Imekuwa matatizo sasa...

Ni kuhusu mjomba wangu.

Ni kijana mwanaume wa miaka 19.

Mwaka jana mwezi wa saba aliiba shilingi milioni moja na nusu nyumbani kwao.

Aliitumia ndani ya wiki moja na kuimaliza.

Alishikwa akapelekwa central,akakaa kama wiki mbili hivi.

Dada yangu alikuwa na mawazo hadi blood psessure ilikuwa ikipanda.

Kwa upendo aliokuwa nao dada yangu kwa mwanae walimtoa central na kumsamehe.Lakini leo kaiba tena laki moja nyumbani kwao.

Dada amekuwa na mawazo sana akijuta kumzaa.

Kama ni shule kijana huyo akiulizwa anasema bado anataka.

Dada amempeleka kwenye maombi lakini bado habadiliki.

Anaomba ushauri wenu kwan kama kumpenda anampenda sana lakini ndo hivyo anampa hasara....

Asikate tamaa na maombi kwasbb atabadilika tu kupitia maombi,kuna mtoto huku nafikiri kabla hata ya kufikisha miaka 16 aliwahi kuiba iba sana na baya zaidi alishamuua mwenzie kwa kumchoma kisu tumboni,mama yake wa kambo aliamua kumweka kwenye maombi na sasa huyu kijana yupo very decent,anasoma na anafanya vizuri sana darasani.akikata tamaa kumuombea ni kumpa shetani nafasi.Pia ajitahidi kuficha pesa vizuri ikiwezekana aweke kwenye Mpesa au bank.
 
Mwombeeni tu kwa Mungu muweza wa yote! Yupo kwny ukuaji huyo ataacha mwenyewe mi kakaangu mpaka ilifikia tukahisi amerogwa maana yy alikua zaidi ya huyo bt kwa huruma za Mungu aliacha mwenyewe!
 
asante sana mkuu.god bless you!
 
Mwombeeni tu kwa Mungu muweza wa yote! Yupo kwny ukuaji huyo ataacha mwenyewe mi kakaangu mpaka ilifikia tukahisi amerogwa maana yy alikua zaidi ya huyo bt kwa huruma za Mungu aliacha mwenyewe!

asee!.kilichobaki ni kumuombea kwa mungu tu!
 
Sio ushauri kwa dada tu hata kwa wale ambao wanatarajia kupata watoto hauwezi kumpenda mtoto kwa hali ya juu hata kama una kipato kiasi gani kimtazamo hapa huyu dada alianza kumzoesha mwanae hela nyingi za matumizi tupunguze haya matatizo yapo mengi sana
 
Huyo kijana lazima alianza kidogo kidogo wazazi wane wanapotezea

Kumtoa central tu kunampa kiburi kijana kuwa hamwezi kumfanya lolote

Hapo kijana anatakiwa atafutie adhabu mujarabu ya kukomesha tabia hiyo
 
huyo ni mtoto mtukutu tu hata angezaliwa na askofu.kunaweza kusiwe na makosa katika malezi au yakawepo. Kuna tabia za kuzaliwa nazo ambazo mazingira hayazibadilishi ndo maana watoto mapacha wa mfuko mmoja mmoja anaweza kuwa daktari mwingine akawa kibaka. Huyo kwa umri wake wamkubali tu kama alivyo, wampende hivyo hivyo mpaka itakapotangazwa vinginevyo. hela hata zikifichwa wapi ataiba vitu, akikosa cha kuiba nyumbani ataiba popote.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom