Ili CHADEMA ifanikiwe malengo yake unaishauri ifanye nini?

Ili CHADEMA ifanikiwe malengo yake unaishauri ifanye nini?

4. Achaneni na siasa za harakati maana policcm wapo kwa ajili ya kujeruhi, kuua, kutesa, kupora mali za watu, nk. Kwa kisingizio cha kuzuia maandamano na mikutano wanayoizuia pasipo na sababu za msingi. Badala yake mjikite zaidi kwenye kutoa elimu ya uraia kwa wananchi, kama wanavyofanya viongozi wenu kwenye mikutano yao ya hadhara! Yaani wananchi wanatakiwa waelimishwe kutokana na ukweli kwamba wengi wao ni wajinga kupitiliza.[/I]
[/QUOTE]
Mbona Mbowe alikua mtu wa diplomasia na alianza mpaka maridhiano ila bado wakaengua wagombea wa chadema? Au Nccr ile 2020 si walitengeneza ushirikiano na CCM kabisa wakawa wanakishambulia chadema tu ila bado wagombea wao walienguliwa.
 
CHADEMA imekuja mapema sana.

Watanzania wengi hawaelewi maana halisi ya demokrasia wala utawala bora. Nimekutana na watu wengi hata wenye digrii na kazi za kitaalamu wasioelewa wala kuona umuhimu wa demokrasia.

Wanaona katiba mpya, tume huru, reforms (no reforms, no election) kama mkakati ama wa kuiondoa CCM madarakani au kuwaingiza wapinzani kina Lissu Ikulu, BASI!

Hawaelewi kuwa demokrasia inaweza hata kuwaimarisha CCM madarakani. Kwa mfano, kuna wakati naamini kuwa 2020 Magufuli angehakikisha uchaguzi kuwa huru na wa haki angeshinda uRais kwa kura halali kabisa ingawa CCM ingepoteza wabunge wengi. It was a lost golden opportunity for JPM & his flock of ardent devotees.

Hadi siku uelewa wa demokrasia utakapowafikia wengi halafu wawe WAMEPIGIKA HASA ndipo CHADEMA itakapoeleweka na hakuna nguvu ya dola itakayothubutu kuanzisha vagi na hicho chama. Itakabiliana na inferno ya people’s power katika ubora wake.
 
Kuna baadhi ya watu husema CHADEMA inakosea jinsi ya kufanya siasa zake. Jee ili ifanikiwe kisiasa, CHADEMA inatakiwa ifanyeje siasa zake?
  1. Kiunganishe chama, kiondoe makundi (team Mbowe, team Lissu) na kuepuka mipasuko ya ndani. Hakuna manufaa ambayo chama itakipata kwa kupigana wenyewe kwa wenyewe, mfano mzuri ikiwa mambo yanayoendelea kwa sasa ndani ya chama.

  2. Iweke mikakati ya kukijenga chama from the grassroot na kuzipa nguvu ya kiuchumi ngazi za kata, wilaya, mikoa kuendesha shughuli za chama kutokea chini na hasa vijijini na kwenye miji midogo ambako ndiyo kuna wapiga kura wengi.

  3. Ijikite kwenye mbinu za kuchukua dola kwa kukiimarisha chama kiuchumi na kiutendaji. Pia kuwe na mikakati ya kuongeza idadi ya wabunge, madiwani na wawakilishi ambao ni wapaza sauti za wananchi na watunga sheria.

  4. Chama kiwe tayari kupokea criticism na kujiboresha kwenye maeneo yenye mapungufu. Si kila anayekosoa hakitakii chama mema, tuwe tayari kupokea maoni tofauti tofauti hasa kutoka kwa wanachama wetu.
 
CHADEMA imekuja mapema sana.

Watanzania wengi hawaelewi maana halisi ya demokrasia wala utawala bora. Nimekutana na watu wengi hata wenye digrii na kazi za kitaalamu wasioelewa wala kuona umuhimu wa demokrasia.

Wanaona katiba mpya, tume huru, reforms (no reforms, no election) kama mkakati ama wa kuiondoa CCM madarakani au kuwaingiza wapinzani kina Lissu Ikulu, BASI!

Hawaelewi kuwa demokrasia inaweza hata kuwaimarisha CCM madarakani. Kwa mfano, kuna wakati naamini kuwa 2020 Magufuli angehakikisha uchaguzi kuwa huru na wa haki angeshinda uRais kwa kura halali kabisa ingawa CCM ingepoteza wabunge wengi. It was a lost golden opportunity for JPM & his flock of ardent devotees.

