.

Muda huu na andika post hii mke wangu yupo Dar, nimemuuilza yupo kwa nani hasemi. Nimeumia sana ikabidi niongeee na mama mkwe nikamueleza situation. Akampigia simu mwanae, kilichofuata akanitusi na kunitamkia maneno ambayo yamenichafua sana nafsi yangu.

Namnukuu "Unampigia simu mama akusaidie nini?, kama nato** si mimi wewe inakuhusu nini? Na nakuapia lazima nit**we huku ili utulie."

Imeniuma sana mpaka sasa moyo wangu umefunga siwez tena tena endelea nae ingawa nampenda na bila mimi asingekua hapo alipo leo" Nimejizuia sana kulipa kisasi nimeshindwa ukizingatia familia yao nimeibeba sana kwa mambo mengi.

Nikumbushe kitu, ukwel ni kwamba nilikuwa sijatoa mahari mpaka sasa ingawa tuliishi nae kama mke na mume. Lakini mpango ulikua mwezi huu na nilikua nimekwisha andaa kila kitu. Hata nashindwa nianze vipi kuwaeleza wazee.Nina mengi nimeyaruka kuyaeleza maana mimi si mwandishi mzuri. Natamani ningemsimulia mtu aandike.

Naomba ushauri wenu wadau na maswali pia kama yapo ila kama nitapata mtu wa kunipa njia nzuri ya kisasi nitafurahi.

Asanteni
1. Kama huna uwezo wa kumwacha usimfuatilie 2. Inawezekana humtoshelezi japo kuna wengine hata urushe maji godoro lote liloe bado atatoka tu, kwa maana ingine ile ni hobby 3. Tafuta mchepuko utakufa siku si zako. Asante kwa kunisoma
 
Mkeo anaenda kulea familia ya mtu mwingine?! Ulimruhusu awe bekitatu mwenyewe acha akudharau tu.
Gharama ulizotumia kumsomesha umeshindwa vipi kumlipia chumba/hostel?!
nli lipa chumba hicho kitu kulifanyika bila taarifa
 
Huyu mwanamke ni laana Kanitumia message tena wkt mm nme amua kumukalia kmya
form no where katuma hii tena
" Mi nilshoan wengi tu wanao jutia ila hawakupungukiwa kitu
Sion ajabu usipoteze muda kunitisha sana muda mrefu ety kukumbuka maan hata wee utakuja uona umuhimu wangu baadae"
 
angalia pale ulipojikwaa na usiangalie pale ulipoangukia. maisha ni safari yenye kuumiza kuliko kufurahisha. inawezekana pesa anayopewa ndiyo inayomzuzua na kukutusi. Usilie, kuumia wala kuamini kwenye ulipaji wa kisasi. mshtakie MUNGU na muachie mashtaka juu ya matatizo yako. kwani MUNGU hana uwezo wa kifichwa kitu na kiumbe chake. Simama futa vumbi tafuta mwingine safari yako iendelee
 
Kutokana na majibu yake ya sms, huenda wewe ulikuwa ukimuumiza kimapenzi na hivyo basi na yeye kaamua kulipa kisasi. Yawezekana wewe kumsomesha na kuwasaidia nduguze ndio kulikupa kiburi cha kuishi naye vile utakavyo bila kumpatia upendo wa dhati ukiamini kuwa hana uwezo wa kukuacha. Hebu jichunguze na wewe kwanza.
 
Hata kama unampenda vp piga moyo konde uachane naye.Tulia na ujipange upya juu ya suala zima la mahusiano,mchumba hasomeshwi wahenga walinena zamani.
 
Kutokana na majibu yake ya sms, huenda wewe ulikuwa ukimuumiza kimapenzi na hivyo basi na yeye kaamua kulipa kisasi. Yawezekana wewe kumsomesha na kuwasaidia nduguze ndio kulikupa kiburi cha kuishi naye vile utakavyo bila kumpatia upendo wa dhati ukiamini kuwa hana uwezo wa kukuacha. Hebu jichunguze na wewe kwanza.
nakiri nisha wahi mkosea lkn cio kwa perception ya kiburi cha kumsomesha wala msaada ila nliomba radhi yaka pita, all the way unawezaje kuishi na mtu wa ivo?
 
Pole sana,kwanza tulia utafakari kabla ujafanya maamuzi yoyote
 
Sasa mkuu unataka ushauri gani? Mpe talaka .. Uzinzi si kitu cha kuvumilia kwenye mahusiano..
 
dawa yabishooo kuwa bishoo zaidi yake...kama ana mdogo wake jivutie weka ndani..yy. analiwa na ba mdogo wewe unakula dada mdogo kitu mali kwa mali wala ukoo haujaenda mbali alafu wala cyo kisasi hicho
 
pole sana ndugu yangu ila avatar yako kiboko aisee sijui ungeibadili kidogo
 
Back
Top Bottom