Madalali si watu wazuri. Wakati naanza kujitegemea kwa mara ya kwanza nilivyokuwa kichwa panzi nikamtafuta dalali anitafutie chumba sebule jiko. Basi akanicheki imepatikana twende. Tukaenda hadi hiyo sehemu nikaiona, yani huwezi amini nilikuwa naona kabisa ni mabondeni sijui alikuwa kaaniroga yule.Madalali ni watu wabaya sana.
madalali hawana UTU kabisa.
......
Usipokuwa makini Dalali anaweza kukuuzia kitu cha laki 1 kwa shilingi laki 3
....
View attachment 3385554View attachment 3385555
Wengi wao ni washirikina mno.Madalali si watu wazuri. Wakati naanza kujitegemea kwa mara ya kwanza nilivyokuwa kichwa panzi nikamtafuta dalali anitafutie chumba sebule jiko. Basi akanicheki imepatikana twende. Tukaenda hadi hiyo sehemu nikaiona, yani huwezi amini nilikuwa naona kabisa ni mabondeni sijui alikuwa kaaniroga yule.
Mimi nikasema nimepapenda bei, gani? Nikaambia laki na nusu, nikasema sawa hapo dalali ashaniambia anakula pesa ya mwezi. Nikaletewa mwenye nyumba, nikamwambia nalipa kodi ya mwaka mzima. Dalali kusikia hivyo, akaninong'oneza, ukilipa kodi ya mwaka mzima inabidi unipe kodi ya miezi miwili.
Na mimi nilivyokuwa fala nikampa laki tatu nzima haki.
Kesho yake narudi sasa, najiuliza mimi ndiye nimelipia mwaka huku jamani.... mbona hapafai.
Daa nimecheka hapa kwenye gari wat poo lol poo lol pplMadalali ni watu wabaya sana.
madalali hawana UTU kabisa.
......
Usipokuwa makini Dalali anaweza kukuuzia kitu cha laki 1 kwa shilingi laki 3
....
View attachment 3385554View attachment 3385555
Likija swala la madalali wa magari ogopa mno sehemu 3 dar; Sinza, Amana Ilala na Lumumba.Mwaka jana nilienda Lumumba kuweka tint gari. Kuna jamaa yangu ni dalali nikawa namtania apige picha gari naiuza milioni 10, ilikuwa IST. Jamaa alikuwa anajua namtania kwahiyo hakutilia maanani tukaendelea na story zetu.
Baada kama ya siku 2 na scroll Facebook Market place nakuta picha ya gari yangu imepostiwa inauzwa Milioni 14. Picha ni za pale Lumumba.
Nikampigia jamaa yangu wa Lumumba simu kumwambia kuwa nilikuwa namtania, akasema mbona yeye hakupiga picha wala kupost gari.
Kupiga namba iliyowekwa kwenye tangazo jamaa kadai gari atakuwa nayo kesho yake nimtafute, asubuhi kumpigia akanambia tukutane Ilala, nikaenda na Boda hadi ilala kwa dalali mwingine ambae akapiga simu tena kwa jamaa tuliokuja kugundua yupo Lumumba. Tukaenda watu 3 sasa Lumumba kwa kutumia Bajaj.
Kufika kwa jamaa wa Lumumba ikiwa nipo kwenye bajaj nikasikia na yeye anamuita yule jamaa yangu kumuuliza kuhusu ile IST iliyokuja jana yake ikasemekana inauzwa, kuwa ana mteja wa milioni 9 cash (kumbuka imepostiwa Mil. 14). Jamaa akamwambia ilikuwa ni utani tu na nani alimruhusu kutangaza biashara, jamaa likabaki linang'aa macho.
Kupitia mtu mmoja tu kusikia kwamba nauza gari bila hata kuuliza akaamua kupiga picha gari na kuipost bila hata kumjua mmiliki.
Dalali ni mithili ya majambazi yasiyokuwa na huruma maana wana uwezo wa kumzunguka mwenye mali, mteja mpaka wao wenyewe.