Ukiona una bahati mbaya kimapenzi, basi unamajini. Au laana uliofanya hapo mwanzo.

Somoe

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
754
282
Historia yangu ni ndefu, ila nafupisha kadri iwezekanavyo. Nikiwa na umri wa miaka 17, nikatiwa mimba, alie nitia mimba alitaka kunioa, nilimkataa kwa sababu miguu yake mirefuu sana, na macho yake kama goroli, nilimkubali kwa sababu binamu yake alinishawishi. Basi Yule jamaa alie nitia mimba akashauriwa amuoe ndugu yangu, mtoto wa baba yangu mkubwa, ndoa ikafungwa, mie sikujari. Muda si mrefu nami nikaolewa na mwenye pesa nyingi sana, ambae sikumpenda kama kimapenzi au mume, ila nilimpenda kama binadam tu, kufanya mapenzi lazma tugombane kwanza. Tukifanya mapenzi mara 1 kwa wiki, au mara 4 kwa mwezi. Mungu nisamehe maana njaa ikanisababishia niolewe nae, jamani, maana nilivo mkataa alie nitia mimba nikatimuliwa nyumbani. Nilikua sina pa kushika. Babu yangu aliposikia nimeolewa na kajitu flani, akaniroga nisiolewe tena, ndoa yangu ile ikavunjika ghafla, sikujari kama kawaida yangu, wanaume si wengi tu. Mwezi tu baada ya ndoa kuvunjika nikapata mpenzi mwingine mimba ingine ikaingia tena, nikagundua huyu jamaa anaupungufu wa akili lakini nilitaka mwenyewe, nae ghafla tuka achana. Miaka 22, kijana, ninawatoto 2 kila mtoto na baba yake, na wote nje ya ndoa. Kutoka hapo sikutaka mwanaume tena, na wala swala la kuolewa halikuwepo kichwani mwangu. kila alie jitokeza kunipenda na kutaka kunioa nilimtukana na kumdharau, leo nikikumbuka naona huruma. Nikanunua DILDO, hivo nikiitaji kufanya mapenzi najisugua nalo, na kuna wakati mwingine ilikua naota ndoto nafanya mapenzi na mwanaume ninae mpenda sana, hivo ikawa sitaji mume. Mwaka 2010, nikawa na hamu ya kuzaa tena, ili niwe na watoto 4, nikafunga ndoa na mtu nisie mjua, tulikutana mtandaoni, mungu wangu, sijui ndio mpango wa shetani alinilaani, ikanifanya nianze kumkumbuka alie nitia mimba nikamkataa kisa tu eti miguu mirefu, lakini alikua na lugha tamu, mwenye heshma na mwenye busara kijana wa watu, nikajiona laana hii imenifika, sikumjua mungu. Sio hapo tu, niliefunga nae ndoa alinipa pesa nyingi na kunisaidia na mtoto wangu mgonjwa, sikumjari, nilikuwa najifikiria mwenyewe. Na walio nipenda kweli na kunisaidia niliwadharau, leo navamia walaghai, nikaamini kuwa ni kweli sio kila mwanaume anafaa kuwa mume, wengine akili za kupewa, hasie funzwa na ***** ufunzwa na ulimwengu.


Nikagundua labda mungu alitaka kunionesha, maana mimi nilikua bingwa wa kuwafanyia wanaonipenda mabovu, yakanirudia. Nikaomba omba mungu pale anisamehe na najua makosa yangu, nikalia lia. Nikaanza kuswali, akili yangu ikatulia. Lakini swala la kuolewa sitaki tena, mikosi gani hii tena, nimelaanika teyari, walio nipenda niliwadharau na kuwakataa, nilipotaka mume nilivamia hamnazo. Rafiki yangu mmoja akaniambia ndege mjanja unasa kwenye tundu mbovu.


Mwaka ukapita, hadi mwaka 2013, mtu mmoja tulikuwa marafiki wa siku nyingi, siku akaniomba nikamtembele, akapika chakula kizuri, tukala tukanywa, ghafla tukafanya mapenzi, ndio hapo hapo tukawa wapenzi, nikaanza kuota ndoto anachinja watu, mara ananikaba, ananiua, nikawa sitaki kuonana nae, tukawa tunagombana, kuna siku akaniambia "tell me baby" you know I love you so much baby. You are so nice, tatizo lako lolote niambie nipo teyari kulipokea, usiwe na wasi. Basi nikamuambia naota anachinja watu nk, akaniambia huyo ni pepo. Kila siku ugomvi, hatuelewani, akaniambia kama haya mapepo yangu siku yatoa, mapenzi yetu hayato dumu, ikawa namtukana, na kufanya nae mapenzi sitaki, nikamtuhumu kuwa yeye ni mshirikina na anamini mambo hayapo.

Vuta nikuvute mwisho nikakubali. Wakaniombea haikuchelewa majini yakapanda na yakasema sitoweza kuolewa au kuwa na mume, majini yakaendelea kukasema nimerogwa na babu yangu, na wao majini ndio yametumwa wanifunge akili, nisau ndoa, na yavunje ndoa zangu na uhusiani wangu na nichukie wanaume na niwadharau ili wakimbie wenyewe.

Mimi ni muislam lakini kwa yalio nitokea nikaokoka haraka sana, mpaka anoiting water ya Tb joshua nikapuliziwa, majini yamekimbia. Sasa najiuliza hivi nilikua mimi kipindi kile? Lakini nimesoma katika kitabu kimoja, kinasema mtu akiwa na majini iwe umetupiwa au umeyakwaa sehemu, huyo mtu atakua na matatizo ya ndoa, au uhusiano. Majini yatakusababishia umpende mtu mbovu au mtu hasie faa, yaani utavutiwa kimapenzi na mtu mwenye majini kama wewe mwenyewe, ili wewe umuone mbovu na yeye akuone mbovu, ili iwe ngumu kusaidiana na musidumu, ndio ujanja wa majini

Hivo ukiona kila unae mpenda ni mbovu, au utajiona una bahati mbaya basi jua unamajini. Majini yanakusababishia uchague wabovu tu kila mara. Kuhusu pesa na uchumi, mwanamke unaweza kuchuma mali nyingi sana, ili husiitaji mwanaume wa kukusaidia, au wa kuishi nae ili majini yakutawale. Na mwanaume uwa wanamikosi mikosi na kuyumba kiuchumi, ili wasipendwe na wanawake.

Tafadhali wasaidieni wapenzi wenu, mie nimepata mwanaume mwenye busara na mwenye akili timamu na anae mjua mungu jamani, kanisaidia. Amevumilia matusi yangu, dharau zangu, alikaa kimya kijana wa watu. Hajawai kunidhalilisha wala kunisema kwa marafiki zake, halafu nimemfanyia mabovu mengi aibu hata kusimulia. Kuna wakati nikifoka akisinyaa akishika moyo wake kama anataka kulia. Alisema ipo siku yataisha tu. Kanimbia wimbo wa samaki akioza usimtupe, mnunulie ndimu umkaushe. Nimelewa maana yake ingawa sikusema kitu karibu nilie, asante mungu. Ukimuona mpenzi wako haeleweki mpeleke akaombewe, uenda karogwa au ameyavaa majini. Nilikua siamini majini wala uchawi, ila sasa nimeamini. sasa naishi kwa amani na upendo, he is my king, sasa akienda bafuni kuoga na mimi nakaa huko huko, kila alipo nami nipo. Nilikua sijui kupenda ila sasa najua jamani, naomba mungu anisamehe kwa makosa yote niliofanya. Ukimuona mtu anavua nguo usimseme vibaya na kumkimbia, tafuta nguo umvishe na tafuta msaada, kanivumilia miaka 3 na nusu, eh mungu mbariki, asanteni kwa kusoma yalionikuta
 
Hongera yako, hata siku moja: Mungu hawezi kukutanisha vitu ambavyo vimekamilika! La ha shaa!, watu mnajibebesha mizigo bure, eti namtaka mtu ambaye......, mara ajiheshimu....mara... yaani mambo kibao. Mnasahau kwamba ili mdumu zaidi mnahitaji kufundishana na kuonyana kila siku ndani ya ndoa zenu, maana kila mmoja anakuja na mapungufu yake. Mke kama hajui kupika basi mueleze maana inawezekana tangu utoto wake alikuwa anasoma shule alafu nyumbani kulikuwa na house girl, ndoa zinakuwa ngumu kwasababu kila mmoja anafikiri nikimpata yule nitafanikiwa maana anaonekana hana shida; lakini akiingia ndani akawa mke utaanza kusema afadhali ningeoa shetani!. Hongera yako dada maana umefunguliwa; umeijua kweli na hata sasa uko huru!
 
Back
Top Bottom