Imani inapozidi sayansi

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,738
215,924
Habari za J'mosi wandugu,

Leo hii nimepata story ya shost Juliana, aliniaga anakwenda Marekani miaka mingi kidogo imepita. Shost alikuwa mjasirimali, alikuwa na saloon ya kutengeneza nywele, ndani ya saloon yake pia aliuza nguo, handabags, perfumes mwenyewe aliliita boutique. Maisha yalivyozidi kusonga mbele ili kuweka uhusiano mzuri na wateja alianza aliwapa watu bidhaa hata wakiwa hawana pesa ili wamlipe pesa baadae. Watu wengi hawakua waaminifu na bishara ilianza kuporomoka.

Juliana alikua na boyfriend alieitwa Mark, uhusiano wao haukua mzuri sana kwa karibia miezi kumi au mwaka mmoja hivi. Mark hakuwa wa kumpa msaada hata wa mawazo Juliana. Wakati bishara inayumba Mark ndiyo alikua hata kuonekana haonekani.

Mama mdogo wa Juliana alikwenda Marekani siku nyingi sana na mume wake, waliondoka na mtoto mmoja lakini wakiwa kule walipata watoto wengine wawili. Gharama za malezi ya watoto katika nchi za watu ni kubwa hivyo mama mdogo alivyosikia biashara ya Juliana haiendi vizuri alimshauri aende Marekani kumsaidia ulezi wa watoto na yeye aangaze na macho kidogo.

Juliana alianza mchakato wa kupata visa, baada ya refusal moja alifanikiwa kupata visa. Mark aliposikia Juliana amepata visa khee mapenzi yasirudije kwa nguvu. Kumbe alikua anajua Juliana anavyompenda na akifika kule atamvuta tu na yeye. Juliana kuona simu za Mark, si furaha aliyokua nayo moyoni, walianza kwenda dinner na mpaka tunda Mark alipewa. Kumbe bwana katika kile kipindi Mark alipotea alikutana na ji mama lililokua linampa mapesa na kumweka mjini, na Zaidi ya yote jimama lilimegea Mark UKIMWI kidogo ambao nae alimmegea Juliana kidogo akiwa anajiandaa na safari.

Juliana amefika Marekani akaishi kwa mama mdogo, mama mdogo na mume wake wote ni waajiriwa, walikwenda kazini J3-Ijumaa na weekende walikua na mapumziko. Makubaliano yao ilikuwa Juliana anakaa na watoto J3-Ijumaa, weekend wazazi wenyewe wanajukumu la kukaa na watoto wao na yeye anakuwa mapumziko. Pamoja na hayo mama mdogo na mume wake walimpa Juliana $200 kwa mwezi.

Juliana alianza kutumia ujuzi wake wa kusuka nywele kutafuta wateja, weekend akiwa off alisuka watu nywele na kulipwa pesa, alisuka nywele za $ 50, 70 mpaka 100. Pia katika kujichanganya Juliana alisaidia wanawake wenye biashara ya kupamba kumbi za maharusi na kupika chakula, na walimlipa ujira wake. Karibu kila weend Juliana alikuwa na uhakika wa kuingiza $ 200-300.

Juliana mambo yamechanganya bwana, anatuma madola nyumbani kuwasaidia. Mama mdogo na mume wake walimshauri atafute mwanasheria afungue kesi ya kuomba kibali, sijui kesi hii ni kwa misingi gani lakini faili lake lilikuwa idara ya nyumbani, ingawa hakuwa na kibali cha kufanya kazi. Juliana alipata umaarufu, weekend watu walimbook mwezi au wiki sita mbele kwenda kuwasuka nywele. Baada ya kama miaka mitatu hivi, Juliana alipata mteja mwenye mafua makali sana, Juliana kuambukizwa mafua na yeye akaanza kuumwa. Homa imekua homa, Juliana aliugua mpaka ilibidi kwenda hospitali, baada ya vipimo kutoka ndiyo ikajulikana Juliana ni HIV+.

