Sikujua kuwa watu hawanipendi kiasi hiki, wamenifitini mtani ninakokaa na kazini. Yaani wamemtafuta mwenyenyumba yangu nilikopanga na kumjaza maneno ya uongo, mwenye nyumba kaja leo alfajiri kaniambia nitafute nyumba kwingine baada ya miezi 3 nimrudishie nyumba yake, Akaondoka kodi yangu ilikuwa inaisha mwezi ujao hapa nilikuwa najipanga nimpelekee kodi ndo haya yamenifika. Nawaza jinsi ilivotabu kupata nyumba inayokidhi viwango......
Kufika kazini nikiwa na mawazo kibao nikaitwa na bosi daaah, nimepewa lawama za uongo si mimi niliyefanya hayo nikajaribu kumueleza bosi kuwa hayo ni makosa ya secretary na watu wa idara ingine bosi kamaka na kusema ripoti zote zinaonesha mimi ndo nimesababisha ofc ikakosa hiyo tenda na hivo kusababishia kampuni loss. Daaah nimeumia na nimevunjika moyo wa kufanya kazi mnoo.