Ilani ya CHADEMA 2010-2015

Kuwa na Ilali nzuri ni kitu kimoja, cha muhimu hao CHADEMA wanatakiwa wawe wamejipanga vizuri kuweza kuiuza hiyo ILANI kwenye kampeni zao, vinginenvyo hiyo ilani wataisoma ''MENDE'' tu kwenye makabati na haitakuwa na maana yeyote hata kama ina tisha!
 
Nchi hii siku zote inaangushwa na mikoa ya Mwaza, tabora na Shinyanga. Kuna almost 75% ya wapiga kura halafu hawana uelewa wowote juu ya maswala ya kisiasa, wao bora liende.
 
Sasa ndo hapo mnataka mdahalo la JK ataeleza nn na llani yake ya kiimra?
Ndo maana kaingia mitini aibu atakayo pata na llani yake ataificha wapi!
 
Ni kweli kabisa MMkj, hebu angalia Majiji kama Dar na Mwanza, kama kwa huo tunaoita uelewa wao wangeonyesha nguvu zao za kura na kuukataa ubabaishaji wa CCM unadhani hali ingekuwaje? Ngome kuu za upinzani zilipaswa kuwa katika miji mikubwa na sio kama ilivyo sasa.
Na kama majiji yetu yangekuwa na nguvu za upinzani hadithi ingekuwa nyingine kabisa.
 
Licha ya kuwa na ilani nzuri CHADEMA wanatakiwa wajipange kimkakati na watawanye resource zao kwa namna kuwa kunakuwa na group ambazo zitatembelea wananchi wote wa nchi hii ili kuuza sera hizo hasa vijijini. Ukweli ni kuwa Dr Slaa hawezi kupita kila kona ya nchi hii peke yake kwa siku sabini.

Kunatakiwa kuwe na safu ya uhakika kuhakikisha kuwa kila mtanzania anafikiwa. Hii itasaidia kuondoa woga wa wapiga kura. Watu wengi wanateseka lakini wana hofu ya ccm huko vijijini na wanaogopa usipopigia kura ccm utaadhibiwa. Hii nimeshuhudia katika ziara yangu hivi karibuni Huko vijijini. Baado wananchi wanaambiwa mkichagua upinzani wataleta vita. Hivyo kama mnataka amani chagueni ccm
 
Nina wasiwasi kuwa Tanzania haina tofauti yoyote na Kenya au Zimbabwe linapokuja swala la uchaguzi. Ni bora kuhakikisha kuwa vyama vyote vinajiimarisha vya kutosha kulinda na kudhibiti na upigaji na uhesabuji wa kura kwa karibu sana.

Angalizo/Vision

Chadema wamewashinda CCM kwa kupata Kura nyingi za nafasi ya Rais, na wabunge wengi pia;
Habari mpya ni kwamba sio Chadema walioshinda, ni CCM; Kura za Tanga zilikuwa bado kuhesabiwa wakati tunatoa taarifa ya kwanza


Hilo ni Angalizo tu kwa Chadema nikimaanisha kwamba mipango yote mizuri watakayo panga 'haina maana' kama hakuna mkakati Madhubuti wa kulinda Kura, hata kama mkakati huo utawaudhi baadhi ya watu.. especially the so called 'Wanaharakati wa Human rights'

Get prepared
 
WANAJIANDAA KUCHEZA RAFU, wanajiandaa kwa mikakati yao ya kishetani, CHADEMA ni makini naamini wameng'amua. othewise ccm Wanaenda kushindwa, na wakianguka wale , hawataamka.
 
Tatizo watanzania wengi ni wanafiki...

They say one thing and they act differently...:mad2:
 
wandugu tuwekeeni attachement ya hiyo ILANI YA UCHAGUZI YA CHAMA CHETU-CHADEMA, 2010
 
Hivi wapiga kura wengi wa Tanzania hasa kule vijijii ambako ushindi wa tsunami wa ssm upo wanafahamu maana ya ilani? For sure watachagua sura na kile walichozoea?? Tatizo ni kwamba wazalendo wengi wenye uelewa wa kupiga kura na maana yake huwa hawapigi kura!!!?? Tuamke sasa, tujitolee katika kulikomboa taifa hili. Yaani tukishindwa tena kufurukuta safari hii basi itachukua muda sana kuiweka ssm chali kwa awamu nyingi zijazo.
 
So TRUE. God help us. But sadly , God helps those who help themselves.
 
Wanachohitaji CHADEMA ni mpango madhubuti wakujitangaza...wawe na mawakala kila mahali, especially vijijini.
Wanahitaji KUSIKIKA ili KUELEWEKA ili kuwapa wananchi SABABU YA KUWAPA WAO MADARAKA.Wanatakiwa wawajulishe
watu kwamba CHADEMA IS THE TO GIVE and make their lives better ,NOT TO TAKE and make it worse than it already is...which is what Chama Cha Mafisadi is all about.

PIGA KURA KAMA UNAICHUKIA TANZANIA KAMA ILIVYO NA UNATAMANI MABADILIKO!
 

Mkuu nakubaliana nawe kuwa watu wana chuki, na hasira, mfano mdogo tu ni chaguzi za Busanda, Tarime, Kiteto na Biharamulo. Hata hao wa vijijini wamechoka na si lazima sana wasome hata wakiambiwa tu itatosha. Kwenye Biblia kuna mstari unaosema "Heri asomaye na kuyasikia maneno ya kitabu hiki". Mimi nasema ambaye hatasoma atasikia na watanzania sasa wako tayari kwa mabadiliko.

Go CHADEMA!!! Go Slaa
 

Timing ya kutoa hizi sera zao ni muhimu sana kuzingatia! Kumbu kumbu zangu bila aibu CCM/CUF walisema wao ndo waanzilishi wa vita vya Ufisadi! Kwasababu hawa CUF-CCM ( naandika hivi kusudi maana kuna ndoa kati yao) wanaweza copy na kuweka kwenye ilani zao. Wasubiri hadi kampeni rasmi zianze.
 

CHADEMA mliomo humu ndani please take this a challenge and work on it. Tengenezeni ilani version ya kuwawezesha wadanganyika wa kule namanyere kuelewa, i am sure you will defeat them. Go Slaa...
 

I couldn't agree more...you can get everything right but ukikosea hapo tu umekwenda na maji. What transpired in the primaries epitomizes the magnitude and complexity of the whole problem
 
hahahahaha
wacha nicheke mie

kuna mijitu humu inaonekana ina machungu na nchi hii lakini wapi unafiki tu.

subirini octoba
 
CHADEMA mliomo humu ndani please take this a challenge and work on it. Tengenezeni ilani version ya kuwawezesha wadanganyika wa kule namanyere kuelewa, i am sure you will defeat them. Go Slaa...


we uko upande upi?

unaposema Go slaaa unamanisha kweli?
 
Je wanachama na wakereketwa wa CHADEMA NA SERA ZAKE walijiandikisha kupiga kura? Je, CHADEMA kinaweka takwimu au kumbukumbu ya "potential" wapiga kura wao kiasi kwamba waweze kuwazungukia na kuweka "birika vuguvugu" saa zote , ili siku ya kupiga kura basi kweli wajitokeze kwa wingi kukipigia chama chao kura?
Bila hivyo, ilani itawazingua lakini haitawaletea mabadiliko wanayotamani.Kadhalika, huwezi kutegemea ilani tu ndio iwabadilishe mawazo wanachama wa vyama vingine - ushabiki wa vyama ni kama ushabiki wa vitu vingine iwe ni mpira au mziki kuna loyalty fulani ambayo ni ngumu kuipindua kirahisi.Ndivyo nionavyo mimi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…