Pamoja na matukio mengi ambayo tumekuwa tukijadili, kuna hili la chenji ya rada naona bado hatujafahamishwa limeishia wapi.
Tuliambiwa kuwa Uingereza walishaturudishia hizo pesa na tukaahidiwa kuwa fedha hizo zitanunulia madawati ili watoto wetu wasiendelee kukaa chini.
Je kuna mwenye habari kwamba hayo madawati yalishanunuliwa kwa hiyo fedha? Nani alipewa jukumu la kuratibu matumizi ya hizo fedha?
Naomba, hasa kwa ndugu Wabunge, hilo swali liulizwe bungeni ili wananchi waweze kujua fedha hizo zimetumika vipi.