Mama mdogo na mume wake ngachoka, wakifikiria jinsi ya kumtunza Juliana na ugonjwa wa muda mrefu. Walifikia uamuzi wa kumwambia arudi nyumbani ambako atapata tiba. Mama mdogo aliajiriwa kwenye kampuni ndogo tu, mwenye kampuni ni mama wa kizungu. Kwa bahati nzuri siku moja wakiwa wanaongea na boss wake, mama mdogo alimhadithia mkasa ulipata kwa mgeni alienae. Yule mama wa kizungu kusikia mkasa huo alikua na shauku sana ya kumwona Juliana, kwani yeye alikua na mtoto mmoja tu wa kiume ambae alishakufa kwa HIV na mama yule alisema hata kubali kuona mwenye ugonjwa huu anapata tabu. Aliahidi kumweka Juliana kwenye insurance yake, Juliana aliambiwa atumie dawa yeyote ambayo ni nzuri kwake, bila kufikiria gharama.

Dawa zilivyomkubali Juliana alipendeza sana, akakutana na Ade, mzee wa ki-Nigeria wa miaka 50 hivi ambae alikwenda Marekani kama kijana na sasa umri umemfika hata hajaoa. Ade alimpenda sana Juliana, alitaka mwanamke wa ki-Afrika wa kufunga nae ndoa, alichoshwa na vituko vya wa-Marekani. Juliana alimpeleka Ade kwa mama mdogo na baba mdogo ambako alieleza nia yake, mama mdogo alimuuliza Juliana umemwambia mwenzako janga ulilonalo? Juliana alijibu nimemwambia na yuko vizuri tu.

Julia wakati huo yuko kwenye undictable status, harusi ilifungwa nzuri tu ya kanisani. Ade alikua na vibali hivyo alivyomfile Juliana na yeye mambo yakawa mswano. Tatizo la kumngoja Ade yuko bafuni anaoga na yeye kupata dawa halikua kubwa, kasheshe ni ule mzigo wa miezi sita unaopewa unauweka wapi huyu mtu asijue. Swala hili lilimuumiza sana Juliana.

Mapenzi wakati huo yameshamiri, Ade na Juliana wanavaa nguo sare wakienda kanisani. Juliana ameshafundishwa kupia egusi soup, okra soup, pounded yam, assorted meat, jolof rice, na vingine vingi. Siku moja Ade ametoka kazini amekuja na kipeperushi cha mchungaji kutoka Nigeria atakua Marekani kuombea wenye matatizo ya magojwa, wasiopata watoto, mikosi na mambo mengine. Juliana kupata habari ile alifurahi sana.

Juliana alishiriki siku zote za maombi na kufunga. Waliambiwa walioombewa wamempona kabisa na wasishindane na nguvu za Mungu wamtegemee yeye na waache hizo dawa wanazokunywa kwani wamepokea uponywaji. Juliana asitupe zigo lake la ARV zilizokuwa ndani ya kitanda cha box! Maisha yamekwenda, baada ya muda ameanza kuugua, lakini mawazo ya kuwa yeye ni mwathirika alishayatoa siku nyingi sana. Kuugua mwisho ilibidi aende hospitali, akalazwa akafanyiwa vipimo, majibu yalipotoka ilibidi daktari amweleze Ade matatizo ya mkewe ni kuwa HIV imeshadevelop kuwa AIDS na hatua iliyofika ni stage mbaya sana. Ade alipomuona Juliana baada ya maelezo hayo alimpiga vibao kwanza, walinzi wa hospitali kumtoa nje, baba wa watu Analia kama mtoto mdogo, umeniua wewe mwana mke. Ni kweli vipimo vilionyesha kuwa Ade pia alishaathirika kwa ugonjwa huo.

My take, msaada Mungu aliomletea Juliana ulikua ni yule mama wa kizungu aliyekubali kugharamia matibabu yake.
 
