Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 57,103
- 128,721
Wanabodi, Hii ni makala yangu kwenye Gazeti la Nipashe la Jumapili ya jana.
Short version for Gen ZiiInasemekana GenZii hawana time kusoma makitu marefu, hivyo Nawawekea short version kwa numbers
- Dini zote zinafundisha utii kwa mamlaka halali za nchi, kwa sisi Wakrsto tunafundishwa kumpa Mungu yaliyo ya Kimungu na kumpa Kaisari yaliyo ya Kaisari, ikiwemo kulipa kodi na utii kwa mamlaka halali za nchi.
- Rais Samia baada ya kutangazwa na INEC kuwa ndiye mshindi, tangazo hilo ndio hitimisho la uchaguzi, na mshindi aliyetangazwa kushinda uchaguzi huo anakuwa ni mshindi halali kabisa kisheria hata kama ushindi wake umepatikana kwa bao la mkono na kugharamiwa na damu za Watanzania.
- Kufuatia ripoti za waangalizi wa uchaguzi kuwa uchaguzi, kuna watu wanadhani kutokuwa huru na haki, maana yake uchaguzi ni haramu.
- Tanzania tuna changamoto ya kutafsiri sheria, kuna tofauti kati ya uhalali wa kisheria na haki ni vitu viwili tofauti.
- Japo uchaguzi ulikumbwa na dosari, kwa mujibu wa Katiba yetu, Tume ya uchaguzi INEC, ikiisha mtangaza mshindi, uamuzi huo ni wa mwisho, final and conclusive, hata kama kulitokea dosari kiasi gani, likiwemo bao la mkono, matokeo haya yanakuwa ni matokeo ya halali kisheria, hata kama sio matokeo halali ki haki!.
- Kufuatia uhalali wa kisheria wa matokeo ya uchaguzi Rais Samia baada ya kuapishwa anakuwa ni rais halali kisheria, hivyo ni lazima aheshimiwe na wote kwa ile heshima ya lazima ya wajibu wa kuheshimu mamlaka halali.
- Japo Rais Samia ni Rais halali kisheria, sio lazima awe Rais halali ki haki kwasababu haki na sheria ni vitu viwili tofauti, kuna vitu ni halali kisheria lakini sio vya haki, na kuna vitu ni vya haki lakini sio halali.
- Neno halali, haramu batili na isiyo halali ni hoja za kisheria, sio kila kisicho halali ni haramu, kuna vitu sio halali lakini sio haramu.
- Kitendo cha INEC kumtangaza Rais Samia ndie ameshinda uchaguzi kinamfanya Rais Samia kuwa mshindi halali hata kama uchaguzi ulikumbwa na dosari za vurugu na maandamano.
- Mahakama ni mamlaka halali, mshindi akiisha apishwa, uapisho huo umemhalalisha kuwa rais halali wa Tanzania.
Ushauri Wangu- Japo uchaguzi umesababisha madhara kwa vifo na uharibifu wa mali, hivyo kugharamiwa na damu za Watanzania watu wana machungu na hasira, tusiendelee kuchochea moto kwa kunyoosheana vidole kwa kubambikiana kesi za uhaini, badala ya tujikite kwenye kuliponya taifa.
- Tuendelee kupeana pole wote kwa yote na tuiombe serikali yetu, ikubali kutoa msamaha wa jumla kwa wahusika wote. Tumeona waandamanaji wakipandishwa kizimbani, kwa kubambikiwa kesi ya uhaini ambayo hukumu yake ni kifo, tunaomba na wauwaji nao washitakiwe kwa kesi ya mauaji ambayo nayo hukumu yake ni kifo.
- Kilichotokea ni matokeo tuu ya uzembe, jeuri na kiburi cha serikali yetu kutokuwa sikivu. tutibu chanzo na serikali yetu ikubali to bear all the responsibilities of its own making.
- Haki huinua Taifa (Mithali 14:34) na haki na amani vinabusiana (Zaburi 85:10) wenye kutoa hukumu dhidi yetu na dhidi ya wengine watoe hukumu kwa haki
- (Quran 4:58) na Haki ifanywe kipaumbele (Quran 16:90) tudumishe Tanzania ya uhuru na umoja na zaidi tujenge Tanzania mpya yenye haki na furaha ambavyo ni vilele vya amani ya kweli.
Mungu Ibariki Tanzania
Paskali