Ilivyo ngumu kuvunja maagano na viapo katika koo na familia

Ilivyo ngumu kuvunja maagano na viapo katika koo na familia

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
359,869
Reaction score
828,395
Naileta mada hii kutokana na mwenzetu mmoja ambaye tulijadiliana naye! Hivyo naomba pia niwashirikishe nanyi kwakuwa pengine na kwa vyovyote wahitaji wapo

Tunapokuwa wakubwa na kujitambua huwa kuna vitu tunaviona sio vya kawaida kwenye ukoo na hata kwenye familia. Na mara nyingi vitu hivyo huambatana na matokeo hasi
Vichache kati ya hivyo ambavyo pia ndio kama vya msingi ni
Mahusiano, ndoa na familia
Ajira na kipato

Biashara na uwekezaji
Elimu maarifa na vipaji
Dini imani na vipawa
Mafanikio umaarufu na kutambulika

Wanaobahatika kuwa na tafakuri na kujali huona kabisa kuna vitu haviko sawa kwenye familia au ukoo kwenye baadhi ya vitu nilivyoidhinisha hapo juu

Hii hali inatesa na kuumiza sana na baadhi huchukua hatua kwa kuanza safari ya kutafuta suluhu ya kudumu ili kuikomboa familia ama ukoo

Ni kwenye safari hiyo iliyojaa sintofahamu nyingi ndio baadhi kama si wote hukutana na magumu michangano na mengine mengi

.Waganga wa kienyeji (wengi feki na matapeli)
.Wapiga ramli (sometimes chonganishi)
. Wasoma nyota viganja na taroti
.Manabii na mitume wa kuungaunga
. Wasoma visomo na watoa kafara za damu

Kote huko utazunguka na kuzungushwa lakini utapata ahueni ya muda tuu na baada ya hapo mambo kuharibika zaidi
Baadhi yetu kabla ya kuchukua hatua yoyote huamua kuwatafuta wazazi mababu ama ndugu na kujaribu kuwauliza

Kinachotuumiza sana waafrika ni kushindwa kuhifadhi mambo yetu kwenye maandishi na sauti..

Wenzetu waliweza! Maana walitengeneza mitego lakini pia wakahifadhi kwa siri namna ya kuitegua

Maagano yenye nguvu pamoja na mambo mengine yalinenewa kwenye namba.. Kumbuka namba ndio zinaendesha dunia
Kwa mfano kama agano la kutofika mbali kielimu kibiashara ama kimahusiano kutokana na hasira ama kisasi cha mtamkaji liliangazia
Mwaka
Mwezi
Wiki
Siku
Saa
Dakika
Mavazi
Uelekeo
Kwahiyo sometimes si lazima amwage damu ya mnyama ama kufanya vitu vya kishirikina.. Akiipangilia vema formula yake namba kimekulamba familia au ukoo
Sasa anachotakiwa kufanya ni kuhifadhi mahali pa siri kwakuwa viapo vingi, manuizi maagano na malipizi hufanya kazi mhusika anapokata pumzi..

Sasa kuweka hakiba kama mambo yatabadilika vile alivyotaka yawe anatakiwa kumkabidhi mwanaukoo anayemuamini ili aje atumie formula husika kutegua agano, KIA po ama lipizi

Kama hiyo formula ikikosekana kwasababu zozote zile hakuna namna zaidi ya kusubiri si chini ya vizazi vitatu ama vinne!
Je nimeeleweka?

Kuna familia zina laana ya asili | Page 12 | JamiiForums Kuna familia zina laana ya asili
 
Hivi kwanini waafrika hawataki kukubaliana na ukweli kuwa maisha kiasili ni magumu na magumh zaidi huku kwetu afrika kwa sababu muda umetizidi mbio na system zetu za maisha hazilipi kutokana na spidi kali ya DUNIA MPYA

Tunaishia kulaumu laana za ukoo na mambo mengi ya kufikirika
 
Nothing is perfect under the sun! Ila ninaamini kuna mengi bado huyajui ama unayapuuzia
 
Ni muhimu sana ndani ya ukoo wako ama familia yako ni kitu gani mkifanya kinawapa changamoto nyingi ama ni kipi kinawapa changamoto kidogo

Chenye kuwapasua vilivyo msilazimishe kipigeni chini fasta chenye mwelekeo chanya tembeeni nacho na matunda mtayaona!

Sometimes hivi vitu sio makosa yetu bali ni urithi wa damu kupitia kizalia cha DNA
 
At first glance, okay itakuwa solution kusubiri laana hiyo itoweke Kwa vizazi vijavyo vipi kuhusu Mimi WA Sasa nataka itoweke NAMI Nile Raha za Dunia kama mafanikio etc

Mshana Jr
Huwezi kulaanika ama kufanyiwa maagano kwenye vyote kuna baadhi vitakubeba hivyo ishi navyo.. Vyenye changamoto kubwa kila ukivigusa vitue
 
Hivi kwanini waafrika hawataki kukubaliana na ukweli kuwa maisha kiasili ni magumu na magumh zaidi huku kwetu afrika kwa sababu muda umetizidi mbio na system zetu za maisha hazilipi kutokana na spidi kali ya DUNIA MPYA

Tunaishia kulaumu laana za ukoo na mambo mengi ya kufikirika
Naunga mkono hoja
 
Yeah,agano linaanza kazi muhusika anapo kata pumzi

Waebrania 9:16-17
[16]Maana agano la urithi lilipo, lazima iwepo mauti yake aliyelifanya.
[17]Kwa maana agano la urithi lina nguvu palipotukia kufa kwa mtu; kwa kuwa halina nguvu kabisa, akiwa yu hai yeye aliyelifanya.

Na wale tunaoamini ktk Holy Spirit, huwa anatuonyesha maagano yanayotusumbua na jinsi ya kuyatatua. Tumuweke karibu 🙏
 
Na wale tunaoamini ktk Holy Spirit, huwa anatuonyesha maagano yanayotusumbua na jinsi ya kuyatatua. Tumuweke karibu
 
Yeah,agano linaanza kazi muhusika anapo kata pumzi

Waebrania 9:16-17
[16]Maana agano la urithi lilipo, lazima iwepo mauti yake aliyelifanya.
[17]Kwa maana agano la urithi lina nguvu palipotukia kufa kwa mtu; kwa kuwa halina nguvu kabisa, akiwa yu hai yeye aliyelifanya.

Na wale tunaoamini ktk Holy Spirit, huwa anatuonyesha maagano yanayotusumbua na jinsi ya kuyatatua. Tumuweke karibu 🙏
Katika Biblia, agano ni ahadi takatifu, inayofunga, na isiyo na masharti kati ya Mungu na wanadamu ambayo inaunda msingi wa uhusiano wao. Makubaliano haya, ambayo mara nyingi yametiwa muhuri katika damu, yanaashiria uaminifu thabiti wa Mungu ili kuwakomboa wanadamu, wakihama kutoka kwa ahadi za Agano la Kale za ulinzi na baraka hadi ahadi ya Agano Jipya ya mioyo ya ndani, iliyobadilishwa kupitia Yesu.
 
Back
Top Bottom