Imani kubwa ya Wachina kwa Serikali yao imethibitisha nini?

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,034
dcc451da81cb39dbaf3c18c77f10c12daa1830b6.jpeg

Shirika kubwa zaidi la mahusiano ya umma duniani la Edelman, hivi karibuni limetoa ripoti ya mwaka 2022 ya “Edelman Trust Barometer”, ikionesha kuwa imani ya Wachina kwa serikali yao imefikia 91%, na kushika nafasi ya kwanza duniani.

Katika miaka ya karibuni, nchi za Magharibi zimekuwa zikiipaka matope serikali ya China, na kusema inapuuza haki za wananchi wake, lakini kwa nini Wachina wanazidi kuiamini serikali yao kuliko watu wa nchi za Magharibi, chanzo chake ni nini, na inathibitisha nini?

Mwaka 2017 na 2018, serikali ya China ilishika nafasi ya kwanza katika orodha ya “Edelman Trust Barometer” kuhusu imani ya watu kwa serikali yao. Mwaka huu, kwa mara nyingine tena, serikali ya China imeshika nafasi ya kwanza kwa alama ya asilimia 91, ambalo ni ongezeo la asilimia 9 kuliko mwaka uliopita, na ni kiwango cha juu zaidi katika mwongo mmoja. Kinyume kabisa na China, asilimia 39 tu ya Wamarekani ndio wana imani kwa serikali, pengo kati ya nchi hiyo na China limekuwa kubwa zaidi tangu kuanzishwa kwa ripoti hiyo ya Edelman.

Matokeo haya yanaweza kuwa jambo ambalo wanasiasa wa baadhi ya nchi za Magharibi haswa Marekani hawataki kuyaona, kwani mara kwa mara wanachochea mvutano katika uhusiano kati ya serikali ya China na wananchi wake, na hata wanatarajia “mapinduzi ya rangi” kutokea nchini China. Ripoti hiyo ya Edelman imewashangaza, kwa nini Wachina wana imani kubwa namna hii kwa serikali yao, na hii inamaanisha nini?

Imani kubwa ya Wachina kwa serikali yao inatokana na utekelezaji wa pande zote wa wazo la kiutawala la serikali inayoongozwa na Chama cha Kikomunisti cha China, ambalo linazingatia zaidi wananchi, ambapo inaonyesha kuwa, serikali ya China ni serikali halisi inayosimamia kikamilifu maslahi ya watu. Rais Xi Jinping wa China amesisitiza mara kwa mara kwamba, “matumaini ya watu ya kupata maisha bora ndio lengo letu.” Serikali ya China inazingatia maslahi ya watu, inazingatia uboreshaji na ustawi wa maisha ya watu, na wakati wote imejitolea kuhakikisha usalama na utulivu wa maisha ya watu. Tangu kutokea kwa janga la COVID-19, tofauti na baadhi ya nchi za Magharibi ambazo zimetumia janga hilo kama nyenzo ya kisiasa ya kushambulia wapinzani wao na kupata kura, zikipuuza maisha ya watu, serikali ya China imeweka umuhimu zaidi kwa usalama wa maisha ya watu, na kuchukua hatua madhubuti za kuzuia na kudhibiti janga hilo. Kutokana na hatua mwafaka za serikali, utaratibu wa kawaida wa maisha na kazi nchini China ulirejeshwa haraka, na kuongeza imani ya wananchi katika kushinda janga hilo.

Imani kubwa ya Wachina pia inatokana na juhudi kubwa za serikali za kustawisha tena taifa, ambapo inaonesha kuwa serikali ya China ni serikali inayoweza kuwaongoza watu wake kutimiza ndoto zao za maendeleo. Katika zaidi ya miaka mia moja iliyopita, kila Mchina ana ndoto ya kustawisha tena China. Historia na hali halisi vimewaambia Wachina kwamba ndoto hii inaweza kutimizwa tu chini ya uongozi wa serikali chini ya Chama cha Kikomunisti cha China. Katika miaka miwili iliyopita tangu kutokea kwa janga la COVID-19, uchumi wa nchi mbalimbali duniani umeathiriwa sana. Hata hivyo, China bado imepata mafanikio makubwa. Mwaka 2020, China ilikuwa nchi pekee ya uchumi mkubwa duniani ambayo ilitimiza ukuaji wa uchumi. Katika mwaka huo huo, China ilitangaza kuwa imeondokana na umaskini uliokithiri, na kutimiza lengo la kujenga jamii yenye maisha bora kwa pande zote, ambalo ni lengo lake la kwanza la miaka 100. Mwaka 2021, uchumi wa China ulikua kwa asilimia 8.1, ambacho ni kiwango cha juu zaidi katika mwongo uliopita, na pato la taifa kwa mtu lilifikia dola 12,500 za Marekani, ambayo ni karibu sana na kigezo cha dola 12,695 ili kuwa nchi yenye pato la juu kilichowekwa na Umoja wa Mataifa.

