Historia ya kabila la Wakurya

Jitu jeusi

JF-Expert Member
Oct 18, 2015
1,704
2,363
Je Wajua?

KABILA LA WAKURYA

Abakuria (au Wakurya) ni kabila la watu wanaoishi katika wilaya za Rorya, Tarime na Serengeti kwenye mkoa wa Mara, kaskazini mwa Tanzania, na katika wilaya za magharibi na mashariki mwa Mkoa wa Nyanza katika sehemu ya kusini mashariki ya Kenya.

Mnamo mwaka 2005, idadi ya Abakuria ilikadiriwa kuwa 690,000, ikiwa ni 430,000 wanaoishi nchini Tanzania na 260,000 nchini Kenya. Lugha yao ni Kikuria.

Abakuria ni wakulima na wafugaji, huku Abakuria wa nchini Kenya wakiegemea sana kwa kilimo nao wa nchini Tanzania wakiegemea sana ufugaji.

Kilimo cha asili walikuwa wanalima ulezi mtama na viazi tu kwa ajili ya kutengeneza Togwa (obosara) na Pombe.

Mazao mengine yalianza kulimwa miaka ya 1900 baada ya wajerumani kuhimiza kilimo. Wakurya hawapendi kutawaliwa wala kuonewa hivyo walikuwa na saiga lika ya vijana kwa ajili ya ulinzi na usalama hivyo utumwa haukuwaathiri sana. Ila kwa kupenda kwao vita walijiunga sana na jeshi K.A.R (King African Rifle) kupigana vita ya kwanza na ya pili na ya Uganda.

Wakurya ndilo kabila ambalo huona vita kama Mchezo na kuua wakati wa vita ni kama kucheza tu na usiombe ukutane nao wakiwa na hasira. Ila ni watu wema sana wakati wa amani usipowachokoza hawana ubaya na MTU ila ukiwakosea bila kujua hukusamehe hats kabla hujaomba msamaha ila ukiwakosea makusudi hawana msamaha kabisa.

Wakurya ni watu ambao hawasalimu amri ukionesha kuwashinda huenda kujipanga upya na kutafakari ni jinsi gani watashinda na si watu wa kukata tamaa na wakiwa na mori hawaogopi chochote wala lolote wako tayari kukabiliana nalo.

Hasa Abakuria walio katika wilaya ya Serengeti wanatambulika kama wafugaji. Abakuria wanafanana na Wakisii wa nchini Kenya kwa lugha na umbile. Wanadhaniwa walikuwa kundi moja hadi waliposhambuliwa vikali na Wamasai mnamo karne ya 19 na kusambaratishwa katika maeneo tofautitofauti.

Lakini kuna lika ambalo liliandaliwa likapewa mafunzo ya kivita ili kukabiliana na wamasai kwa kutumia pinde na mishale ambapo waliwafuata wamasai na kuwaua kwa wingi ndipo ukawa mwisho wa vita kati ya wamasai na wakurya pia eneo la mbuga ya serengeti na masai mara likapatikana baada ya wamasai kufukuzwa hadi arusha.

Ndipo wakurya wakaweka makao yao ya kudumu eneo hilo na kuendesha Shughuli ya ufugaji na kilimo.
Utengano huo ulisababisha kuweko kwa lahaja mbili ambazo zinaeleweka na kila kundi.

Wakurya ni watu wenye upendo sana wakati wa amani hukubali kukaa na wageni na kuchukuliana kama ndugu, na hii ilipelekea kuwepo wakulya wenyeasili ya makabila jirani mfano kuna wakurya wenye asili ya wajaluo, wasukuma, wamasai n.k.

Abakuria wamegawanyika katika "makabila madogo" au koo kumi na sita, nazo ni:
Nyabasi,
Bakira,
Bairege,
Bagumbe (wanaoishi katika wilaya za nchini Kenya na Tanzania),
Batimbaru,
Banyamongo,
Bakenye,
Basimbiti,
Basweta,
Barenchoka,
Baikoma,
Bamerani na mengineyo.

Makabila haya madogo yote yapo pia katika kabila la Wakisii nchini Kenya.
Kabila la Abakuria pia linakaribiana na kabila la Wazanaki katika Mkoa wa Mara nchini Tanzania. Itikadi zao kadhaa zinafanana.

Asili ya Wakurya ni Misri, walifika Congo kati ya 322. KK
Hapo zamani kulikuwa na mtu aliyeitwa monto, huyu ni mzazi wa wabantu wote.
Monto alizaa Range miongoni mwa wanae,
Range alizaa Magaiwa,
Magaiwa alizaa, alimzaa Mkurya.
Mkurya alizaa watoto watano ambao ni
Nyanchage,
Wangwe,
Mongoso,
Nano na
Mendi.

Nyanchage aliwazaa Mtimbaru, Mosi, na Mosonga hawa ndio tunawaita inchage.
Wangwe aliwazaa Moracha, Mwirege, Keroba, Mugumbe na Gisiri. Hawa ndio tunaowaita Engwe, kemoramba yagesaka.
Watu walivyozidi kuongezeka ukoo wa Gisiri ulikimbilia umasaini nao huitwa Osiri hadi leo huko umasaini.

Kutokana na kosa alilolifanya Gisiri, (ni stori ndefu), ukoo wa Moracha ulibadili jina ukaitwa abanyamongo (wenye maghala ya chakula).
Ukoo wa Mugumbe ulibadili jina ukaitwa abalenchoka (wala nyoka, waliishi mlima wa nyoka).

Mongoso alimzaa Mkira, mtoto pekee. Huyu ndo mzazi wa abakira na maana ya Mongo Mongoso leo ni tembo dume.
Nano aliwazaa Mokenye, Musweta na Msimbete. Hawa ndio waitwao inano yaani nyani.

Kutokana na hawa waliibuka watu mbalimbali kama abakine, abarieri, abamera, abanyanccha na abangoreme.
Mendi alizaa mtoto mmoja tu Munchari, hawa hujiitia emendi yaani panya mdogo au irigeki.

TOHARA (SARO) Orodha hii ni kutoka kwa Wairegi na Wanyamongo, Ila Majina ya Saro kwa wakurya yanafanana tofauti ni miaka. Miaka ambayo walikuwa hawatairi ilikuwa na Matatizo ya Vita au Kiangazi maana utaratibu ulikuwa wanaruka mwaka mmoja mmoja. Ijulikane kuwa kabla ya karne 19 tohara haikuwa kwa wakati mmoja kama sasa.

1. 1868 KEMBARAGUNI(GAIRORWE) WAIREGI Wairegi kukimbilia ng'ambo ya mto Mara, Nyamisangura, Kiagata
2. 1870 - 1880 GINGORI-WAIREGI
3. 1872 MERICHO-WAIREGI
4. 1874 GITURANI-WAIREGI
5. 1876 GESAMBISO-WAIREGI
6. 1878 NTINGURI-
7. 1880 NGICHARO
8. 1882 KEROBA
9. 1884 MUNGIRE-WAIREGI/MACHALE-WANYAMONGO
10. 1886 GIBURA/ITUMBE
11. 1888 KEHOCHA-WAIREGI/GISAMBISO-WANYAM
ONGO
12. 1890 GITIRA-WAIREGI
13. 1892 KIRINA-WANYAMONGO/MACHALE-WAIREGI
14. 1894 KIRINA-WAIREGE
15. 1896 NGINOGO-WANYAMONGO/ABAMASE-WAIREGI
16. 1898 GETEBA-WAIREGI
17. 1900 NGINOGO-CHUNUCHI-WAIREGI/ROMORE(ABASABALINGO)-WANYAMONGO
18. 1910 ROMORE-WAIREGI
19. 1912 NGINARO-WAIREGI
20. 1914 MESONGO-WAIREGI/NGINARO(AMAITANG
'OMBE)
21. 1916 ABAKAMPUNI-WAIREGI
22. 1918 - 1920 ABAKARAMU-WAIREGI/ABAMESONGO-WANYAMONGO
23. 1920 - 1926 ABAKAMPUNI/ABAKARAMU-WANYAM
ONGO (KIANGAZI KIKUBWA WAILEGI KUKIMBILIA MTO MIGORI)
24. 1926 ABAKEHA-WANYAMONGO
25. 1928 MINGISI-WAIREGI/ABABIRISI-WANYAMONGO
26. 1930-1934 MOTO-WANYAMONGO/NTIGURI-WAIREGI (MASHAMBULIZI YA VIWAVI JESHI)
27. 1932 ABANGEREZA-WANYAMONGO (MACHIMBO YA KERENDE MINES)
28. 1936-1937 NGICHARU-WAIREGE (MINES ZA NYAMONGO ZILIFUNGWA VITA YA MJERUMANI NA MWINGEREZA)

