Ni kuhusu mjomba wangu.
Ni kijana mwanaume wa miaka 19.
Mwaka jana mwezi wa saba aliiba shilingi milioni moja na nusu nyumbani kwao.
Aliitumia ndani ya wiki moja na kuimaliza.
Alishikwa akapelekwa central,akakaa kama wiki mbili hivi.
Dada yangu alikuwa na mawazo hadi blood psessure ilikuwa ikipanda.
Kwa upendo aliokuwa nao dada yangu kwa mwanae walimtoa central na kumsamehe.Lakini leo kaiba tena laki moja nyumbani kwao.
Dada amekuwa na mawazo sana akijuta kumzaa.
Kama ni shule kijana huyo akiulizwa anasema bado anataka.
Dada amempeleka kwenye maombi lakini bado habadiliki.
Anaomba ushauri wenu kwan kama kumpenda anampenda sana lakini ndo hivyo anampa hasara....
Asikate tamaa na maombi kwasbb atabadilika tu kupitia maombi,kuna mtoto huku nafikiri kabla hata ya kufikisha miaka 16 aliwahi kuiba iba sana na baya zaidi alishamuua mwenzie kwa kumchoma kisu tumboni,mama yake wa kambo aliamua kumweka kwenye maombi na sasa huyu kijana yupo very decent,anasoma na anafanya vizuri sana darasani.akikata tamaa kumuombea ni kumpa shetani nafasi.Pia ajitahidi kuficha pesa vizuri ikiwezekana aweke kwenye Mpesa au bank.
Mwombeeni tu kwa Mungu muweza wa yote! Yupo kwny ukuaji huyo ataacha mwenyewe mi kakaangu mpaka ilifikia tukahisi amerogwa maana yy alikua zaidi ya huyo bt kwa huruma za Mungu aliacha mwenyewe!
asante sana mkuu.god bless you!
Heh! Kama kila kitu kiko sawa basi ana mapepo!!kuhusu ushauri tumemshauri sana.kwa upande wa makundi wala hakuna rafiki yake ambaye ni mwizi.
hata mimi sijui ana tatizo gan.kama ni bangi havuti.sembe hatumii.mademu wala hana kabisa.namjua vizur sana..
Sasa pesa yote hiyo anaifanyia nini kwa kipindi kifupi hivyo?
...anatamani hata huyo mtoto afe..
I doubt it. Si kweli.
its true.mama yake alisema hivyo.
aachwe aendelee kuipa familia yake hasara?