nasrimgambo
JF-Expert Member
- Jan 10, 2017
- 1,919
- 2,520
Kabla ya kufika dini zilizoingia nchini kwa meli, waafrika, wa hapa Tanzania ya sasa walikuwa tayari wana imani zao za asili. Ambazo zilitamalaki na watu wakaziamini kwa uwazi kabisa nazo zikaongoza maisha yao koroho.
Sasa zinaonekana zimepotea, na kufyekelewa mbali na dini za uislamu na ukristo,
huo ni mtazamo mmoja uliopo, na ndio mtazamo uliotamalaki.
Ila pia kuna mtazamo wa pili, ambao haujatamalaki kama mtazamo wa kwanza, huu ni mtazamo kuwa imani za mtu mweusi hazijafa kabisa, na bado zipo kama zilivyo awali ila tu zipo kimya.
tukianza na mtazamo wa kwanza, inaonekana wale watu walioamini imani za kaifrika kiidadi ni wachache sana ama wameisha, kila mtu kama si muislamu ni mkristo, kuanzia aina ya majina wanayotumia, aina ya sikukuu wanazosherehekea, ibada wanazofanya na kadhalika
kwa kifupi hizi dini za kuja zilifanikiwa kwasababu imani za kiafrika hazikuwa na mifumo rasmi ya kurithisha imani yani kwa kizungu imani za kiafrika hazikuwa organized religion
Kwanza zilikuwa ni imani ambazo hazitafuti wafuasi wapya, kwasababu ijapokuwa waliamini katika uwepo wa Mungu, waliamini kuwa Mungu huwasiliana na walio hai kupitia wafu, yani mababu waliokufa ama mizimu kwa lugha maarufu.
Hivyo kila mtu, kila ukoo, kila kabila, ilikuwa wanamuomba Mungu kupitia mababu/mizimu yao, hakukuwa na haja ya kutaka mtu mwengine aamini unachoamini kwasababu hata akiamini hakimsaidii, yani mfano mimi nikitokea ukoo wa Mgambo basi ningeamini kuwa namuomba Mungu kupitia mababu wa ukoo wangu au kabila langu, hivyo mababu wa Mosha au Rugamalira hawawezi nisaidia, hivyo hakukuwa na haja ya kumfanya Mosha aamini mababu zangu kwasababu hawamsaidii, na mimi sikuonekana kuhitsjika kuabudu kama kina Mosha kwasababu wanachoabudu hakitonisaidia kwasababu mimi sio wa ukoo wao, hivyo mababu zao hawanitambui. Hivyo wakati dini mpya zinapambania kupata waumini wapya walioamini imani za kiafrika hawakuona umuhimu wa kutafuta waumini wapya wa imani zao maana waliamini imani zao ziliwasaidia wao wenyewe wao kama wao na hakukuwa na haja ya kuaminiwa na watu wengine
Pili ni imani ambazo hazikuwa na siku rasmi za ibada wala sikukuu. Leo hii mtu akiwa muislamu basi kila ijumaa ya kila wiki kuna namna atakumbushwa kuwa yeye ni muislamu, tena adhana mara tano kwa siku anakumbushwa, akiwa mkristo kila jumapili anakumbushwa kuwa yeye ni mkristo, waafrika imani zetu hazikuwa na hilo, hakukuwa na ijumaa wala jumapili. Waafrika walienda sehemu za kuabudia pale wanapopata matatizo tu, mtu hapati mtoto au ukame umezidi ndio wanaenda kutambika ula kama mtu ana neema ilikuwa hakuna haja ya matambiko
Sikukuu za kiafrika nyingi hazikuwa za sikukuu za kiimani, sikukuu zilikuwa kusherehekea mavuno msimu wa kuvuna na sherehe za jando na unyago kwa vijana ama mtoto akizaliwa, hakukuwa hata na miezi ya kufunga.
Pia imani za kiafrika hazikuandikwa vitabuni, hii inatokana na sanaa ya uandishi kuchelewa kuzaliwa kiasili maeneo yetu.
hili la mwisho la kutoandikwa kwa imani zetu linaonesha sio tu imani za kiafrika zilikuwa hazisambai kwa ufanisi ila pia kulikuwa na nafasi kubwa kwa uongouongo kuingizwa kwenye imani, maana kama mafundisho yanatokea kichwani mwa mtu na kusambazwa kwa mdomo lazima kuna waongo ambao pia kwa urahisi wangefundisha wezao uongo, hiyo ndio kasoro kubwa ambayo imani za kiafrika ilikuwa nayo
Sasa kuna mtazamo wa pili kuwa imani hizi za kiafrika bado zipo, kwamba bali na kuamini dini mpya kwa namna fulani waafrika wengi bado wana chembechembe za imani za kiafrika, mfano mkubwa na wa dhahiri, ambao tunauona ni imani ya kusafisha makaburi
Imani hii bwana imeshika mizizi hasa hapa Tanzania. Yani watu wengi nchini wakienda kwao kusafisha makaburi akirudi anajiona mwepeeeesi, anaona kajiletea nuru kwenye mambo yake
mfano mwengine ni wa watu kuamini kuwa ndugu zao waliokufa wanaumia ama kupendezwa na matendo tunayofanya duniani
kuamini kuwa mtu aliyefariki anafurahia au kuchukia matendo ama eti ukisafisha kaburi ni unajiletea wepesi wa mambo, hizo ni asilimia mia kama sio tisini ni imani asili za kiafrika
kwasababu dini za uislamu na ukristo haziamini katika wafu, kwa waislamu, wanaamini mtu akifa, mwili unakuwa umekufa roho inabaki ila roho hiyo inakuwa inategemea tu rehema za Mungu, yani waislamu wanamini roho ya mtu aliyekufa haiwezi kukusaidia chochote maana roho hiyo inategemea rehema za mwenyezi Mungu kama alikuwa mwema anapata rehema njema kama alikuwa muovu basi kazi anayo hadi siku ya kiama, hivyo kufagia kaburi la mtu huyo ama kuamini kuwa anapendezwa ama kuchukia matendo yako huko ni kujidanganya maana roho hiyo kiislamu muda huo inakuwa bize ikihangaikia rehema za mwenyezi Mungu, na roho hiyo inategemea zaidi kuombewa na walio hai na haiwezi kusaidia walio hai kwa lolote
kwa wakriato, wao wanaamini wafu wamelala fofofo hadi siku ya kiama, hivyo kufagia makaburi ili upate nuru na kuamini kuwa jamaa aliyefariki anachukizwa ama kupendezwa na matendo yako ni nje ya ukristo,
kwa misingi hiyo, imani za kiafrika bado zina mizizi vichwani mwa watu weusi.
Mababu zetu bwana hawakupambana kupata waumini wapya maana waliamini haina haja kufanya hivyo, na kweli hakukuwa na haja kwa misingi ya imani hizo, ila ajabu walichoamini bado kinasurvive kimtindo, zilikuwa ni imani zenye nguvu