Ndugu tuwe makini nimeona dadili za corona tena inaweza kuwa kali kuliko zilizopita. Nina dots chache hapa:
1. Kifo cha Membe na Lumutuz, haijasemwa directly nini kimewatoa but maelezo ya daktari yanaashiria ni masuala hayo
2. Mamangu mzee kuugua mafua kali haijapata kumtokea na yeye kajaliwa kinga kubwa sana dhidi ya mafua. Tunaweza kuugua wote nyumbani mafua yeye asiugue. Korona iliyopita hakuugua mafua hata kidogo wakati wengine wote tulisikia dadili zote za korona!
3. Mimi nina wiki sasa kifua kilianza polepole na sasa kimezidi kubana ilikuwa usiku tu lakini sasa hata mchana hasa nikilala. Niko busy na mitishamba huku kijijini.
4. Nasikia pia mahospitali watu wenye changamoto za upumuaji wameongezeka sana recently.
Dadili za kipindi hiki zinaweza jumuisha:
1. Kubanwa kifua hasa ukiwa umelala. Inaanza na kusikia kama vile vitu vinachomachoma kifuani
2. Kuumwa kichwa kwa mbali
3. Mafua (baadhi)
4. Hakuna kikohozi
Mytake: Kwa bahati mbaya Tanzania serikali yetu ipo nyuma ya wakati, ni serikali ya maji ya shingo, ubabaishaji, usiri usiojali maisha ya watu, uzembe na kutwajibika kutokana na madhila zinazowapata wananchi wake. Take your steps based on the previous pandemic, usisubiri mtu.
Of course kirus hiki ni strain tofauti kutokana na zilizopita. Viral strains ni nyingi kama mjuavyo virus hubadilika kila wakati na kila kirus kina dadili zake na ukali wake.