Majina ya Wakurya
Chacha
Mwita
Marwa - Pombe
Masero - Ngozi
Mseti
Wangwe - Chui
Matiko, Butiku - Usiku
Wambura - Mvua
Magesa - Mavuno
Nyamohanga - Dudu
Lyimo
Wesiko - Nje
Mseti
Ryoba - Jua
Mniko
Waitara - Ghala
Turuya
Mkami - Kamua
Bisaku - Mlango
Mirumbe - Ukungu
Maseke - Makapi
Nchama - Njama
Msabi - Omba
Nokwi - Mungu
Machela - Njia
Masese - Mbwa
Maina
Masaga - Mboga (Ichinsaga)
Masagati - Twiga
Masaite
Mahiri -Vita
Muhiri - Vita
Mnanka
Matinyi - Mnyama
Machugu - Tembo
Wangwe - Chui
Wandwi - Simba
Magige - Nzige
Magabe - Mpaji
Range
Msoba - Mpweke
Msubi - Mzee wa Mila (Mtaalam)
Motega
Itinde - Tuta
Gisiri/Kisiri
Sagara - Mjusi
Mrimi - Mkulima
Makore
Mgendi
Meremo - Kazi
Merengo
Mgosi
Mgaya - Asili ya Jaluo
Mwikwabe - Asili ya Masai
Ghati - Kati
Bhoke - Asali
Rhobi - Fuatia
Wankuru - Kobe
Nyaihemba - Mtama
Wanchela - Njia
Muhiri
Nyangi - Harusi
Otaigo
Nchagwa
Wanchala - Njaa
Wegesa - Mavuno
Mrange
Sese - Mbwa
Mbusiro - Mbegu
Matinde - Matuta
Nyanokwi - Mungu
Majina ya kikurya mengi yanaitiwa kwa jinsia zote (endoko) hasa kutoka kwa babu na bibi wa pande zote mbili.
Mengine yanaitiwa kulingana na matukio.

KUHUSU MAJINA;
Wakurya wana majina sita ya wazaliwa wa kwanza.
Matatu ya kiume na matatu ya kike.
Naanza na ya kiume Mwita, Marwa na Chacha.
Nitamaliza na ya kike Ghati, Bhoke na Rhobi

MAJINA KWA WANAUME
MWITA
asili yake ni uguita, yaani kuua/Kifo. Wakurya kitu kinachowashinda kupambana nacho huamua kukienzi. Kifo kiliwashinda wakaamua wakienzi kwa kuwapa wazaliwa wa kwanza jina hilo ie to familiarize with that misfortune!!! Ili wakizoee.

CHACHA
asili yake zimekuja, ni jina walilopewa watoto wa kiume waliozaliwa wakati ng'ombe zimeibwa au zimeletwa toka umasaini au usukumani. Wakurya huamini ng'ombe wote ni wao, hivyo ni kama waliporwa, kwa hiyo vijana walipoenda kuiba ilikuwa sio kuiba ila kuzifuata na kuzileta. Zimekuja/Chacha.

MARWA
Marwa ni pombe iliyoandaliwa na kunywewa kusherehekea ng'ombe zilizoletwa.

MAJINA KWA WANAWAKE,
BHOKE
Bhoke ni asali, kitamu, kitu kilichopatikana bila jasho na kitakacholeta vitamu. Hupewa mtoto wa kike kwa sababu huleta ng'ombe bila jasho, ni baraka kwa familia. Linganisha ng'ombe anazoleta Bhoke na zile za kuiba, zinazopatikana kwa kumwaga hata damu. Kwa hiyo ni asali /Bhoke.

RHOBI
Rhobi hutokana na neno Erhobilo, hii ni shangwe inayofanywa na wanawake na wanaume kufuatia tukio zuri kama kurudisha ng'ombe zilizoibwa, Kushinda Vita, Kukabiliana na Wanyama Wakali Simba na Chui. Shangwe hiyo ikifanywa na wanaume pekee huitwa engoliga. Lakini wafata nyayo wanapofika nyumbani nyimbo zao huimbwa na wote, na hapo huitwa Erhobilo, ndo asili ya jina Rhobi hivyo watoto wakike wakizaliwa kipindi hicho hupewa jina hili.

GHATI
Ghati, hutokana na neno la kimaumbile yaani umbile la mwanamke (uke). Hiyo Ghati maana yake ni *oghotia* ikimaanisha kupasuka au Kati. Kwamba wamepasuka ndo maana wanabeba ujauzito. Hili ni jina la kuenzi umbile la wanawake.