Juliana kama ugonjwa wenyewe ulipoanza kujulikana........kuna jirani yetu naye anasambaza kweli ukimwuliza anakwambia kwani naye aliupata kwenye soda yaani majanga.......nawapongeza sana wale wanaotambua tatizo na kuamua kutosambaza kama juliana
 
Matatizo ya Juliana ni kukataa kukubali kuwa yeye ni muathirika na anatakiwa kutumia dawa maisha yake yote.
 
Wengi wao wanapotumia dawa wanaamini wamepona au hawataweza kuambukiza na ndipo wanaendelea kusambaza
Mkuu ukiwa unatumia dawa na kufikia undictable status, nafasi ya wewe kuambukia mtu mingine ni 1%
 
Kuna familia wanakufa na huo ugonjwa kuanzia wa kwanza hadi mwisho kama vile wanaambukizana unaweza fikiri mapepo
Lakini kwa dunia ya leo, wanaotumia dawa wana uhakika wa maisha, hao wanaokufa labda hawajajitambua kama ni wagonjwa.
 
Habari za J'mosi wandugu,

Leo hii nimepata story ya shost Juliana, aliniaga anakwenda Marekani miaka mingi kidogo imepita. Shost alikuwa mjasirimali, alikuwa na saloon ya kutengeneza nywele, ndani ya saloon yake pia aliuza nguo, handabags, perfumes mwenyewe aliliita boutique. Maisha yalivyozidi kusonga mbele ili kuweka uhusiano mzuri na wateja alianza aliwapa watu bidhaa hata wakiwa hawana pesa ili wamlipe pesa baadae. Watu wengi hawakua waaminifu na bishara ilianza kuporomoka.

Juliana alikua na boyfriend alieitwa Mark, uhusiano wao haukua mzuri sana kwa karibia miezi kumi au mwaka mmoja hivi. Mark hakuwa wa kumpa msaada hata wa mawazo Juliana. Wakati bishara inayumba Mark ndiyo alikua hata kuonekana haonekani.

Mama mdogo wa Juliana alikwenda Marekani siku nyingi sana na mume wake, waliondoka na mtoto mmoja lakini wakiwa kule walipata watoto wengine wawili. Gharama za malezi ya watoto katika nchi za watu ni kubwa hivyo mama mdogo alivyosikia biashara ya Juliana haiendi vizuri alimshauri aende Marekani kumsaidia ulezi wa watoto na yeye aangaze na macho kidogo.

Juliana alianza mchakato wa kupata visa, baada ya refusal moja alifanikiwa kupata visa. Mark aliposikia Juliana amepata visa khee mapenzi yasirudije kwa nguvu. Kumbe alikua anajua Juliana anavyompenda na akifika kule atamvuta tu na yeye. Juliana kuona simu za Mark, si furaha aliyokua nayo moyoni, walianza kwenda dinner na mpaka tunda Mark alipewa. Kumbe bwana katika kile kipindi Mark alipotea alikutana na ji mama lililokua linampa mapesa na kumweka mjini, na Zaidi ya yote jimama lilimegea Mark UKIMWI kidogo ambao nae alimmegea Juliana kidogo akiwa anajiandaa na safari.

Juliana amefika Marekani akaishi kwa mama mdogo, mama mdogo na mume wake wote ni waajiriwa, walikwenda kazini J3-Ijumaa na weekende walikua na mapumziko. Makubaliano yao ilikuwa Juliana anakaa na watoto J3-Ijumaa, weekend wazazi wenyewe wanajukumu la kukaa na watoto wao na yeye anakuwa mapumziko. Pamoja na hayo mama mdogo na mume wake walimpa Juliana $200 kwa mwezi.

Juliana alianza kutumia ujuzi wake wa kusuka nywele kutafuta wateja, weekend akiwa off alisuka watu nywele na kulipwa pesa, alisuka nywele za $ 50, 70 mpaka 100. Pia katika kujichanganya Juliana alisaidia wanawake wenye biashara ya kupamba kumbi za maharusi na kupika chakula, na walimlipa ujira wake. Karibu kila weend Juliana alikuwa na uhakika wa kuingiza $ 200-300.

