Ili umpate huyu binti inakubidi ulipe mahari ya ng'ombe elfu moja.

Ili umpate huyu binti inakubidi ulipe mahari ya ng'ombe elfu moja.

Busu la Kenge

JF-Expert Member
Joined
Jun 13, 2025
Posts
2,310
Reaction score
4,207
Huyu binti hapo chini kwenye Video ni wa kutoka kabila la Mundari. Ili umuoe umpatate lazima ulipe mahari ya ng'ombe 1000.


Mundari ni kabila dogo linalopatikana kilomita 75 kaskazini mwa mji mkuu wa South Sudan Juba.

Kabila hili linapenda na kutukuza ng'ombe kuliko kitu chochote.

Ng'ombe katika jamii hii anatumika kama sifa(status), nguvu, pesa na mahari.

Ki mila na kidesturi mkojo wa ng'ombe wanatumia kuoga na kupaka rangi nywele zao.

Mundari ni wafugaji na wakulima. Zao lao kubwa ni mtama na ulezi.

Likija swala la ng'ombe huwaambii kitu Mundari. Wanatukuza na kuthamini ng'ombe kuliko kitu chochote.

Ng'ombe wao ni wakubwa na wana pembe kubwa kama ng'ombe jamii ya Watutsi na Ankole.

Vijana wa Kimundari wanalala na ng'ombe zao kuwalinda kuibiwa kutoka makabila mengine.
images (1).jpeg



adriz Mjusi Sharobalo Shammy- hydroxo BICHWA KOMWE - ephen_
 
Kama ni yule yule basi alishaolewa. Alipata umaarufu sana na watu walijitolea kumzawadia. Alipewa mpaka Range mpyaaa na wadau...
 
Warefu wasio na tako mara nyingi ni gogo vitandani(no offense),even so ningesugua Hadi itoe moshi Kila nikikumbuka ng'ombe wangu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom