Ili kuleta mgawanyo sawa wa raslimali za taifa, utumishi serikalini usizidi miaka kumi

comte

JF-Expert Member
Dec 11, 2011
8,222
5,946
1146004
 
Tunawaona Watumishi wanafanya kazi mpaka wanastaafu hawajafanya kitu,hoja sio mpaka ufanye kitu ,miaka 10 tayari una mtaji na uzoefu,mpishe na mwingine
Yatakua Maajabu ya Dunia haya...sababu kubwa ni nini asa ya kufanya hivyo. Kuboresha utendaji wa kazi au kila mtu aonje kazi serikalini
 
Kwa vile huna kazi unataka wenzako nao wasiwe na kazi, hivi kwa mishahara hii miaka kumi utakuwa umefanya nini la maana.

Walioko kwenye ajira ndio huwa wanawakejeli wengine kwa kusema hawataki kazi, hivyo kuwe na muda miaka 10-15 unatoka wanaingia wengine kisha ukajiajiri.
 
Yatakua Maajabu ya Dunia haya...sababu kubwa ni nini asa ya kufanya hivyo. Kuboresha utendaji wa kazi au kila mtu aonje kazi serikalini

Yes maana huo ndio mgawanyo wa keki ya taifa.
 
Mugabe anachekesha mbona yeye alikaa miaka kibao hakuondoka Hadi jeshi likamuondoa.Anyway Hilo wazo no zuri kwa baadhi ya sekta kutengeneza jenerali wa jeshi,daktari bingwa,profesa hiyo miaka kumi midogo.Nchi itakuwa haina madaktari bingwa,maprofesa na magenerali wa jeshi ushauri wako wa miaka Kumi ukifanyiwa kazi
 
Sawa!In vizuri ruhusa itoke kwa anayetaka kustaafu kwa hiari yake afanye hivyo hakuna Hana ya Ulazima was kusubiri miaka 55. Hats kama nimetimiza miaka 40 na nahitaji kustaafu sheria iniruhusu . Tuanzie hapo kwanza!
 
Ni sawa na kusema timu ibadili kikosi kuzima kila mwaka. Miaka kumi ndo mfanyakazi yupo kwenye peak anatakiwa arudishe fadhila ya uzoefu aliopewa na mwajiri.
 
Tatizo kubwa la wazo hili ni kwamba mfanyakazi anakusanya uzoefu kadiri anavyoendelea, hivyo shirika litafaidikaje na hiyo rasilimali? usifikirie tu gharama za kumlipa mshahara, fikiria utakamuaje uzoefu anaoupata kwa faida ya shirika?
 
uko sahihi
Hiyo miaka Kumi Ni ya kutengeneza expert Sasa unatengeneza akishafikia u expert unamstaafisha wakati hapo ndio anatakiwa kuanza kuonyesha uwezo wake na kuleta faida.
 
uko sahihi
Hiyo miaka Kumi Ni ya kutengeneza expert Sasa unatengeneza akishafikia u expert unamstaafisha wakati hapo ndio anatakiwa kuanza kuonyesha uwezo wake na kuleta faida.
Ndio maana simuelewi kabisa Magufuli anapowastaafisha maprofesa, wakati ndio wanaiva. nchi za wenzetu profesa anaendelea kutumika hata anatumia wheelchair. sasa huku kwetu sijui kwa sababu maprofesa tunawa-abuse na kuwa-misuse mpaka wanakuwa vichekesho. lakini haitakiwi iwe hivyo kabisa. across the board mfanyakazi anakuwa mzoefu anavyoendelea, na inatakiwa mikakati ya kukamua uzoefu huo na pia kuhakikisha kwamba kuna mtu wa kumrithi ili kuhifadhi uzoefu katika shirika.

udhaifu mkubwa wa zoezi la kuondoa wafanyakazi wa VYETI FEKI pia ulikuwa hapo. kuna watu walikuwa wamepewa mafunzo kazini na wataalamu kutoka nje. huo ujuzi walioupata haupatikani popote hapa nchini. sasa unaposema mradi hana cheti rasmi au halali, kumbe ana ujuzi kaupata kazini, ni HASARA KWA TAIFA
 
Yatakua Maajabu ya Dunia haya...sababu kubwa ni nini asa ya kufanya hivyo. Kuboresha utendaji wa kazi au kila mtu aonje kazi serikalini
Issue ni kuboresha utendaji ni vema utumishi ukawa wa Mikataba mtu anapimwa kwa mkataba walio wekeana kwa muda fulani akishindwa analipwa haki zake anaondoka sio huu ukiajiriwa basi mpaka ufe hata kama utendaji wako hauna tija
 
mzee kwa mishahara ya bongo hii sera haifai kabisa. utaliza na kuua watu kwa misongo ya mawazo. kama mtu anafanya kazi hata miaka minne na hawezi nunua hata kiwanja achilia mbali ujenzi wa nyumba unategemea nini ?
sio kama hapendi, ni level tu ya mshahara alionao ndio maana anashindwa kufanya hivyo na kujikuta anajenga nyumba uzeeni
 
Kwa vile huna kazi unataka wenzako nao wasiwe na kazi, hivi kwa mishahara hii miaka kumi utakuwa umefanya nini la maana.

Ingefaa endapo

Umri wa kustaafu kwa hiari uwe miaka 40 - 50 baada ya kufika miaka 50 mtu astaafu kwa lazima...

Masaa ya kufanya kazi yapunguzwe iwe masaa 7 kuanzia saa 2 asbh Hadi saa 9 mchana.

Au siku za kufanya kazi ziwe 6 jumatatu Hadi jumamosi wapige kazi lakini masaa ya Kazi yapunguzwe yawe masaa 6 kwa siku.
 
Tatizo serikalini wanatoa maslahi duni kiasi kwamba inakuwa ngumu kutoa contracts za miaka 2-5, mtu ataondoka bila kuwa na uwezo wa kununua hata baiskeli.....huu mfumo uliopo ndo unawapa unafuu serikali kwa sababu wanatoa mishahara kiduchu na kuweza kujikopesha michango ya watumishi wake ambayo wanachangia kila mwezi kwenye mifuko ya kijamii...
 
Back
Top Bottom