MILA NA DESTURI ZA WAKURYA

NDOA KWA WAKURYA
Ndoa za kimila. Kwa Wakurya.
Nyumba nthobhu, mwanamke aliyezaa watoto wa kike tu, ili atakapokufa baadae nyumba yake isitoweke huamua kuoa binti wa kuendeleza uzao wa nyumba yake.
Nyumba mboke ni kama mwanamke hakuzaa kabisa iwe binti wala mvulana, huyu huoa ili apate uzao.

Nyumba ntune ni kama kijana alizaliwa kwao na vijana wengine au peke yake, lkn bahati mbaya akafa kabla ya kuoa hasa kama alikuwa amepita umri wa utoto (ubhulisia). Hivyo familia hukaa na kupanga kuoa mke wa kufufua jina la kijana huyo aliyekufa.

Nyumba nyana ni aina ya ndoa ambayo mwanaume anayeoa ni taahira au kilema au zezeta. Kwa kuwa jina la mwanaume halipotei ukuryani, basi ndugu wa familia huombwa kuoa na kuzaa watoto lkn watoto ni wa huyo kilema ambaye kwa kawaida anakuwa hawezi majukumu ya kutungisha au kulea mke na watoto.

Nyumba nguru, inatokea kama familia haikubahatika kupata mtoto wa kiume mapema, lkn baadae akazaliwa, wazazi wakiwa wazee na wamekata tamaa. Huyo mtoto huolewa mwanamke ambaye huja kuzaa kuendeleza uzao wa mtoto. Mtoto huyu akikua huchagua aidha kukubali huyo mke au vinginevyo lkn mwisho wa siku ni familia yake.

Eteto ni aina ya ndoa ya kawaida. Mwanaume anaoa mke wake au mke wa pili (okohareka).

Ikumbukwe Kuwa, awali mwanaume wa kuoa aina ya ndoa hapo juu ni yule aliyechaguliwa kutoka kwenye ukoo au familia ya wahusika.

Namna ya kuoa ilikuwa, ukiwa Mkubwa Baba yako anakwambia Uoe hivyo wazazi walikuwa na jukumu kubwa kukuchagulia mchumba na kulipa mahari, ila kama wewe mwenyewe umempenda binti ukawaambia wazazi wakamkataa inabidi utafute mahari umtolee na inakuwa mwanzo wako kujenga nyumba yako na kuhamia.

Ila kama wazazi watataka ujitenge walikuwa wanakugawia mali za kuanzia maisha. mara nyingi wakurya walikuwa wanaanza kujitenga kuanzia kijana mkubwa hadi wa mwisho anabakia na wazazi kwenye eneo husika.

Binti wa kikurya akitaka kuolewa aidha unaweza kuongea naye mkakubaliana halafu unakwenda kuongea na wazazi wakakupangia wanahitaji ng'ombe wangapi, kama una uwezo wa kutoa mahari hiyo basi unapanga harusi. Ila kumtorosha Binti wa kikurya ilikuwa ni kosa kubwa sana na unakuwa umekosea ukoo mzima hivyo huamua kuja kuchukua mahari kwa nguvu na kama hauna kitu uchachezea kipigo.

SHEREHE ZA WAKURYA
Wwakurya wana sherehe maalumu ambazo husherehekewa baada ya mavuno, hivyo hata harusi ikipangwa mara nyingi hupangwa kwa kukadiria mavuno yamemalizika, hivyo watu hualikwa kuja kusherehekea wakijua kuwa hamna kazi za muhimu kama vile kilimo.

Wakurya wakati wa harusi huambiana na kukaribishana kwenye harusi bila ubaguzi na kila mtu anayekuja kwenye harusi lazima anywe (Togwa au Pombe) ale na kushiba (Ugali na Nyama). Watoto, Vijana, Wazee na Wanawake hukusanyika pamoja na kula pamoja kufuatana na makundi haya.

SHEREHE ZA TOHARA (SARO)
Hizi ndizo sherehe ambazo huamsha hisia za furaha katika koo za kikurya na mara nyingi zilikuwa zinafanyika kuanzia mwezi wa nane hadi wa 12 ila kwa sasa hufanyika mwezi wa 12 tu kwasababu rika inayoruhusiwa kutahiliwa wapo shule.

SHERIA ZA KUHITIMU (ISUBO)
Katika kabila la wakurya kuna mafunzo ambayo hutolewa kwa watu wa makamo ambapo mtu anapohitimu hutunukiwa heshima kubwa sana (Umusubi). Pia sherehe kubwa hufanyika wakati wa kutunukiwa heshima hiyo (isubo).

FB_IMG_1561564514253.jpeg
 
Back
Top Bottom