babalao 2
JF-Expert Member
- Apr 6, 2012
- 5,398
- 3,243
IMAM wa Msikiti wa Thaqi B,Hamza Omary (37) maarufu kama Mohamed amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mwanza,akikabiliwa na mashitaka mawili ya uchochezi.
Alifikishwa mahakamani hapo jana mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Godfrey Mwambapa.Wakili wa Serikali, Felista Lelo alidai kuwa mshtakiwa alitenda makosa hayo kati ya Desemba mwaka jana na Februari mwaka huu katika Msikiti wa Thaqi B wilayani
Nyamagana jijini Mwanza.
Katika shitaka la uchochezi,Wakili alidai Imam huyo anadaiwa kuchochea chuki kwa nia ovu chini ya Kifungu Namba 63 B (i) (ii) cha Kanuni ya Adhabu Sura ya 16, kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.
Alidai katika kipindi cha miezi hiyo, mshitakiwa akiwa katika mkutano wa kidini kwenye Msikiti wa Thaqi B, alitamka maneno ya uchochezi yaliyosema: "Ardhi yetu inaelekea pazuri kwenda kuchinjana na makafiri, kwa hali hii kuchinja ni halali".
Alidai kuwa maneno hayo yalichochea chuki miongoni mwa Watanzania. Katika shitaka hilo, Imam huyo hakutakiwa kujibu lolote,kutokana na mahakana hiyo kutokuwa na mamlaka hadi hapo itakapopata ridhaa kutoka kwa Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP).
Katika shitaka la pili, Lelo alidai kuwa mshtakiwa anakabiliwa na shitaka la kuchochea uhalifu chini ya Kifungu 390 na 35 cha Sheria
ya Kanuni ya Adhabu Sura ya 16, kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.
Alidai kuwa katika kipindi hicho cha Desemba mwaka jana hadi Februari mwaka huu katika Msikiti wa Thaqi B,akihutubia mkutano wa kidini,aliwachochea wasikilizaji kufanya uhalifu wa mauaji,ambao ni kosa chini ya Kifungu 196 na 197 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu.
Alidai kuwa katika mkutano huo, mshitakiwa alitamka maneno "Ardhi yetu inaelekea pazuri kwenda kuchinjana na makafiri, kwa hali hii
kuchinjana ni halali". Mshtakiwa alikana shitaka hilo na kupelekwa rumande baada ya wakili wa Serikali, kuiomba Mahakama isimpatie dhamana.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Machi 13, mwaka huu,ambapo Mahakama itatoa uamuzi wa pingamizi la dhamana.
Wakati huo huo Polisi inaendelea kumsaka Mkurugenzi wa Kituo cha Redio cha Kwa Neema Fm,Askofu Augustino Mpemba pamoja na Shehe, Ilunga Kapunga wakituhumiwa kuchochea chuki za kidini.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Ernest Mangu alisema viongozi hao wa dini hawajapatikana. Alisema baada ya kufuatilia, Polisi ilibaini kuwa Shehe Ilunga yupo India kwa matibabu.
Kwa upande wa Mpemba ambaye ni Askofu wa Kanisa la Tanzania Field Evangelism,alisema hajulikani alipo.Aliwaomba raia wema wenye taarifa za askofu huyo, kutoa ushirikiano kwa polisi kueleza alipo.
Source. Habari leo.
Kwa mwendo huu Wachochezi watahubiria kutokea mapangoni.