Hadi siku uelewa wa demokrasia utakapowafikia wengi halafu wawe WAMEPIGIKA HASA ndipo CHADEMA itakapoeleweka na hakuna nguvu ya dola itakayothubutu kuanzisha vagi na hicho chama. Itakabiliana na inferno ya people’s power katika ubora wake.
Well said bado kuna wajinga wengi sn
 
  1. Iunganishe chama, iondoe makundi (team Mbowe, team Lissu) na kuepuka mipasuko ya ndani. Hakuna manufaa ambayo chama itakipata kwa kupigana wenyewe kwa wenyewe, mfano mzuri ikiwa mambo yanayoendelea kwa sasa ndani ya chama.

  2. Iweke mikakati ya kukijenga chama from the grassroot na kuzipa nguvu ya kiuchumi ngazi za kata, wilaya, mikoa kuendesha shughuli za chama kutokea chini na hasa vijijini na kwenye miji midogo ambako ndiyo kuna wapiga kura wengi.

  3. Ijikite kwenye mbinu za kuchukua dola kwa kukiimarisha chama kiuchumi na kiutendaji. Pia kuwe na mikakati ya kuongeza idadi ya wabunge, madiwani na wawakilishi ambao ni wapaza sauti za wananchi na watunga sheria.

  4. Chama kiwe tayari kupokea criticism na kujiboresha kwenye maeneo yenye mapungufu. Si kila anayekosoa hakitakii chama mema, tuwe tayari kupokea maoni tofauti tofauti hasa kutoka kwa wanachama wetu.
Umeandika point, 5. Chama kiendelee kusaidia wananchi wanaonewa na polisi au mahakamani kwa kuwawekea mawakili, yani kila wilaya kuwe na wakili mmoja au 2 wa kutetea wananchi
 
1. Kujijenga kiuchumi, ni muhimu sana kuwa na vyanzo vingi vya mapato. Mbowe alifeli sana eneo hili, ilipaswa kipindi tunapata ruzuku ya mabilion kwa mwaka ndio tungewekeza kwenye majengo na viwanja leo hii tusingekua hapa tulipo.

2. Kuanzisha media, ni muhimu sana kuwa na media imara both mainstream kama ITV au Online media kama za chadema TV n.k hii itasaidia sana kufikisha sera, habari na agenda za chama kwa watu wengi kuliko sasa hivi TV zinaogopa kuweka habari zao.

3. Kuelekeza nguvu kwa wananchi, mfano kuandaa maandamano ya kupinga ukosefu ajira, CCM iliahidi ajira milioni 10 mwaka 2020 inabidi wananchi wazidai. Serikali iliahidi meli 5 hapa Pwani kwa vijana ila mpaka leo kimya, inatakiwa watu waandamane kudai hizo ahadi walizopewa. Kuelekeza nguvu huko kunawafanya wananchi wapambane na CCM bila wao chadema kuingia kwenye equation.

Odinga ametumia sana hii mbinu utasikia walimu wamegoma, vijana wanadai ajira, wamama wanadai bei ya unga ishuke n.k so hasira kwa serikali inapanda mwishowe support kwa uponzani inapaa sana.

Lakini haya yote bila reforms za uchaguzi, bado Chadema haiwezi kushinda chaguzi yoyote.
Sahihi kabisa, reforms kwanza...kwa sasa kuitenganisha ccm na polisi hata kwa darubinini ngumu. Reforms za uchaguzi, reforms za katiba. Baada ya hapo mengine yatafanyika, we MUST play on neutral ground.
 
CHADEMA imemaliza wajibu wake na imefanya vyema. Kazi imebaki kwa wananchi aidha tuendelee kutawaliwa na wakoloni weusi( CCM ) au tuingie barabarani na kumngoa adui CCM.
 
Wazo zuri. Ishughulike na CCM kivipi?
Mfano wanaweza kujijenga kwa wananchi kwa kuweka mawakili kila Wilaya kusaidia wananchi kwenye uonevu hasa polisi na mahakamani bure, mabaraza ya ardhi na nyumba kuna kesi nyingi sn lakini wananchi wamebaki kama yatima, kijingine babala ya kudai tume huru wanaweza wakadai tupige kura kidijitali ambayo ndiyo komesha ya CCM badala ya kupiga kura manually tunaweza kupiga kwa mashine(Electronic Voting Machines)
1745583207473.png
 
Back
Top Bottom