Imani za kishirikina

o_2

JF-Expert Member
Jul 20, 2017
348
287
Kwako ndugu jamaa na rafiki popote ulipo,

Maisha ni mtihani ambao kufaulu kwake kupo mwisho wake. Mwisho wa maisha ni kifo. Kifo ni fumbo kama tujuavyo, hakuna anayejua muda wala saa wapi kifo kitakukuta. Japo inasemekana wapo ambao wanaonyenshwa vifo vyao.

Maisha ni makatili sana kila wakati. Unaweza ukawaza kwanini mimi nipo hivi kwanini yule yupo vile. Kwanini mimi masikini kwanini yule ni tajiri vyoote hivyo vina mwanzo wake.

Nirudi kwenye kichwa hapo juu imani za kishirikina. Kwa kifupi kabisa hii dunia ina maajabu sana. Wapo wakristo, wasabato, wapagani, waislam, mabudha n.k. Wote hao kuna kitu wanakiamini kuendana na imani zao lakini kwenye mambo ya kishirikina anaweza kushiriki muumini yoyote wa dini na madhehebu ambayo nimeyataja hapo.

Wapo wakristo wanga, waislam wanga na wasabato wanga. Wapagani sina uhakika sana. Na kila kitu cha kushirikiana kinachofanyika kina matokeo yake haijalishi.
Jana nilikutana na kisa kimoja. Kwenye jamii tunayoishi yapo mambo ya ajabu sana.

Mida ya jioni kwenye saa moja saa mbili hivi usiku nilikutana na kioja kimoja. Nilienda kutazama EPL mechi ya Aston Villa dhidi ya Manchester City. Wakati wa mapumziko nikasema niende ghetto mara moja kwani mahali banda la mpira lilipo sio mbali saana na mahali nimepanga. Bwana wewe!

Nimefika nikakuta kijana mmoja yupo na mganga wa kienyeji. Tunguli, kichwa cha mbuzi, madawa dawa mengine kioo na unga. Mama mwenye nyumba alikuwepo pia hapo eneo hilo.

Nikapatwa na mshangao! Kulikoni tena?? Akaniambia wala usiogope, dunia ina watu wabaya sana.

Nikamjibu wala siogopi nikaendelea na kilichonirudisha baadae wakati natoka kuelekea kumalizia kipindi cha pili nikaona kuna kitu kinachomwa na moto wa wastani unawaka.

Sikujali, nikaenda zangu.

Sasa kwa vyovyote vile lazima athari itakuwepo. Kwasababu naamini chochote kile utakacho kifanya lazima kinamatokeo yake. Kama kuna mtu alikuwa anakaangwa basi nimpe pole popote huko alipo na Mungu amsaidie.

Tunaishi nao.
 
Back
Top Bottom