Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 48,705
- 149,939
Nafikiri wakati umefika tuwe na limit ya mtu kumiliki ardhi.Mtu mmoja asiruhusiwe kumiliki zaidi ya ekari tano za shamba na pia kuwe na limit ya mtu kumiliki kiwanja/viwanja vilivyopimwa na ikiwezekana tuwe na square meter maalumu za kiwanja kama maximumu kwa mtu mmoja.
Sheria iruhusu wale tu wanaotakama kumilki mashamba/maeneo makubwa kwa ajili ya kufanya uwekezaji wa mashamba au viwanda na ambao watatoa ajira kwa watu wengine na wao piwa wawe na limit maalumu ambayo itaweza kuongezwa kwa ruhusa maalumu ya raisi na si vinginevyo.
Pia,sheria itoe adhabu kali kwa watakaoikiuka ikiwa ni pamoja na ardhi husika kutaifishwa iwapo mtu atamiliki ardhi kubwa kwa ujanjaujanja ikiwamo kutumia majina ya watu wengine kama vike ndugu,jamaa na marafiki.
Tusiendelee kuruhusu watu wenye uwezo wa kifedha kuendelea kuhodhi maeneo makubwa ya ardhi ili hali wananchi wengine hawana ardhi.
Leo hii kuna watanzania hawana uwezo wa kununua/kumiliki ardhi lakini kesho na keshokutwa mtanzania huyu nae atakuja kuwa na uwezo huo hivyo ni lazima alindwe.Kila mtu ana haki ya ardhi na umasikini usiwe sababu.
Hili likitushinda basi tuwe na sheria ya ku-control uzazi kama China vinginevyo tutakuja kupigana vita ya ardhi miaka ijayo.
Tatizo la ardhi nchii hii pengine ni kubwa kuliko hata tatizo la ajira na ni bomu linalosubiri kulipuka.