GAMBLER
JF-Expert Member
- Nov 22, 2009
- 303
- 11
Na Exuper Kachenje
Gazeti la Mwananchi
IKULU jana ilitoa taarifa ya kumuomba radhi mkurugenzi wa wilaya ya Ngorongoro, Kayange Jacob baada ya Rais Kikwete kukataa kumkabidhi gari la wagonjwa na kuvunja hafla iliyoandaliwa kwa ajili ya kutoa msaada huo kwa halmashauri mbili.
Katika tukio lisilo la kawaida lililotokea Ikulu siku tatu zilizopita, Rais Kikwete alimuhoji mtendaji huyo wa Ngorongoro sababu za kuonekana Ikulu siku hiyo na kuhoji aliyemualika kwenye hafla hiyo iliyolenga kukabidhi magari mawili ya wagonjwa kwa halmashauri za wilaya za Longido (Arusha) na Mbozi (Mbeya).
Rais Kikwete alisema Ngorongoro haikuwa sehemu ya halmashauri ambazo zingegawiwa magari hiyo na akaamua kuondoka kwa hasira, akiacha hafla hiyo ikizimika ghafla.
Baadaye jioni Ikulu ilitoa taarifa kuwa Rais Kikwete alimkabidhi gari mkurugenzi wa Halmashauri ya Mbozi, Levison Jeremiah Chilewa kwa ajili ya wakazi wa eneo la Kamsamba.
Juzi, Katibu wa Rais Prosper Mbenna alikabidhi gari lililosalia la wagonjwa kwa mkurugenzi wa Halmashauri ta Longido, Christian Laiser katika hafla iliyofanyika Ikulu pia.
Lakini jana, Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais ilitoa taarifa kwa vyombo vya habari ikimwomba radhi Kayange na kutoa ufafanuzi wa tukio hilo.
"Tunachukua nafasi hii kuomba radhi kwa usumbufu uliompata Bwana Kayange Jacob na kwa jinsi tukio hilo lilivyomfanya aonekane kwa wananchi.
Rais Kikwete anatambua haja ya vituo vya afya katika wilaya ya Ngongororo na wilaya nyingine nchini kupatiwa magari ya kubeba wagonjwa. Serikali inaendelea na juhudi za kununua magari hayo, na rais anaahidi kuwa katika mgao ujao na Wilaya ya Ngorongoro watafikiriwa," inasema taarifa hiyo.
Taarifa hiyo inaongeza kusema: "Tunapenda kufafanua kuwa palifanyika makosa katika kupeleka taarifa kutoka Ikulu kwamba badala ya kumuita mkurugenzi wa Wilaya ya Longido kuja kuchukua gari la wilaya yake, akaitwa mkurugenzi wa Wilaya ya Ngorongoro.
Makosa hayo yamerekebishwa, na jana, Januari 19, 2010 katibu wa rais, Ikulu, Bwana Prosper Mbena amekabidhiwa gari hilo kwa mkurugenzi wa Wilaya ya Longido, Bwana Christian Laizer."
Sakata hilo limehusishwa zaidi na utendaji wa wasaidizi wa Rais Kikwete ambao wamekuwa wakilaumiwa kwa kumsabishia kiongozi huyo matatizo kadhaa kwenye kadamnasi, likiwemo tukio la hivi karibuni la kwenda kufungua hoteli ya kitalii ambayo kesho yake ilibomolewa na Tanroads kutokana na kujengwa ndani ya hifadhi ya barabara.
Hata hivyo, taarifa hiyo ya Ikulu haijaeleza kama watendaji waliohusika na uzembe huo uliomsababishia usumbufu, kero na aibu mkurugenzi huyo wa Loliondo watachukuliwa hatua.
Mbali na matukio hayo mawili, wasaidizi wa Kikwete wamehusishwa na uzembe wa kutomuandalia rais sehemu ya kukaa wakati alipoenda kwenye misa ya mazishi ya mbunge wa zamani wa Mbeya Vijijini, Richard Nyaulawa Novemba mwaka juzi.
Wasaidizi hao walichukua kiti alichokuwa akitumia mchungaji, lakini Kikwete akakikataa na kwenda kukaa kwenye benchi pamoja na waombolezaji wengine.
Oktoba mwaka huohuo, wasaidizi wake walishindwa kumuandalia gari mke wa rais wa zamani wa Madagascar, Marc Ravalomanana wakati alipowasili nchini kwa ziada fupi.
Rais Kikwete alilazimika kuchelewa kuingia kwenye gari lake ili aelekeze wasaidizi wake jinsi ya kumpatia usafiri mke huyo wa rais mwenzake.
Katika tukio jingine, Rais Kikwete alilazimika kubatilisha uteuzi Anatory Choya kuwa mkuu wa wilaya ya Biharamulo baada ya kubaini kuwa alikuwa na kesi ya tuhuma za rushwa. Hata hivyo, Kikwete alimteua tena Choya kuwa mkuu wa wilaya ya Mbulu baada ya mahakama kumsafisha.
Katika sakata la juzi, Rais Kikwete alimuhoji Kayange maswali kadhaa ambayo yalionekana kumfedhehesha mkurugenzi huyo wa Ngorongoro.
"Wewe bwana unatoka wapi," alihoji Rais Kikwete na mkurugenzi huyo alijibu kuwa anatoka wilaya ya Ngorongoro.
"Unasema unatoka Ngorongoro,"aliendelea Rais Kikwete na kuhoji: "Hapa umefikaje; umekuja kufanya nini na nani kakualika."
Baadaye aliwageukia wasaidizi wake na kuwauliza: "Huyu amekuja kufanya nini hapa; Nani kamwalika."
Akamgeukia tena Kayange na kumwambia: "Hatuwezi kukupa gari hii. Hii ni kashfa kubwa, nakumbuka vizuri msaada huu niliahidi kwa wananchi wa wilaya ya Longido wakati nilipofanya ziara kijiji cha Engalinaibo kipindi cha ukame ambako nilifika Kituo cha Afya wa Engalinaibo wakaniambia hawana gari la wagonjwa na nikawaahidi nitawaletea.
"Nakumbuka nilipofanya ziara wananchi wale waliniambia wanayo dispensary (Zahanati ) lakini, hawana gari la wagonjwa na sio nyinyi!. Hatukupi bwana, sio lako hatukupi." "Hatuwezi kukupa gari; watafuteni wanaopaswa kupewa gari hii; hii ni kashfa kubwa; document zote zimeandikwa kwa Kijiji cha Engalinaibo, iweje tuwape watu wa Ngorongoro."