Image of virgin Mary grows on tree

Hujathibitisha mungu yupo. Chochote utakachosema kuhusu mungu ni moot, hogwash, malarkey.
Lengo hapa hakuna aliekuwa na haja ya kuthibitisha uwepo wa mungu. Mtu huthibitisha pale penye utata na hakuna kati yetu (isipokuwa wewe) ambaye anahitaji uthibitisho. Sasa wewe ulioko nje ya uzio na unataka tukubaliane nawe basi fanya kazi ya kuthibitisha kinyume na hakika tuliyonayo.Wewe unakadhania thibitisha thibitisha, nani athibitishe kitu kisicho na mjadala, sasa wewe kwa akili zako unatakiwa ututowe ujingani kwa kutuonyesha kuwa hayo tunayoyaamini si kweli.
Umekuwa ukipoteza muda kwa kumtaka kila mmoja athibitishe na hakuna hata kati yetu tulilijali hilo, sasa aidha huna cha kufanya hata unangangania jambo ambalo lishaonyesha kuwa hutolipata au una tatizo la kutofahamu ishara, kwani ni wazi hakuna anaejali kutowa uthibitisho wakati kati yetu hatuna wasiwasi na mtizamo wetu.
 
Mimi siamini kuwepo mungu, niambie wewe unayeamini.
Kwa hivyo hukutakiwa kuniuliza kitu usichokiamini.
Nimesema wewe una tatizo linakusumbua, yaani hukijuwi kitu halafu unauliza maana. Unless you came across something then you can ask about it.
 
Angalau nimefarijika kujuwa kuwa yuko Mungu mmoja tu, lakini dotnet kama ni mmoja si angekuwa huyo baba badala ya mtoto? Nauliza tu.
 
Hujajibu swali kwa nini mungu mwenye ujuzi wote, uwezo wote na upendo wote aumbe ulimwengu ambao mabaya yanawezekanika kama huu.

Sio kuwezekanika tu, anaweza yeye mwenyewe akawapiga vibaya wale anaopenda kuwaadhibu kutokana na upuuzi wao. Tena alikuwa zamani ananuia kufuta kizazi chote anaacha waaminifu wachache tu. Hujasikia habari za gharika au Sodoma hata kama huziamini lazima utakuwa umezisikia. Hivyo basi usikosee kuutafsiri upendo na huruma zake kuwa anaukubali upuuzi, ukiingia anga zake bila utaratibu aubukitaka kushindana naye atakuharibu vibaya utashangaa Mungu gani huyu? Anatisha ujue hilo.

Sisi tunaoamini tunasoma habari za watu wa kale aliokuwa akiwaongoza nabii Musa. Kulikuwa na watu wabishi wewe enzi za Musa yaani wewe hata sekunde huwafikii kwa ubishi. Musa alikuwa anapata wakati mgumu.

Siku moja wakamwambia Musa ee, kama vipi mwambie Mungu wako aje tuongee naye bana sio kila siku anakutuma kwetu tu yeye yuko wapi? Musa akawambia basi siku fulani muda fulani atakuja mkamsubiri kwenye mlima.

Siku na saa ilipofika, Mungu akaanza kuja pale mlimani. Ni hivi, huo umeme, ngurumo, tetemeko na miali ya mwanga mkali watu walipuga kelele wakimsihi Musa amwambie Mungu arudi waendelee kumtumia Musa kama mjumbe. Mungu akarudi. Na ujue hizo ngurumo na miali ya mwanga mkali ilikuwa ndo anajiandaa kuinuka tu hahaha pata picha angepiga hata hatua moja tu ingekuwaje?

Hii habari, hata kama huiamini nakuambia udiendelee kuuliza oh Mungu ana uwezo oh huruma mbona anaacha ebola so and so, hiyo habari hapo juu inakusomesha kuwa Mungu wetub(tunaoamini) anatisha! Ebola kitu gani wakati yeye mwenyewe anafuta kizazi chote. Guess what pamoja na yote hayo, Mungu wetu ndiye Yehova, mtu akubali akatae haibadili kitu maana mtu huyo hajui hata urefu wa maisha yake, anaishi kwa hofu hajui yajayo anajua yaliyopita tu.
 
Lengo hapa hakuna aliekuwa na haja ya kuthibitisha uwepo wa mungu.

Wrong.

Mimi nina haja ya kuthibitishiwa kwamba mungu yupo, ili watu wanaposema "mungu hivi, mungu vile" nijue wanaongelea kitu chenye uthibitisho na si hadithi za kiimani tu.

Kama unasema hakuna aliyekuwa na haja ya kuthibitisha uwepo wa mungu napata mashaka kwamba unasoma ninachoandika.

Mtu huthibitisha pale penye utata na hakuna kati yetu (isipokuwa wewe) ambaye anahitaji uthibitisho.

Sasa unajua kwamba nataka huo uthibitisho, kwa nini unasema hakuna mtu anayetaka uthibitisho huo?

Unaelewa unachoandika mwenyewe?



Sasa wewe ulioko nje ya uzio na unataka tukubaliane nawe basi fanya kazi ya kuthibitisha kinyume na hakika tuliyonayo.

First of all, unajuaje nani yupo ndani ya uzio na nani yupo nje ya uzio? Uzio wa nini? Wa ujinga?

Second of all, one cannot prove a negative. Those wh say something is there have the burden of proving that it is there.The one who questions that assertion need only ask for proof.

Third, I do not necessarily want people to agree with me. I just want a rigorous examination that is logical and comprehensive. If the idea of the existence of a godhead wins the argument on the logical merit, I am prepared to accept that. In fact I will be relieved. Because all the problems of this world will rest on god's shoulder, not mans. I think subconsciously people want to believe in a god because they are lazy and are not ready to accept responsibility. If god created the universe and he is all powerful, then the big picture things could be slated to god for a solution, we could just go down and pray and god will make it toasty.

People who do not believe in the existence of a god have to do more work, planning etc. There is no god to pray to, you gotta do the work yourself.

This is part of the reason why countries with a high inclination for religiosity are backwards in education and economy. Too much dependence on god. Watu watakufa migodini huko, kifusi kimeanguka, rais badala ya kuangalia masuala ya quality/ process control, anaishia kusema "ni kazi ya mungu". Tunaishi ki kudra kudra. In fact tuna msemo wa Kiswahili kabisa unasema "Jitihada haishindi kudra". Kwamba wewe jitahidi unavyotaka lakini kama hujapata kudra hufiki popote. Ndiyo mentality ya kidini dini hii inayotufanya tuwe masikini mpaka kesho.



Wewe unakadhania thibitisha thibitisha, nani athibitishe kitu kisicho na mjadala, sasa wewe kwa akili zako unatakiwa ututowe ujingani kwa kutuonyesha kuwa hayo tunayoyaamini si kweli.

Nikuonyeshe mara ngapi? Nimetoa objection due to logical inconsistencies in the nature of your god and the observable universe. Sijapata majibu. Tatizo hata nikikuonyesha utaelewa ninachoandika?



Sasa kati yangu mimi ambaye sina cha kufanya na wewe unayemjibu mtu ambaye hana cha kufanya nani afadhali?

Kuna watu wanafuatilia mjadala na kujifunza hapa.

Na ukisema hakuna anayejali kutoa uthibitisho unathibitisha kwamba hujui kusoma, kwani watu wanajaribu.

Tatizo hawawezi kuthibitisha. Kama usivyoweza wewe.

Kubali tu, siwezi kuthibitisha, huyu mungu wetu ni wa kuungaunga kuliko mungu wa maboksi. Hathibitishiki.
 

Thibitisha kwamba mungu yupo.

Halafu ujibu kwa nini mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote aumbe ulimwengu ambao una ubaya, mateso na magonjwa kama huu.

Kwa nini aumbe ulimwengu ambao atakuja kufuta vizazi? Alikosea kama mtoto wa darasa la kwanza anavyokosea kwa kuandika kwa penseli na kufuta kwa ufutio?

Hujajibu hili swali.
 
Unafahamu madai na pia unafahamu Public.
Kwa ufupi madai ni kitu kipya na Public ni walio wengi.
Sasa hebu jiangalie, wewe ni public au wale walio wengi humu? Wewe huwezi kuwa Public kwani sisi tuaminio mungu ndio public nawe ni solitary person basi
Kuhusu madai, nini madai? Madai ni dhana au jambo jipya unalolileta mbele ya watu, sasa naona hili la Mungu si madai kwani watu wote wanalijuwa na ndio maana hakuna zaidi ya wewe humu aliyekuja na kuonyesha kuwa nimeleta madai.
Pengine wewe sasa ndio unaleta hayo madai mbele ya hiyo public, na ikiwa hivyo maelezo yako yakurudie mwenyewe kuwa ulitakiwa uthibitishe kuwa Mungu hayuko. Wala hizo tentieth au thitieth zisingefika kama ungethibitisha hayo madai yako uliyoyatowa kwenye public kuwa hakuna mungu.
 

Madai ni kitu kipya kwa definition gani?

Do you even know that this is a public forum?
 

Unamtukana Mungu kwa kumfananisha na mtoto anayekosea? Kweli hujui ulitendalo.

Utasubiri sana uthibitisho (ishara) na hutakaa uupate, huenda unatumaini hilo ukiangalia huku na kule uone kama atatokea atakayethibitisha.

Ipo siku itathibitika kwako tena kwa njia ambayo ama utafurahi sana kujiona kuwa ulikuwa mpumbavu kabla (mpumbavu amesema moyoni, hakuna Mungu) au utajuta sana na ku wish ungepata muda wa kumtumikia huyo Mungu usiyemkubali sasa kwa kwa maandishi lakini moyoni kwako nina uhakika kweli inakushuhudia vinginevyo (guilty for pretending).

Waiting for proof? Keep waiting.
 

Nimemtukana vipi mungu wakati yeye mwenyewe kaumba viumbe, halafu hakufurahishwa kawafutilia mbali?

Huyu mungu ana tofauti gani na mtoto anayejifunza kuandika, akaona hakupatia muandiko, akafuta aanze upya?

Umeanidka
"Utasubiri sana uthibitisho (ishara) na hutakaa uupate..."
halafu bada ya hapo tu umeandika tena
"Ipo siku itathibitika kwako tena kwa njia ambayo ama utafurahi sana kujiona kuwa ulikuwa mpumbavu kabla (mpumbavu amesema moyoni, hakuna Mungu) au utajuta sana na ku wish ungepata muda wa kumtumikia huyo Mungu
...

Wewe mwenyewe hujui kama unaenda au unarudi! Unajichanganya changanya tu. No wonder unaamini mungu ambaye huwezi kumthibitisha.
 
​Naona ni pande mbili na labda tupige kura ili mmoja wetu akubali kubadilisha mfumo, unataka nithibitishe kuwepo kwa mungu nami nataka uthibitishe kuwa hayupo. wewe una sababu zako nami nina zangu na hakuna aliye juu ya mwenziwe kwani unilazimishe wakati wewe hutaki kulazimishwa?
 

Ukweli haujali kura.

Hata dunia nzima ikipiga kura kusema kwamba jua halipo, kama lipo litaendelea juwapo tu.

Ukifikiri ukweli unategemea kura utakosea sana tu.
 
Ukweli haujali kura.

Hata dunia nzima ikipiga kura kusema kwamba jua halipo, kama lipo litaendelea juwapo tu.

Ukifikiri ukweli unategemea kura utakosea sana tu.
Hebu jaribu kunielewa. Hatuwezi kuupigia kura uwepo wa Mungu, nilichokwambia kuwa wewe baki na msimamo wako wa kutaka uthibitisho wa kuwepo kwa mungu nami nibaki na msimamo wangu wa kutaka uthibitishe kuwa hakuna Mungu.
Iwapo unalazimisha basi kuwepo kura na ukishinda basi mimi nitafanya unavyotaka wewe. Kupiga kura juu ya uwepo wa Mungu loh! Mungu asitukutanishe mimi na wewe kabisa.
 

Bado kura haijasimamia ukweli automatically, kwa hiyo kama wengi wanaweza kuwa wajinga na ujinga ukashinda, kura si njia nzuri ya kuamua mambo.

Mimi nishakwambia sababu ya kutowezekanika kwa chochote kisichokuwapo (sio tu mungu) kutowezekana kuthibitika kwamba hakipo. Na mfano nikakutolea. Na challenge ya kuthibitisha kimoja ambacho hakipo nikakupa. Mpaka sasa hujaweza kuthibitisha.

What's your excuse?
 
Ikiwa ni hivyo nimekupa uthibitisho wa kuwepo Mungu. Pengine kama mwenyewe ulivyojilabu kuwa unajuwa kusoma tofauti na wengine nilikuuliza jee umesaidia kiasi gani cha kuuumbwa binaadamu na si kiumbe mwengine, ulijiamulia vipi gender yako, ulijiamulia vipi kutokeza huku kwa wajinga, na jee kipindi gani cha umri wako umekichukia kiasi kwamba unaendelea kuwa mzee na mwisho ( kwa niliyokuuliza mimi) hili pande la ardhi unalolikanyaga ulilipia kiasi gani huko kokote ulikokuwepo kabla ya kuja hapa?
 

Uthibitisho wako wa kuwepo kwa mungu umeutoa wapi? Weka link hapa.
 
Uthibitisho wako wa kuwepo kwa mungu umeutoa wapi? Weka link hapa.

Linki gani zaidi ya wewe Kiranga, kwani si wewe ninaekuzungumzia na umeshindwa kuonyesha hiyo planning na hard working uliosema ndio msingi wa binaadamu.
Sasa ninakwambia kuwa yuko alie kuleta wewe Kiranga na akakupa na akili ukashindwa kuzitumia vizuri na kuanza kumkejeli.
Sasa ni zamu yako thibitisha kuwa hakuna kitu kama hicho bali wewe ni wewe na hard working na plani zako tu!
 

Utathibitishaje kwamba kile ambacho hakipo hakipo?

Utaanzia wapi?

Utatafuta fingerprint?

Kilichopo ndicho kinachothibitika kwamba kipo. Kisichopo hakithibitishiki kwamba hakipo.

Thibitisha kwamba mungu yupo kusema "link gani zaidi ya wewe Kiranga" si uthibitisho kwamba mungu yupo.
 
Yaani huu ndio upeo wa hoja zako? Siamini kuwa binaadamu hungangania kitu hata kama kimechuja.
Pengine hukujijua kuwa uthibitisho wa kuwepo kwa mungu ni uwepo wako wewe? Usishangae na wala usilazimishe vitu wakati wewe mwenyewe umeumbwa katika mambo ambayo huwezi kuyagusa. Uthibitisho wa kuwepo kwa mungu ni uwepo wa wewe na kama unabisha basi thibitisha kuwa picha fulani au video fulani inaonyesha kuwa wewe huwezi kuwa kithibitisho cha kuwepo mungu.
Ninachokwambia mimi ni kuwa Mungu kakuumba nawe kataa na uniambie wewe umeteremkaje sijui wapi?
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…