Imekuwa matatizo sasa...

Dr.viruz

Senior Member
May 28, 2013
123
195
Ni kuhusu mjomba wangu.

Ni kijana mwanaume wa miaka 19.

Mwaka jana mwezi wa saba aliiba shilingi milioni moja na nusu nyumbani kwao.

Aliitumia ndani ya wiki moja na kuimaliza.

Alishikwa akapelekwa central,akakaa kama wiki mbili hivi.

Dada yangu alikuwa na mawazo hadi blood psessure ilikuwa ikipanda.

Kwa upendo aliokuwa nao dada yangu kwa mwanae walimtoa central na kumsamehe.Lakini leo kaiba tena laki moja nyumbani kwao.

Dada amekuwa na mawazo sana akijuta kumzaa.

Kama ni shule kijana huyo akiulizwa anasema bado anataka.

Dada amempeleka kwenye maombi lakini bado habadiliki.

Anaomba ushauri wenu kwan kama kumpenda anampenda sana lakini ndo hivyo anampa hasara....
 
JJ10

JF-Expert Member
Jan 13, 2014
282
0
Wewe umemshauri nini? Kingine kumpenda mtoto sana' na yeye akajua kwamba unampenda matokeo yake ndo hayo!!

Avae sura ya Mbuzi' amtupe ndani hata miezi miwili' then akirudi amkanye na ampe shughuli yakumpatia miambilimiambili itampunguzia tamaa na ataweza kupata anachokitamani bila kuiba..

Kingine yawezekana wewe ndo linakuuma hilo kumbe mjombaako anachukua na haibi kama wewe ulivyochukulia' akijua hii pesa ya mama! Na mamayake anachukulia poa ingawa' anataka kuwaonyesha kwamba anaumia kumbe hayo maumivu hayapo moyoni! So liangalie hilo pia'
 
MankaM

JF-Expert Member
Apr 20, 2013
9,456
1,500
anapenda good laifu wakati hana uwezo huo harafu inategemea mazingira alolelewa kama alizoeshwa kupewa mpunga na ikatokea amesitishiwa hiyo huduma hapo msimlaumu huyo bado kijana mdogo sana asa anasa ndio zitamuua anabahati anaiba za nyumbani kwao lakin akiingia uswahilini hakika atarudi na ngeu
 
Dr.viruz

Senior Member
May 28, 2013
123
195
Wewe umemshauri nini? Kingine kumpenda mtoto sana' na yeye akajua kwamba unampenda matokeo yake ndo hayo!!

Avae sura ya Mbuzi' amtupe ndani hata miezi miwili' then akirudi amkanye na ampe shughuli yakumpatia miambilimiambili itampunguzia tamaa na ataweza kupata anachokitamani bila kuiba..

Kingine yawezekana wewe ndo linakuuma hilo kumbe mjombaako anachukua na haibi kama wewe ulivyochukulia' akijua hii pesa ya mama! Na mamayake anachukulia poa ingawa' anataka kuwaonyesha kwamba anaumia kumbe hayo maumivu hayapo moyoni! So liangalie hilo pia'

mkuu kama kuuma inamuuma sana dada.hadi sasa bado tu anahuzunika.anatamani hata huyo mtoto afe..
 
JJ10

JF-Expert Member
Jan 13, 2014
282
0
mkuu kama kuuma inamuuma sana dada.hadi sasa bado tu anahuzunika.anatamani hata huyo mtoto afe..

Anatamani afe kwaajili ya laki moja? Au milioni na laki 1? Mwambie asikufuru' amtengenezee mazingira ya yeye kujipatia miambilimiambili!! Maana itakuwa alimzowesha kumpatia' then akakata ghafla.
 
Dr.viruz

Senior Member
May 28, 2013
123
195
Anatamani afe kwaajili ya laki moja? Au milioni na laki 1? Mwambie asikufuru' amtengenezee mazingira ya yeye kujipatia miambilimiambili!! Maana itakuwa alimzowesha kumpatia' then akakata ghafla.

wala hakuwa akimpa pesa.kuhusu tabia yake pia ni mwenye kiburi na jeuri.amepigwa mara nyingi sana lakini bado haachi.
 
Ennie

JF-Expert Member
Jan 15, 2011
7,140
2,000
Poleni.
Haiwezi kuwa imeanza ghafla hivyo,malezi ya kijana yalikuwaje?
At 19 kijana anakuwa na mahitaji ya kiasi fulani cha pesa,anakipataje ni kwa family kuamua ila kama hasomi wala hana ajira anaweza kutafutiwa kamradi akakuze mwenyewe.
Umemtaja sana dada yako ambaye ni mama wa mtoto,baba wa mtoto yuko wapi?
Anafanya nini kukpomesha hili?
Udongo upate ungali maji..........
 
Dr.viruz

Senior Member
May 28, 2013
123
195
siunajua wanaume walivyo.baba amekasirika sana hatak mchezo anataka mtoto akae central kama miezi miwili.
 
Dr.viruz

Senior Member
May 28, 2013
123
195
Poleni.
Haiwezi kuwa imeanza ghafla hivyo,malezi ya kijana yalikuwaje?
At 19 kijana anakuwa na mahitaji ya kiasi fulani cha pesa,anakipataje ni kwa family kuamua ila kama hasomi wala hana ajira anaweza kutafutiwa kamradi akakuze mwenyewe.
Umemtaja sana dada yako ambaye ni mama wa mtoto,baba wa mtoto yuko wapi?
Anafanya nini kukpomesha hili?
Udongo upate ungali maji..........

kuhusu malezi kalelewa vizuri sana kwan baba na mama yake wameshika dini sana.
 
HARUFU

Platinum Member
Jan 21, 2014
28,283
2,000
Mpe pole dada yako na kwa pamoja poleni sana.

Nina wasi wasi mbali na starehe za wachumba isijekuwa ameanza kula sembe, mfuatilieni nyendo zake kwa ukaribu.

Afanye starehe zote lakini sembe, zidini Ombeni Mungu asifike huko
 
mrsleo

JF-Expert Member
Jan 13, 2014
2,472
2,000
Mpe pole sana dada yako kaka yangu alikuwa hvyo aliwasumbua sana wazazi, alipigwa sana, amewekwa sana segerea lakn haikusaidia, mwisho wa siku walipooba haina jinsi akatimuliwa nyumban. Tunamshukuru Mungu ghafla tu alikuja kubadilika akaachana na uchafu wote na sasahv ana maisha yake na familia yake, kwa kweli hatukutegemea ni Neema tu ya Mungu. Kwahyo hata huyo ikimpendeza Mungu atambadilisha tu kwa experience yangu huwa hakuna jinsi
 
HARUFU

Platinum Member
Jan 21, 2014
28,283
2,000
kuhusu malezi kalelewa vizuri sana kwan baba na mama yake wameshika dini sana.
Mkuu dini sio sababu, unaweza lelewa maadili ya dini au naweza sema unatokea kwenye familia yenye maadili ya dini lakini utakapokua kiumri unapoteza mwelekeo au unakiuka miiko ya familia
 
Dr.viruz

Senior Member
May 28, 2013
123
195
Mkuu dini sio sababu, unaweza lelewa maadili ya dini au naweza sema unatokea kwenye familia yenye maadili ya dini lakini utakapokua kiumri unapoteza mwelekeo au unakiuka miiko ya familia

mkuu hebu fikiri angekuwa mwanao halaf amefikia hatua hii,ungefanyaje?
 
Dr.viruz

Senior Member
May 28, 2013
123
195
Mpe pole dada yako na kwa pamoja poleni sana.

Nina wasi wasi mbali na starehe za wachumba isijekuwa ameanza kula sembe, mfuatilieni nyendo zake kwa ukaribu.

Afanye starehe zote lakini sembe, zidini Ombeni Mungu asifike huko

hata mimi sijui ana tatizo gan.kama ni bangi havuti.sembe hatumii.mademu wala hana kabisa.namjua vizur sana..
 
Ennie

JF-Expert Member
Jan 15, 2011
7,140
2,000
kuhusu malezi kalelewa vizuri sana kwan baba na mama yake wameshika dini sana.

Inawezekana makundi na ujana vinamsumbua,mtafutieni Counselor aongee naye.
Msiache kumuombea pia,kwa rehma za Mungu atabadilika tu awe mtoto mwema.
Poleni.
 
mwekundu

JF-Expert Member
Mar 4, 2013
21,774
2,000
Huyo nawashauri muacheni tu kama alivyo akutane na wababe huko wamle tigo ndo atakoma
 
Dr.viruz

Senior Member
May 28, 2013
123
195
Inawezekana makundi na ujana vinamsumbua,mtafutieni Counselor aongee naye.
Msiache kumuombea pia,kwa rehma za Mungu atabadilika tu awe mtoto mwema.
Poleni.

kuhusu ushauri tumemshauri sana.kwa upande wa makundi wala hakuna rafiki yake ambaye ni mwizi.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom