Imeletwa Posa!

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,810
15,398
Huyu Binti kaniomba msaada, Naomba wana JF mumsaidie:

Huyu jamaa anaishi Oman ana mke na watoto wawili. anataka kunioa niwe mkewe wa pili (Mitala) na nikaishi naye huko.

Baba kaniambia niamue mwenyewe, na hivyo nimeikataa hiyo posa, lakini huyu kaka yangu mkubwa kanishupalia niolewe, kisa kaahidiwa kutafutiwa kazi Uarabuni.

mimi nimekataa kabisaa, na sasa hapa nyumbani kuna vuta nikuvute kuna wanaosema niolewe kuna wanaopinga, kwani mie nataka mwakani niendelee na masomo.

Eti Mzee Mtambuzi nisaidie nifanyeje?
 
Hakuna kitakacho kusaidia zaidi ya shule,kuolewa hakwishi ukiwa na elimu wanaume utanunua unaemtaka,huyo kakako mwambie asikufupishie maisha, huyo bwana mkewe keshamzalia watoto wawili sasa anakutaka wewe ukamzalie Kima au Tembo? wasikushughulishe na Oman wala Dubai soma mwanakwetu...
 
Kama wewe mwenyewe umekataa basi ki msingi safari ya Oman hapo haipo!Kama umekataa kwa dhati kwa sababu ambazo wewe unaona ni za msingi kwa mustakabali wa maisha yako utabaki kuwa sahihi daima.

Simamia katika msimamo wako maana hayo ni maisha yako.Huyo kaka yako kisebengo mwambie aende yeye Oman. Ila usome kweli!
 
Hakuna kitakacho kusaidia zaidi ya shule,kuolewa hakwishi ukiwa na elimu wanaume utanunua unaemtaka,huyo kakako mwambie asikufupishie maisha, huyo bwana mkewe keshamzalia watoto wawili sasa anakutaka wewe ukamzalie Kima au Tembo? wasikushughulishe na Oman wala Dubai soma mwanakwetu...

Ahsante mkuu, nataka kkusanya maoni ili nijue nitamshauri nini huyu Binti.....................
 
Hauwezi kuolewa kisa kaka apate kazi,au shangazi anataka au sijui nani!Kiukweli hao hawakupendi,wanakuona kama bidhaa tu,shukuru umepata picha ya ndugu zako!Ukiamua uolewe hautakua na furaha!

Fanya maamuzi ya faida kwako na wanaokuzunguka hata kama kuna baadhi watachukia!
 
Nimekumbuka nilichoambiwa na babu yangu; Emotional Bribe or rape!yaani huyo mchumba feki wako anabaka hisia zako kwa kucheza na watu wako wa karibu.anawahonga kwa kujifanya yeye ni mwema na ana nia nzuri na maisha YENU wewe na familia yako na kwa kufanya hivi anaziteka hisia za ndugu zako ambao anategemea kuwatumia pasipo wao kujua kukushawishi umkubali.

Nakwambia mdogo wangu when it comes to maisha ya ndoa hakuna kitu kiitwacho faida yetu (wewe na familia ya wazee wako) bali kuna kwa faida YANGU mimi kama muolewa/muoaji. Za mbayuwayu changanya na....
 
Olewa ili kaka yako apate kazi. Watu wapo tayari kuua ndg zao ili wapate hela wewe kuolewa tu unakataa!

We nenda acha ujinga, Elimu yenyewe haitabiriki.
 
hivi bado watu wanauziwa mbuzi kwa gunia eh? huu mwaka gani tena,nshasahau!kha!:rant::hatari::rant:
 
Olewa ili kaka yako apate kazi. Watu wapo tayari kuua ndg zao ili wapate hela wewe kuolewa tu unakataa!

We nenda acha ujinga, Elimu yenyewe haitabiriki.

Ah we Mzee kesho na keshokutwa akirudi hapa na kilio cha kunyanyaswa na mume utamsema kwa nini alidanganyika na Dubai!!
 
Mitala yataka moyo!!!

Mimi namshauri aendelee kukataa kwa nguvu zote, mwambie aendelee na masomo na ajitahidi Mungu atampa mume mwema!
 
Huyu Binti kaniomba msaada, Naomba wana JF mumsaidie:

Huyu jamaa anaishi Oman ana mke na watoto wawili. anataka kunioa niwe mkewe wa pili (Mitala) na nikaishi naye huko.
Baba kaniambia niamue mwenyewe, na hivyo nimeikataa hiyo posa, lakini huyu kaka yangu mkubwa kanishupalia niolewe, kisa kaahidiwa kutafutiwa kazi Uarabuni.
mimi nimekataa kabisaa, na sasa hapa nyumbani kuna vuta nikuvute kuna wanaosema niolewe kuna wanaopinga, kwani mie nataka mwakani niendelee na masomo.

Eti Mzee Mtambuzi nisaidie nifanyeje?

vitu vidogodogo kama hivi, kulipa ada ya watoto, kusimamia mashamba na miradi mbalimbali anafanya mke wangu. Mi niko busy na kusuluhiisha migogoro ya mashariki ya kati, na pia kuokoa uchumi wa ulaya unaodorora kwa kasi.
 
Ah we Mzee kesho na keshokutwa akirudi hapa na kilio cha kunyanyaswa na mume utamsema kwa nini alidanganyika na Dubai!!

hapo namshauri aende kwa machale. Ina maana hajipeleki mzima mzima. Lengo ni bro wake apate kazi.
 
uwe unaanza na tahadhari kaka,mwanzoni nilidhani wewe ndio wataka kuolewa,roho ikanilipuka!ngoja nikanywe maji baridi niishushe kwanza
 
uwe unaanza na tahadhari kaka,mwanzoni nilidhani wewe ndio wataka kuolewa,roho ikanilipuka!ngoja nikanywe maji baridi niishushe kwanza
Hahaha ukajua bunge lishampitisha Cameron. Na sheria ishaanza kutumika. Nalog off
 
mtetezi mkubwa wa wanawake siku izi ni elimu ivo asiache mtetezi wake(elimu) na kukimbilia kuolewa ambako hata akipata shida hawezi kujiengua kisa hana pakujishikiza (nguzo hana ambayo ni elimu aliyoikimbia mwanzo)
 
uwe unaanza na tahadhari kaka,mwanzoni nilidhani wewe ndio wataka kuolewa,roho ikanilipuka!ngoja nikanywe maji baridi niishushe kwanza

Niliamua niiweke kama mletaji alivyoituma. ukweli ni kwamba nilikuwa nimeandaa ushauri wa kumpa, lakini nimeona ni vyema nichanganye na za wana JF, nikiamini kwamba nitapata mseto mzuri wa ushauri, ili kumuepusha binti huyu na kisirani hiki cha ndoa ya kulazimishwa..................
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom