kiss ov love
JF-Expert Member
- Jan 21, 2025
- 9,388
- 16,176
Kuna wengi wamelelewa na Bibi na babu. Au bibi pekeyake na maisha yakasonga tu.Ktk kitu nashukuru, ni kupewa hawa wazazi nilionao, huwa nawaza wasingekua hawa, ingekuaje kwa upande wangu?
ππππ hapo kwenye kujidai kuna shidaDunia imejaa watu weak sana siku hizi.
Huyo kwanza ni dume anajidai KE
hapo ndo shida inapoanzia, ukishajiona mnyonge unaona kulialia ni haki yako.
Unakaa unawalaumu wengine wakati maisha yako ni 100% jukumu lako.
Acha uzwazwa wewe, jikomboe au jinyonge, the choice is yours.
Uko sahihi, kuna wengine wana wazazi kabisa na bado wana maisha kama hayo hayo tu! Swala ni kumove on na kupambana akiwa busy na kazi au familia hatopata muda wa kuwaza hayo yote!Poleee sana Dear!
Ktk kitu nashukuru, ni kupewa hawa wazazi nilionao, huwa nawaza wasingekua hawa, ingekuaje kwa upande wangu?
Pambana dear, iko siku utafurahia kusudi na uwepo wako hapa Duniani.
π€π€π€ thread ifungwe....Punguza kulalamika,nyuzi zako nyingi ni kulalamika tu,
Kulalamika hakuwezi kuibadili hali yako,mabadiliko yanaanza na wewe mwenyewe kwa kubadili fikra zako,
Dunia haina huruma,Dunia ya leo inataka ubishi na ujasiri wa kupambana,
Hizi pole utakazo pewa hapa haziwezi kubadili chochote,
Mama yako aliplay part yake,now it's your turn,
Maisha ni yako,pambana kivyako,life is very short,acha kuishi kinyonge.
Sure, hakuna namna ni lazima kuishi na kuishi ni lazima kupambana kwa kusimama na miguu yako mwenyewe.Mwisho wa siku lazima maisha yaendelee......
Yalitokea ukiwa mdogo,sasa ushakua mkubwa simama kwa miguu yako songa mbele, hata ukikaa kuwalaumu watu haisaidii kitu
Pole sana, pitia hapa https://www.jw.org/sw/maktaba/magazeti/w20010201/Unaweza-Kukabiliana-na-Kivunja-Moyo/Sijui ni lini na mimi ntakuwa na furaha maishani, Furaha yangu ilitoweka pasipo kujua baada ya kumpoteza mama yangu miaka mingi iliyopita nikiwa bado mdogo sana.
Maisha niliyopitia kutoka kwa ndugu, mama wa kambo pamoja na baba asiyejali yananipa hasira sana, sijui hata nimlaumu nani kuzaliwa kwenye hii familia, huu ukoo na huyu mzazi ambaye hakutaka kabisa kusimamia nafasi yake na kutimiza majukumu yake ya malezi ipasavyo kwetu sisi watoto wake.
Natamani kama kungekuwa kuna Dunia nyingine ambayo haitakuwa na binadamu niende nikaishi huko nipotelee nisionekane na mtu yoyote kila mtu asahau kuhusu mimi.
R.I.P mom ulikuwa mpambanaji ukahakikisha kaka amesoma na amemaliza chuo kupitia ujasiriamali wako mdogo mdogo uliokuwa ukifanya, matokeo yake huyu kaka uliyempambania leo hii hakumbuki wadogo zake ametuacha tuteseke peke yetu, hata leo hii simu zake hazipatikani amekuwa addicted na pombe hadi anashindwa kufanya kazi yake kwa ufanisi.
Pengine ungekuwepo mom nisingepita nilikopita ungenifundisha vingi vizuri na imani pia ungenipambania, wala usingeniacha niteseke kama alivyofanya baba. Nasikitika sana kwanini umeondoka nikiwa bado mdogo, bado nakuhitaji mama yanguππ
Kwanini Mungu ameruhusu hili litokee kwangu, kuna muda huwa najiuliza hivi Mungu huwa anaona mateso na matatizo yetu tunayopitia sisi wanadamu, huwa namlaumu sana Mungu kuniondolea mama yangu kipenzi nikiwa mdogo, namlaumu pia kuruhusu mateso yawe sehemu ya maisha yangu, kunipa baba asiyejali watoto wake.
Ninahisi kumchukia baba yangu, hata akinipigia simu sifurahii kabisa, hata kwenda kumsalimia hadi anikumbushe au tu hiyo siku nijisikie mwenyewe. Lakini nimemsamehe kwa yote aliyoyafanya maishani mwangu japo moyoni mwangu naumia sana kila nikiyafikiria maisha yangu yaliyopita.
Natamani hata wakati ule mama yangu angebaki ningetanguliaga mimi, najitahidi kuwa na furaha lakini nikikaa mwenyewe furaha yote inatoweka.
Nawezaje kuondokana na haya maumivu yaliombatana na chuki kwa ndugu zangu?
Unantisha mzee mwenzangu kwahiyo hapa mnyoosho bado πππSure, hakuna namna ni lazima kuishi na kuishi ni lazima kupambana kwa kusimama na miguu yako mwenyewe.
Na tunakoendea maisha yatazidi kuwa tough sana, yaani haturudi nyuma, life linazidi kuwa tough...