Ili CHADEMA ifanikiwe malengo yake unaishauri ifanye nini?

Ili CHADEMA ifanikiwe malengo yake unaishauri ifanye nini?

Kuna baadhi ya watu husema CHADEMA inakosea jinsi ya kufanya siasa zake. Jee ili ifanikiwe kisiasa, CHADEMA inatakiwa ifanyeje siasa zake?
Ifuate ushauri wa Marehemu Lowassa chama ki-graduate kutoka harakati kuwa cha siasa zenye makengo ya kushika dola sio malengo ya kumfurahisha Mariah sarungi maisha yamebadilika watanzania wanataka kusikia sera sio kelele na maandamano hata sehemu sio ya kushupaza shingo lakini chadema wanashupaza ndio maana kila tukio wanajikuta wale wale tu bila kuungwa mkono na wananchi...
 
Watarget kwenye shida za wananchi wakiwashe ndio watafanikiwa ila sio shida za kisiasa watz wakereketwa wa siasa ni wachache sana
 
Ifuate ushauri wa Marehemu Lowassa chama ki-graduate kutoka harakati kuwa cha siasa zenye makengo ya kushika dola sio malengo ya kumfurahisha Mariah sarungi maisha yamebadilika watanzania wanataka kusikia sera sio kelele na maandamano hata sehemu sio ya kushupaza shingo lakini chadema wanashupaza ndio maana kila tukio wanajikuta wale wale tu bila kuungwa mkono na wananchi...
Reform kwanza wananchi watasikia sera vizuri tu
 
Mbona NCCR na ACT zinafanya siasa za kujikomba so called "kujadili issues", ila nao wanalia kuibiwa kura na kuenguliwa wagombea. CCM ni wanafki sana hata ujikombe bado watakuibia tu kura maana wao sio wafuasi wa demokrasia.
 
Reform kwanza wananchi watasikia sera vizuri tu
Reform haiwezi kuja kwa mtindo huo kwa wananchi wa tanzania jua kwanza sio punda ndio maana hata wakiona mtu mtaani ana silaha lazima wakatoe taarifa...
 
Kuna baadhi ya watu husema CHADEMA inakosea jinsi ya kufanya siasa zake. Jee ili ifanikiwe kisiasa, CHADEMA inatakiwa ifanyeje siasa zake?
Wabadili namna wana approach politics za hii nchi. Wameshaonyeshwa namna wanapigwa vita na watu ambao hata sheria hawafuati na wana double standards
 
Kwani hao chadema wanatembea na silaha kudai reform?
kama alivyouliza mleta mada nimesema chadema kiondoke kwenye harakati wanazo shauriwa na Mariah sarungi wajikite kwenye siasa...sijui wewe maoni yako yalikuwa yapi...
 
Mbona NCCR na ACT zinafanya siasa za kujikomba so called "kujadili issues", ila nao wanalia kuibiwa kura na kuenguliwa wagombea. CCM ni wanafki sana hata ujikombe bado watakuibia tu kura maana wao sio wafuasi wa demokrasia.
Stori za kufikirika...
 
kama alivyouliza mleta mada nimesema chadema kiondoke kwenye harakati wanazo shauriwa na Mariah sarungi wajikite kwenye siasa...sijui wewe maoni yako yalikuwa yapi...
Nduguzo huwa wao wapo wapi?kama sii uonevu,utekaji,poteza ama?
 
Kuna baadhi ya watu husema CHADEMA inakosea jinsi ya kufanya siasa zake. Jee ili ifanikiwe kisiasa, CHADEMA inatakiwa ifanyeje siasa zake?
1. Kujijenga kiuchumi, ni muhimu sana kuwa na vyanzo vingi vya mapato. Mbowe alifeli sana eneo hili, ilipaswa kipindi tunapata ruzuku ya mabilion kwa mwaka ndio tungewekeza kwenye majengo na viwanja leo hii tusingekua hapa tulipo.

2. Kuanzisha media, ni muhimu sana kuwa na media imara both mainstream kama ITV au Online media kama za chadema TV n.k hii itasaidia sana kufikisha sera, habari na agenda za chama kwa watu wengi kuliko sasa hivi TV zinaogopa kuweka habari zao.

3. Kuelekeza nguvu kwa wananchi, mfano kuandaa maandamano ya kupinga ukosefu ajira, CCM iliahidi ajira milioni 10 mwaka 2020 inabidi wananchi wazidai. Serikali iliahidi meli 5 hapa Pwani kwa vijana ila mpaka leo kimya, inatakiwa watu waandamane kudai hizo ahadi walizopewa. Kuelekeza nguvu huko kunawafanya wananchi wapambane na CCM bila wao chadema kuingia kwenye equation.

Odinga ametumia sana hii mbinu utasikia walimu wamegoma, vijana wanadai ajira, wamama wanadai bei ya unga ishuke n.k so hasira kwa serikali inapanda mwishowe support kwa uponzani inapaa sana.

Lakini haya yote bila reforms za uchaguzi, bado Chadema haiwezi kushinda chaguzi yoyote.
 
Kuna baadhi ya watu husema CHADEMA inakosea jinsi ya kufanya siasa zake. Jee ili ifanikiwe kisiasa, CHADEMA inatakiwa ifanyeje siasa zake?
1. Tengenezeni mtandao makini wa wadau wa maendeleo ya chama, nje na ndani ya nchi. (Wakati wa utawala wa JK mliwahi kufanya hiki kitu) na wadau wengi mfano Mustafa Sabodo walitoa pesa nyingi kwa ajili ya ujenzi wa chama! Ila kwa bahati mbaya nyingi mlizitafuna kupitia zile oparesheni zenu zisizo na kichwa wala miguu mfano Sangara, sijui ukuta, nk.

2. Jengeni ofisi za chama nchi nzima yakiwemo maeneo yote ya vijijini na mjini! Na kuwepo na uongozi imara.

3. Nendeni mkajifunze mbinu walizotumia wenzenu mfano Zambia, Malawi, Botswana, Ghana, Senegal, nk. Za kuviondoa vyama tawala madarakani kupitia sanduku la kura.

4. Achaneni na siasa za harakati maana policcm wapo kwa ajili ya kujeruhi, kuua, kutesa, kupora mali za watu, nk. Kwa kisingizio cha kuzuia maandamano na mikutano mnayo itisha. Na badala yake mngejikita zaidi kwenye kutoa elimu ya uraia kwa wananchi, kama wanavyofanya viongozi wenu kwenye mikutano yao ya hadhara! Yaani wananchi wanatakiwa waelimishwe kutokana na ukweli kwamba wengi wao ni wajinga kupitiliza.
 
CHADEMA wapo vzr. Hasa uongozi huu mpya hakika umeleta ufufuo. Kilichobaki ni kila mwananchi mwenye akili timamu kuwaunga mkono. Kuwaelimisha wafungwa wa fikra naoiona CHADEMA kama adui kumbe ni mkombozi wao kuwatoa kifungoni.
 
Moja kama malengo ni ya wenyenchi ambao ni wananchi iachane na malengo yake bali ianze kufuata malengo ya wananchi directly (hilo ndilo eventually litawapatia their secondary motive); After all kwani malengo ya wenye nchi na ya kwao yana tofauti ?!!!!

Ila kama malengo ni kama ya wanasiasa na vyama vingine vyovyote duniani kupata kura za kwenda kutawala basi waendelee kupigania viti kwa propaganda, ulaghai na by any means necessarily as it politics nowadays (Populists wanashinda sana sasa hivi ulimwengu) refer kina Trump

Binafsi nadhani ni bora mtu kusimamia your core values no matter hata kama zinakupatia Kura ama hapana cha kufanya ni kuwaelimisha watu kwamba your core values are better than the alternative (sadly hizo sio siasa za karne hii)
 
Back
Top Bottom