Serikali ya China inawaongoza wananchi wake kupiga hatua kubwa kuelekea lengo lake la pili la miaka 100, ambalo ni kujenga nchi ya kisasa ya kisoshalisti yenye ustawi, demokrasia na ustaarabu mkubwa.
 
Hiyo ni human nature ...kadri unavyokandamiza watu ndiyo wanazidi kuwa loyal kwako (mpaka kuwa tayari kufa kwaajili yako) mfano mzuri ni dini ya kiislam
 
Imani kwa serikali inategemeana sana na awareness ya wananchi kuhusu utawala wa nchi katika nchi husika na jinsi gani ambavyo wananchi wanajihusisha katika masuala ya kisiasa ya nchi yao.

Katika nchi ambazo wananchi wake wana awareness kubwa na masuala ya utawala na serikali yao, pia wamejihusisha sana katika siasa, mara nyingi hupelekea wananchi kupoteza imani na serikali mara kwa mara, hali inayochagizwa pia na migawanyiko ya kisiasa ya mara kwa mara.
 
Hiyo ni human nature ...kadri unavyokandamiza watu ndiyo wanazidi kuwa loyal kwako (mpaka kuwa tayari kufa kwaajili yako) mfano mzuri ni dini ya kiislam
Si kweli.
Basi madikteta wasingefurushwa madarakani.Uislamu ni imani.
Nchi za kiislamu zinawatendea mema watu wake wote wanapata basic needs , China wananchi wake wote wanapata basic needs.China na Nchi za kiislamu wananchi wao wananufaika zaidi na raslimali na kodi zao kwann wasizipende serikali zao.
Hata nchi za Afrika ya waislamu watawala wao awawatendei mabaya watu wao
 
Ndani ya miaka 30 tu, serikali ya Uchina imefanikiwa kuwatoa watu milioni 600 kutoka kwenye lindi la umasikini na kufikia uchumi wa kati. Hili halijawahi tokea sehemu yoyote ile duniani, hata Marekani lenyewe ambalo ni taifa ambalo lilikuwa ndiyo tajiri zaidi duniani kiviwanda kipindi cha karne ya 19 (The Gilded Age) halikuwa hivi.

Kitu ambacho chama cha kikomunisti kimejitahidi kuliko mataifa ya Magharibi ni kwamba wamefanikiwa kudhibiti pengo baina ya wale wenye nacho na wasio nacho (The Level of Inequality) ndani ya nchi yao. Ikumbukwe kuwa na uchumi mkubwa hakumaanishi kwamba raia wana usawa wowote ule. Prof Walter Scheidel anasema hivi "There's no nexus between economic growth of a country and reduction in poverty among the citizens"

Mfano halisi ni huu: hadi kufika mwaka 1914 wakati vita ya dunia inaanza Uchumi wa Uingereza ulikuwa ni mkubwa sana duniani, lakini kinachoshangaza ni kwamba asilimia 90% ya mali zote ndani ya nchi zilikuwa zinamilikiwa na asiliamia 10% ya mabwanyenye. Upande mwingine Prof Joseph Stiglitz anasema Marekani kuna wale ambao wanajiita The 1% (The Once Percent) ambao ndiyo ambao wameshikilia uchumi wa nchi. Leo hii kipato cha Bill Bates ni kikubwa mara milioni 1.5 ya kipata ambacho anakipata raia wa kawaida kwa mwaka (Annual Per Capita Income).

Mbaya sasa, kule Marekani matajiri hupewa punguzo la kodi (Tax Cuts), ikiaminika kwamba hili litawahamasisha wao kufanya matumizi zaidi. Nadhani hili nalo halijakaa vizuri sana, maana kama matajiri hawalipi kodi lazima pengo baina ya walionacho na wasio nacho liongezeke tu. Sasa pengo baina ya walio nacho na wasio nacho (The Level of Inequality) ndani ya nchi husababisha matatizo ndani ya jamii ambayo hufanya watu wasiziamini serikali zao.

1. Mfumuko wa bei wa bidhaa na huduma muhimu za kijamii (Rent Seeking Practices husababisha haya)
2. Anguko la kiuchumi (Speculative Market ya The Lehman Brothers mwaka 2008 iliangusha uchumi wa nchi)
3. Kupungua kwa nguvu ya uzalishaji (Low Productivity due to Low Wages)

Sasa nchini Uchina ukiwa tajiri lazima utalipa kodi, ukikwepa utapigwa kitanzi hadi kufa.
Ukitumia RENT SEEKING halafu ukabainika unaswekwa ndani au unalipishwa faini kubwa liwe fundisho kwa wengine.
Marekani The Lehman Brothers imezungua lakini serikali ikawapa Bail Outs na wahusika hawakufikishwa mahakamani.

