Kamanda Moshi
JF-Expert Member
- Apr 1, 2012
- 2,000
- 3,045
Umenena vizuri. Lakini hajajibu swali la msingi, naomba unijibu:
Bikira Maria yuko hai kama alivyo Musa na Eliya huko mbiguni?
Kama ndiyo, unaweza ku-justify kwa angalia mstari mmoja wa Biblia?
Kama hayuko hai, point iko wapi kuwasiliana na mfu?
Pia naomba jibu, kuna shida gani mkiomba kwa Yesu moja kwa moja?
Kama hujui jibu la swali unakubali kitu usichokielewa.
Unaamini Virgin Mary na utakatifu wake, lakini huwezi kuelezea kwa.nini mama huyu na utakatifu wake wote na uwezo wake wa kuwapa Waafrika masikini dawa wasife kama nzi kwa Ebola hajitokezi Monrovia Liberia awape dawa masikini hawa anaenda kutokea sehemu nyingine.
Swali lako la shetani na binadamu nani katangulia lina assume kwamba mimi naamoni katika kuwepo kwa shetani na mungu.
Mimi sikubali kwamba shetani yupo, sikubali kwamba mungu yupo.
Kwa hiyo swali lako kwangu hali apply.
Ukifimiri kwa kutumia akili na kuacha mambo ya mapenzi ya dini pembeni utaona huyu mungu wa waislamu na wakristo ni kamba tu.
Hawezekaniki.
Sawa twende taratibu.
Mimi nina mahusiano ya Ki DNA na mama yangu, mimi siku exist before ya mama yangu, mimi sikumuumba mama yangu, mimi si Mungu wa mama yangu.....
U-mama wa Maria kwa Yesu si sawa na U-mama wa mama yangu kwangu
twende taratibu.
Ndugu, uko serious?
Sio lazima awe na nafasi. Pale Ikulu uliwahi kusikia chochote kuhusu mama wa prof?
kuna maswali mengi ningekuuliza but ngoja nianze na haya,
Eliya pekee ndiye aliyepalizwa mbinguni bila kufa kwa mujibu wa hao watatu uliowarefer hapa, lakini musa alikufa na sehemu ulopata kwa bible inayomuongelea musa ni pale alipokuja yeye na eliya wakazungumza juu ya kifo cha yesu mlimani...wakat yesu akiwa na wanafunzi wake wale watatu...
sasa swali je waamini katika ufufuo?if yes why useme utaombaje kwa wafu? kwani yesu alipomwambia yule mwizi pale msalabani amini amini nakuambia leo hii utakuwa pamoja nami paradisoni in maana wafu wanawasiliana na kuonana?au unadhani yesu alipokufa kwa zile siku 3 alikuwa mfu completely?
hujasikia kwa kua hujajifunza zaidi kuhusu professor. ila kama wataka kumjua zidi professor amini amini nakuambia ni lazima pia utamjua na mama yake.
Naamini maisha baada ya kufa. Lakini sio immediately baada ya kufa ni mpaka siku ya ufufuo ndugu yangu. Kwa sasa maria hayuko hai. Ni mfu. Hata hao watakatifu wengine akina Petro, Yakobo, Yohaba, hata baba wa imani Ibrahim wote ni watu wanasubiri ufufuo. Hivyo maria ni mfu.
Kwa nini bikira Maria hatokei Monrovia Liberia awape watu dawa ya Ebola wasife kwa mafungu kama nzi?
Uwezo anao, upendo anao, kwa nini hatokei huko anaenda kutokea Iowa?
asante kwa hiyo wataka kuniambia maria alikuwa kama kasha tu la kupitishia/kubebea mzigo?
tuanze na maswali rahisi, kwa nini ilikuwa yeye na si mwingine?
na huko kutokuwa na mahusiano ya ki-DNA na maria nani alikuambia ni kweli? nifahamuvyo mie kwa sayansi yangu duni (mind you nimegraduate kwa degree ya Engineering Biotechnology) ili mtoto awepo/afanyike kunahitajika sperm and egg, sasa yesu hakukuwa na sperm from a man, je leo pia wataka kutupa ufunuo mpya kuwa hakukuwa na egg from a mother?
je ndugu yangu wataka kuchanganya concept ya roho na mwili?
maana wengi pia hawaelewi concept hii ya roho na mwili katika biblia. unakaribishwa kwa ufafanuzi zaidi wa chochote.
Swali lako ndugu linatofauti yoyote na kusema kama Mungu anapenda watu na anauwezo kwanini anaacha watu wanakufa sana Palestina na sehemu zingine za dunia? Au mbona wanasayansi wanahangaika kupata dawa ya UKIMWI miaka zaidi ya 30 sasa na asiwasaidie?
Anayeweza kujibu ajibu 😊
Kwan Maria alivyozaa Yesu,,yule mmewe Yusufu hakulala naeee
Hakuzaa wadogo zake Yesu!!?? Kwa hiyo bikra iliendelea tu kujirudiaa????
Nashukuru kunijulisha kuwa ni Eliya pekee aliyepalizwa. Ila ni kweli pia kuwa Musa na Enok wako hai mbinguni.
Naamini katika ufufuo. Lakini Biblia imeweka wazi kuwa ufufuo una majira yake yatakuja. Sio mtu afe leo then immediately afufuliwe aendelee kuishi peponi. Wafu hawako hai (wamekufa) mpaka hapo Yesu atakapowafufua siku ya mwisho.
Mfano wa Yesu na yule mwizi msalabani, maana yake ni kuwa alimsamehe na amempa pas ya kuurithi ufalme wake (siku ya mwisho na watakatifu wengine waliolala katika Yesu Kristo) sio kuwa yeye ametangulia!! Ndio sababu walikufa wote lakini aliyefufuka ni Yesu peke yake, yule mwizi alibaki mfu mpaka leo anasubiri ufufuo ila yeye ana advantage kuwa ataingia mbinguni maana Mungu alishamwambia pale msalabani.
Zaidi ya hapo, kwa nini mungu mwenye uwezo wote na ujuzi wote aumbe ulimwengu ambao mabaya yanawezekanika?
Ukichunguza sana utaona hizi habari za mungu kuwepo zina ujinga kibao.
Hapana hazina ujinga. Mimi naamini Mungu yupo na nimeshamuona!
Na ukichunguza kwa akili za kibinadam utachemka au kudata kabisa. Cha kwanza kabisa amini bila shaka yeyote kuwa Yesu ni Bwana! Yesu ni Mungu na ndiye aliyeufanya ulimwengu (sio dunia tu), ulimwengu (the 9 planets) ukawepo.
Biblia ninayoiamini mimi imeandikwa "mpumbavu amesema moyoni mwake hakuna Mungu". Hivyo ilijua kutakuwa na wapumbavu aina yako (kama unasema hakuna Mungu).
Lakini kila mtu na imani yake ndugu.
Maria alipata mimba kwa huwezo wa Roho mtakatifu ( Njia za Mungu hazichunguziki). Nimejarib kutumia neno Uhusiano wa ni ki-DNA ili huweze nielewa kuwa Maria ni mwanadamu na position yake itabaki kuwa hiyo. Alitumiwa kama walivyo tumika binadamu wengine,
mitume walitumika katika positions zao.
Ndugu, uko serious?