Kwanza Juliana angemweleza Ade kabla ya ndoa kuhusu uhalisia wa mambo, kama Ade angekataa basi halikua andiko, angekubali wangeenda wote kwenye kitengo na Ade angepata ushauri nasaha jinsi ya kuishi na mke mwathirika maisha yangekwenda.
Kuna dada mmoja alikaa kwenye mahusiano akiwa anakunywa dawa bila kumwambia mchumba. Mara nyingi alimuuliza mchumba wake "hivi ukiona mtu mwenye UKIMWI utamtambua"? Mwanauma alijibu "mimi kwa macho tu ninamtambua". Kumbe aliishi nae miaka karibu miwili asimtambue.
Siku anamvalisha pete ya uchumba, dada alimwambia kabla sijakubali, ni kheri ujue haya. Yule mwanaume alichanganyikiwa, alitoka pale na kwenda kucheck afya yake mwenyewe walikua wanakwenda kavu. Alivyopimwa hakukutwa na ugonjwa, alitafakari sana, mwisho alirudi kwa yule dada na kumuuliza ni kwanini hukuniambia siku zote? Dada alijibu hakujua reaction yake itakavyokua na jinsi walivyo relationship inakwenda vizuri, na anakunywa dawa kila siku ili pia kumlinda yeye.
Mwisho wa siku jamaa alimkubali kama alivyo na waliishi vizuri tu kwenye ndoa.