Marekani huduma za afya ziko juu sana kulinganisha na mataifa mengine ya Ulaya ambako huduma ni za gharama sana, lakini kuna UNIVERSAL HEALTH CARE SYSTEM. Nchini Ujerumani serikali inatoa asilimia 77% ya fedha za huduma za Afya, yaani hawana mzaha. Kuna wanafunzi wa Marekani walienda kusoma Ujerumani na kushangaa sana kuona huduma ambazo wangelipia mamilioni ya fedha nchini kwao, kule walilipa bima ndogo tu na kupata huduma bora zaidi. Hapa unadhani raia watakuwa na imani na serikali yao kweli ???

Mwisho kabisa: Serikali yoyote ile duniani hupimwa uimara wake kwa kutathmini jinsi ambavyo inakabiliana na majanga ya kitaifa kama Uchumi na Kiuasalama. Raia wanaweza kusema wanapenda mfumo wa kidemokrasia, lakini amini amini nakwambia raia wakiwa na uhakika wa uhai wao, mali zao na afya zao kutoka kwa serikali basi lazima wataimini hiyo serikali. Imani kwenye serikali za Uchina imeimarika sana kipindi cha UVIKO.

Walivyodhibiti tatizo ndani ya nchi yao, pamoja na kupunguza kasi ya maambukizi na vifo, ni jambo ambalo limeishangaza dunia yote. Kitendo cha kuweza kujenga hospitali za dharura zenye vyumba 1,500 ndani ya siku tano tu, huku kukiwa na vifaa vya kisasa na madaktari unadhania ni jambo la kawaida kweli ??? Bado tena wakaja na chanjo yao wenyewe yenye gharama ndogo ambayo watu aina zote walipata.

Hapo utadiriki kuwashawishi hawa watu waanze kufuata falsafa za kidemokrasia za wakina Plato na Aristotle wa Ugiriki kweli, wakati Marekani kwenye demokrasia wamekufa maelfu ya watu ??? Bado tena watu wengi wamekufa kwa kukosa huduma nzuri, huku makampuni binafsi ya madawa yakihodhi chanjo na kuziuza kwa gharama, huku yakiwasisitiza watu kuchanja hata mara mbili. Sasa watu wanavyoona haya unadhani wataacha kupinga chanjo na kutoiamini serikali yao kweli ???

Chama Cha Kikomunisti hakiaminiki na wachina tu, hata maiafa ya Magharibi yanakiamini ndiyo maana leo yaniajiandaa kuhudhuria mashindano ya Olympic hata kama wanasema bado kirusi kipo. Dunia imefahamu kwamba Uchuna wamekidhibiti na endapo matatizo yatawakuta huko bado watapata huduma zote ambazo watazihitaji kiafya.

FUATILIA JINSI UCHINA ILIVYOKABIDILI CHANGAMOTO ZIFUATAZO HALAFU UTAELEWA:
1. Anguko la kiuchumi mwaka 2008
2. Tatizo la Uviko mwaka 2019
 
Naunga mkono kwa tajiri kupunguziwa kodi au kutolipa kabisa hii inasaidia kupromote uchumi kwa maana tajiri anajengewa uwezo wa kutajirika na kutajirika kwa manufaa ya nchi kadri tajiri anavyowekeza zaidi ndivyo anavyopunguza zaidi tatizo la ajira nchini, masikini wakipata ajira pato la taifa litaongezeka
 
Umenena vyema kabisa. Kwa tathmini ambayo nimeifanya kwa miaka kadhaa iliyopita, waChina siyo tu wanaiamini serikali yao, bali pia wanajivunia serikali yao. Wanajivunia kuwa chini ya serikali ya chama cha communist cha China.
Wanaridhika jinsi serikali yao inavyoendeshwa kisasa, pia imara halafu huduma za msingi zinatolewa kwao bila upendeleo.

Lingine ni kuwa waChina wako smart, wakipanga issue, lazima itekelezwe. Siyo kama marekani kila kiongozi anakuja na sera zake, mara huyu kaja na Obamacare, huyu mwingine kaivuruga kasema haifai. Mpaka sasa wako njia panda. Hawajui wafanye nini. Wana rais ambaye hawampendi, lkn bado hawana chaguo mbadala, mpaka wana mtamani mke wa Obama kuwa rais. Shida sana.
 
Back
Top Bottom