IKWIRIRI KWACHAFUKA-Niliandika. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

IKWIRIRI KWACHAFUKA-Niliandika.

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by MIGNON, May 22, 2012.

 1. M

  MIGNON JF-Expert Member

  #1
  May 22, 2012
  Joined: Nov 23, 2009
  Messages: 2,587
  Likes Received: 1,563
  Trophy Points: 280
  Mabomu ya machozi na vifo tayari vimetokea huko Ikwiriri na chanzo ni mapigano ya wakulima na wafugaji.
  Wakulima wameshambulia vituo vya polisi badala ya kuendelea kupigana na wafugaji,kwa nini?
  Jawabu n wazi kuwa wafugaji wana ukwasi mkubwa kuliko wakulima na kwa mfumo wa rushwa uliopo mara nyingi wanalindwa na vyombo vya dola.Kesi ya mkulima na mfugaji ni mtaji kwa askari polisi na mahakimu,niliandika na bado naandika.
   
 2. Apolinary

  Apolinary JF-Expert Member

  #2
  May 22, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 4,698
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  polen wahanga wa machafuko hayo ninaloomba viongozi wa kisiasa wasiingilie jambo hili, kwani yaweza kuwa mtaji wa chama cha kijani
   
 3. VUTA-NKUVUTE

  VUTA-NKUVUTE JF-Expert Member

  #3
  May 22, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 5,872
  Likes Received: 6,623
  Trophy Points: 280
  Basi watasingiziwa CHADEMA hapo...
   
 4. Songoro

  Songoro JF-Expert Member

  #4
  May 22, 2012
  Joined: May 27, 2009
  Messages: 4,136
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 0
  Hawa ndio watu wa kusini, Rejea vurugu za kupinga mauaji na ukosefu wa Umeme kule songea,Tandahimba mtwara walichimbisha walipocheleweshewa malipo ya Korosho,Ikwiriri Nyumba ya Ocd imegeuzwa kuni baada ya kuendekeza Rushwa kwenye kusuluhisha migogoro ya kiuchumi, Kusin hawaandaman kumpinga Meya wala Kupokea wanasiasa, ukiona wameteremka Barabarani jua sio Blablah za kisiasa ni Mambo mazito ya kijamii ndo maana huwa yanawachanganya watawala kwa sababu ni maandamano ya kijamii sio yale Yanayoongozwa na NGO za kisiasa!
   
 5. Apolinary

  Apolinary JF-Expert Member

  #5
  May 22, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 4,698
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
   
 6. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #6
  May 22, 2012
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,830
  Likes Received: 10,142
  Trophy Points: 280
  si walisema watu wa kusini wamelala? sasa inakuaje tena
   
 7. n

  nyarngato Member

  #7
  May 22, 2012
  Joined: Apr 11, 2012
  Messages: 29
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kuna ndugu zangu wanaishi ikwirir,i kuna mda kulikuwa na tetesi kuwa mashamba yao wamegaiwa wawekezaji wakikorea.. walipo enda Wilayani kweli wakataarifiwa kuwa wilaya Imetenga zaidi ya Eka 3000 kwa ajili ya mwekezaji mkorea na wao wenyewe wakiwa ndani ya hilo eneo bila kupewa taarifa.
  Wakaongea na uongozi wakijiji ikaonekana kuwa viongozi waliokuwapo mwanzo walihusishwa lkn wao hawakuhusisha wananchi, kama kawaida wananchi wakawaambia sasa wao wanakaa kwenye maeneo yao wanamsubiri muwekezaji aje wakati viongozi wa sasa wanashughulikia hilo swala kisheria.
  Sasa kwa namna hii migogoro itazidi kuwapo Ikwiriri
   
 8. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #8
  May 22, 2012
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 14,856
  Likes Received: 2,019
  Trophy Points: 280
  Naomba kusema kuwa mgogoro unaoendelea huko Ikwiriri baina ya wafugaji na wakulima ni muendelezo tu wa matukio kama haya ambayo tumekuwa tunayashuhudia katika wilaya nyingine kama vile Kilosa, Kilindi, Hanang, Arumeru, Mbarali na kwingineko. Tatizo hapa si ukwasi walionao wafugaji au umasikini wa wakulima. La hasa ila ni tatizo la kimfumo ambalo limesababishwa na serikali yetu yenyewe. Kuna tatizo la kauli mbovu na za kibaguzi ambazo zimekuwa zinatolewa na viongozi wa serikali kuhusiana na wafugaji. Mfano kama unakumbuka kauli ya PM Pinda kule bungeni ya kuwa wafugaji warudi walikotoka. Hii ni kauli mbaya sana ambayo ina tafsiri nyingi kwa wafugaji ikiwa ya kujihisi kubaguliwa kutokana na kazi yao. Pia kuna suala la uhamishaji wa wafugaji kutoka katika bonde la Ihefu mwaka 2006 pasipo utaratibu maalum na kuwapeleka katika mikoa ya Lindi, Pwani na Morogoro jambo ambalo ndio sasa linalozua maafa haya yote.

  Ombi langu kwa serikali ni kujenga mfumo bora wa kifugaji ambao utakuwa unalinda maslahi ya mifugo na wafugaji wenyewe. Tazama kuna mikakati mingi ya kilimo ambayo kwa mtazamo wa haraka utaona kuwa hakuna nafasi kwa wafugaji kujiendeleza zaidi ya leo kuambiwa ondokeni Kilombero, ondokeni Rufiji, ondokeni Mbarali, ondokeni Arumeru. Sasa wataenda wapi?
   
 9. Riwa

  Riwa JF-Expert Member

  #9
  May 22, 2012
  Joined: Oct 11, 2007
  Messages: 2,601
  Likes Received: 234
  Trophy Points: 160
  Umenena vyema mkuu Mokoyo...
   
Loading...