Ilani ya CHADEMA Hii Hapa

Regia Mtema

R I P
Nov 21, 2009
2,970
864
Haya kwa wale ambao hatuifahamu ilani ya CHADEMA ya 2005 nimeona ni vema nikawaletea ilani hii ya Uchaguzi Mkuu wa Rais,Wabunge,Wawakilishi na Madiwani ili tuichambue, kuijadili na kuikosoa.
 
Attachments

  • ILANI CHADEMA 2005.doc
    285 KB · Views: 224
Kutoa ahadi kila mtu anaweza, kigumu ni kuonyesha hiyo mipango yote ita cost pesa ngapi na zitatoka wapi?

Ahadi pekee zisizo na kipimo chochote ni ngumu kweli kuzipima.

JK alisema ataunda kazi milioni moja, tunamkamata kirahisi maana aliweka namba na ni tofauti na mtu akisema ataongeza ajira nyingi. Nyingi zinaweza kuwa kumi au milioni mbili. Tumieni SMART kupanga mipango yenu.
 
KAMANDA MPIGANAJI
left_pic2.gif
 
kamanda kweli chadema wanaona mbali kuliko chama chochote kile hapa afrika chadema ipo juuu kwa sana
 
Huyo Kilewo jana alikuwa kwenye NEC ya CCM leo anaifagilia CHADEMA JF, kweli JF tuna wasanii. Ile habari yote ya jana atakuwa alipika tu.
 
Itaongeza ajira. Itatengeneza ajira kuimarisha sekta za ujenzi, madini, kilimo, utalii na huduma za jamii. Itaweka kipaumbele kwa sekta za uchumi zinazotengeneza ajira kwa watu wengi mfano kilimo. Kwa kuwa kipaumbele kimewekwa kwenye elimu, CHADEMA inaamini kuwa shule nyingi zaidi zitajengwa. Kwa hivyo basi waalimu zaidi wataajiriwa. Vilevile, ajira nyingine zitatokana na sekta binafsi. Wananchi wengi hasa vijana watajengewa mazingira mazuri kwa kupewa mikopo kwa ajili ya kuanzisha miradi mbalimbali. Itatoa leseni za bure na likizo ya kodi kwa vijana wafanyabiashara ndogondogo na vijana wanaojishughulisha na uzalishaji mali.
 
Angalia moja ya kipengele cha ILANI YA CCM kuhusu viwanda hivi ccm wako serious bado Tanzania inajivunia na kutegemea viwanda kweli viwanda vyenyewe viko wapi au vile vya Mohamed Enterprises vya kutengeneza pipi na kashata CCM huwa wanaorodhesha kila kitu alimradi yaonekane hata kama hayatekelezeki Gender Sensitive tuwekee Ilani ya CCM ili tuweze kulinganisha vizuri

25. Jambo la tatu la kipaumbele cha CCM katika mchakato wa kujenga msingi wa uchumi wa kisasa wa taifa linalojitegemea ni mapinduzi ya viwanda na miundombinu ya kisasa.
[FONT=DGEABE+Tahoma,Bold,Tahoma][FONT=DGEABE+Tahoma,Bold,Tahoma]Viwanda ndivyo kiongozi wa uchumi wa kisasa[/FONT][/FONT]. Dhana ya viwanda inakumbatia moja kwa moja dhana ya sayansi, teknolojia na uhandisi. Viwanda vina nafasi ya kimkakati katika mchakato mzima wa kujenga msingi wa uchumi wa kisasa wa taifa linalojitegemea.
 
tuwape basi kula zetu wafanye mabadiliko ..
Mie nimechoshwa na siasa za nchi hii

Samahani kwa kutoka nje ya mada who is the original First lady naona mko wawili humu au wewe ndiye yeye, ila kwa kura huwa tunawapa wapinzani tatizo zinaibiwa
 
Ilani inaandikwa na wanazuoni kwa malipo maalum hatimaye kuriziwa na chama..hivyo kwa vyovyote "itakuwa nzuri sana" kwasababu wasomi wameandaa (profesionals)

Ilani nzuri chini ya viongozi wabovu (Mbowe na Slaa) wabinafsi na wasio na uwezo wa kuongoza na kuhamasisha wananchi ni sawa na kitabu kizuri kwa watu wasiojua kusoma...

Sioni na kama kwa aina ya viongozi waliopo huko chadema kutakuwa na kipya sana sana ni club tu ya networking..poleni sana
 
Thibitisha ubovu wa Mbowe na Dk Slaa.
 
Haya kwa wale ambao hatuifahamu ilani ya CHADEMA ya 2005 nimeona ni vema nikawaletea ilani hii ya Uchaguzi Mkuu wa Rais,Wabunge,Wawakilishi na Madiwani ili tuichambue, kuijadili na kuikosoa.

Asante sana.. ngoja tuipitie .. ila huu mwaka mmoja tu uliobaki.. wanatarajia kuwa na ilani hiyo hiyo mwaka huu maana hawakutekeleza ilani yao ya 2005 (kwa sababu hawakushika serikali).. so sidhani kama tunaweza kuwapima.
 
Unaweza kuwapima kwa kuangalia ubora wa ilani yao na mapungufu yaliyopo.Je inatekelezeka au ni too much ambitious!Ilani itabadilika kidogo kulingana na mazingira ya sasa lakini hata katika viwango vya bajeti.
 
Asante sana.. ngoja tuipitie .. ila huu mwaka mmoja tu uliobaki.. wanatarajia kuwa na ilani hiyo hiyo mwaka huu maana hawakutekeleza ilani yao ya 2005 (kwa sababu hawakushika serikali).. so sidhani kama tunaweza kuwapima.

Ukisema huwezi kuwapima utakuwa umekosea vipimo vipo vya aina nyingi hata ile will ya mtu inapimika rais wa marekani Obama alipewa tuzo ya nobel baada ya kuwa madarakani kwa miezi michache tu wakati huo alikuwa hajatekeleza hata ahadi moja lakini wenye akili zao walipima will yake wakaona huyu anafaa

siwatetei Chadema lakini ukiona wanachofanya bungeni ingawaje ni kidogo lakini kinaonekana kwa macho angalia pia halmashauri zao pamoja na kuwa zimezungukwa na urasmu mwingi lakini zinaonekana ukipima kwa quantity(uwingi) huwezi kuona vizuri jaribu kuwapima kwa quality(ubora) unaweza kuona something in it.
 
Huo ni mtazamo wako. si sawa kusema viongozi hao ni wabovu kwa kila mtu. Wanachama wa CHADEMA wamewakubali wewe utasemaje wabovu? Thibitisha ubovu wao kama wewe ni mkweli. Au wewe ni miongoni mwa akina Kafulila?

Back
Top Bottom