Juliana mambo yamechanganya bwana, anatuma madola nyumbani kuwasaidia. Mama mdogo na mume wake walimshauri atafute mwanasheria afungue kesi ya kuomba kibali, sijui kesi hii ni kwa misingi gani lakini faili lake lilikuwa idara ya nyumbani, ingawa hakuwa na kibali cha kufanya kazi. Juliana alipata umaarufu, weekend watu walimbook mwezi au wiki sita mbele kwenda kuwasuka nywele. Baada ya kama miaka mitatu hivi, Juliana alipata mteja mwenye mafua makali sana, Juliana kuambukizwa mafua na yeye akaanza kuumwa. Homa imekua homa, Juliana aliugua mpaka ilibidi kwenda hospitali, baada ya vipimo kutoka ndiyo ikajulikana Juliana ni HIV+.

Mama mdogo na mume wake ngachoka, wakifikiria jinsi ya kumtunza Juliana na ugonjwa wa muda mrefu. Walifikia uamuzi wa kumwambia arudi nyumbani ambako atapata tiba. Mama mdogo aliajiriwa kwenye kampuni ndogo tu, mwenye kampuni ni mama wa kizungu. Kwa bahati nzuri siku moja wakiwa wanaongea na boss wake, mama mdogo alimhadithia mkasa ulipata kwa mgeni alienae. Yule mama wa kizungu kusikia mkasa huo alikua na shauku sana ya kumwona Juliana, kwani yeye alikua na mtoto mmoja tu wa kiume ambae alishakufa kwa HIV na mama yule alisema hata kubali kuona mwenye ugonjwa huu anapata tabu. Aliahidi kumweka Juliana kwenye insurance yake, Juliana aliambiwa atumie dawa yeyote ambayo ni nzuri kwake, bila kufikiria gharama.

Dawa zilivyomkubali Juliana alipendeza sana, akakutana na Ade, mzee wa ki-Nigeria wa miaka 50 hivi ambae alikwenda Marekani kama kijana na sasa umri umemfika hata hajaoa. Ade alimpenda sana Juliana, alitaka mwanamke wa ki-Afrika wa kufunga nae ndoa, alichoshwa na vituko vya wa-Marekani. Juliana alimpeleka Ade kwa mama mdogo na baba mdogo ambako alieleza nia yake, mama mdogo alimuuliza Juliana umemwambia mwenzako janga ulilonalo? Juliana alijibu nimemwambia na yuko vizuri tu.

Julia wakati huo yuko kwenye undictable status, harusi ilifungwa nzuri tu ya kanisani. Ade alikua na vibali hivyo alivyomfile Juliana na yeye mambo yakawa mswano. Tatizo la kumngoja Ade yuko bafuni anaoga na yeye kupata dawa halikua kubwa, kasheshe ni ule mzigo wa miezi sita unaopewa unauweka wapi huyu mtu asijue. Swala hili lilimuumiza sana Juliana.

Mapenzi wakati huo yameshamiri, Ade na Juliana wanavaa nguo sare wakienda kanisani. Juliana ameshafundishwa kupia egusi soup, okra soup, pounded yam, assorted meat, jolof rice, na vingine vingi. Siku moja Ade ametoka kazini amekuja na kipeperushi cha mchungaji kutoka Nigeria atakua Marekani kuombea wenye matatizo ya magojwa, wasiopata watoto, mikosi na mambo mengine. Juliana kupata habari ile alifurahi sana.

Juliana alishiriki siku zote za maombi na kufunga. Waliambiwa walioombewa wamempona kabisa na wasishindane na nguvu za Mungu wamtegemee yeye na waache hizo dawa wanazokunywa kwani wamepokea uponywaji. Juliana asitupe zigo lake la ARV zilizokuwa ndani ya kitanda cha box! Maisha yamekwenda, baada ya muda ameanza kuugua, lakini mawazo ya kuwa yeye ni mwathirika alishayatoa siku nyingi sana. Kuugua mwisho ilibidi aende hospitali, akalazwa akafanyiwa vipimo, majibu yalipotoka ilibidi daktari amweleze Ade matatizo ya mkewe ni kuwa HIV imeshadevelop kuwa AIDS na hatua iliyofika ni stage mbaya sana. Ade alipomuona Juliana baada ya maelezo hayo alimpiga vibao kwanza, walinzi wa hospitali kumtoa nje, baba wa watu Analia kama mtoto mdogo, umeniua wewe mwana mke. Ni kweli vipimo vilionyesha kuwa Ade pia alishaathirika kwa ugonjwa huo.

My take, msaada Mungu aliomletea Juliana ulikua ni yule mama wa kizungu aliyekubali kugharamia matibabu yake.

Kama sayansi ndiyo mwisho wa kila kitu kuna sababu gani ya kuzungumzia habari za Mungu? Bila shaka mleta mada huna ufahamu juu ya Mungu wala uwezo wa nguvu zake. Ndiyo saabu unadiriki kumlinganisha na sayansi. Iambie sayansi izuie vifo kwa sababu watu hawapendi kufa.

Iambie sayansi ikomeshe maradhi.

iambie sayansi itegneneze dunia nyingine ili magaidi wanaotaka kuishi peke yao duniani wahamie kule.

Iambie sayansi iondoe hitaji la kula kwa kuwa chakula kimepungua na watu wanalia njaa.

Imani inayoishia kwenye sayansi ni imani mfu, imani ya kuona na ni sawa na kuabudu mibuyu, masanamu, kwa sababu ya ujinga wa kutokmujua Mungu wala uweza wa nguvu zake, na ufanyaji kazi zke.
 
mbona kama imeishia njia panda ivi!
wewe Sky Eclat ndio mchezo wako huo, unaleta uhondo alafu unatuacha dilema!
 
Mmmmmmmhhhhh! Msaada wa Mungu hauna kikomo, wala mipaka.

Swala ni kwamba Mungu anasema USIZINI NA UNA ZINI KAMA KAWAIDA TU unategemea nini?

Punguza presha, kufanya mapenzi sio jambo la ajabu kama mlivyoaminishwa sunday school, ukiwa responsible you are doing just fine, na nani kakwambia kuzini ndiyo njia pekee ya maambukizi, unataka uniambie hiyo ni God's punishmemt au? Ukimwi unapatikana kwa njia nyingi tu, ukikupata you are just unlucky.
 
Kama sayansi ndiyo mwisho wa kila kitu kuna sababu gani ya kuzungumzia habari za Mungu? Bila shaka mleta mada huna ufahamu juu ya Mungu wala uwezo wa nguvu zake. Ndiyo saabu unadiriki kumlinganisha na sayansi. Iambie sayansi izuie vifo kwa sababu watu hawapendi kufa.

Iambie sayansi ikomeshe maradhi.

iambie sayansi itegneneze dunia nyingine ili magaidi wanaotaka kuishi peke yao duniani wahamie kule.

Iambie sayansi iondoe hitaji la kula kwa kuwa chakula kimepungua na watu wanalia njaa.

Imani inayoishia kwenye sayansi ni imani mfu, imani ya kuona na ni sawa na kuabudu mibuyu, masanamu, kwa sababu ya ujinga wa kutokmujua Mungu wala uweza wa nguvu zake, na ufanyaji kazi zke.
Mungu alishatenda miujiza katika maisha ya Juliana kwa kumkutanisha na mama aliyegharamia matibabu yake, Mungu pia hapendi uongo, Juliana alitakiwa kumwambia Ade hali halisi. Kama vipimo vilionyesha ni mwathirika basi angekubali kufanya vipimo tena akiamini Imani yake imemponya asingefikia hali ya kudhoofika. Imani ipo na Mungu ana uwezo mkubwa sana ila tusimjaribu.
 
Back
Top Bottom