Ikulu Yamwangukia Mkurugenzi aliyetimuliwa na Rais Kikwete | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ikulu Yamwangukia Mkurugenzi aliyetimuliwa na Rais Kikwete

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by GAMBLER, Jan 21, 2010.

 1. GAMBLER

  GAMBLER JF-Expert Member

  #1
  Jan 21, 2010
  Joined: Nov 22, 2009
  Messages: 303
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Na Exuper Kachenje
  Gazeti la Mwananchi


  IKULU jana ilitoa taarifa ya kumuomba radhi mkurugenzi wa wilaya ya Ngorongoro, Kayange Jacob baada ya Rais Kikwete kukataa kumkabidhi gari la wagonjwa na kuvunja hafla iliyoandaliwa kwa ajili ya kutoa msaada huo kwa halmashauri mbili.

  Katika tukio lisilo la kawaida lililotokea Ikulu siku tatu zilizopita, Rais Kikwete alimuhoji mtendaji huyo wa Ngorongoro sababu za kuonekana Ikulu siku hiyo na kuhoji aliyemualika kwenye hafla hiyo iliyolenga kukabidhi magari mawili ya wagonjwa kwa halmashauri za wilaya za Longido (Arusha) na Mbozi (Mbeya).

  Rais Kikwete alisema Ngorongoro haikuwa sehemu ya halmashauri ambazo zingegawiwa magari hiyo na akaamua kuondoka kwa hasira, akiacha hafla hiyo ikizimika ghafla.

  Baadaye jioni Ikulu ilitoa taarifa kuwa Rais Kikwete alimkabidhi gari mkurugenzi wa Halmashauri ya Mbozi, Levison Jeremiah Chilewa kwa ajili ya wakazi wa eneo la Kamsamba.

  Juzi, Katibu wa Rais Prosper Mbenna alikabidhi gari lililosalia la wagonjwa kwa mkurugenzi wa Halmashauri ta Longido, Christian Laiser katika hafla iliyofanyika Ikulu pia.

  Lakini jana, Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais ilitoa taarifa kwa vyombo vya habari ikimwomba radhi Kayange na kutoa ufafanuzi wa tukio hilo.

  "Tunachukua nafasi hii kuomba radhi kwa usumbufu uliompata Bwana Kayange Jacob na kwa jinsi tukio hilo lilivyomfanya aonekane kwa wananchi.

  Rais Kikwete anatambua haja ya vituo vya afya katika wilaya ya Ngongororo na wilaya nyingine nchini kupatiwa magari ya kubeba wagonjwa. Serikali inaendelea na juhudi za kununua magari hayo, na rais anaahidi kuwa katika mgao ujao na Wilaya ya Ngorongoro watafikiriwa," inasema taarifa hiyo.

  Taarifa hiyo inaongeza kusema: "Tunapenda kufafanua kuwa palifanyika makosa katika kupeleka taarifa kutoka Ikulu kwamba badala ya kumuita mkurugenzi wa Wilaya ya Longido kuja kuchukua gari la wilaya yake, akaitwa mkurugenzi wa Wilaya ya Ngorongoro.

  Makosa hayo yamerekebishwa, na jana, Januari 19, 2010 katibu wa rais, Ikulu, Bwana Prosper Mbena amekabidhiwa gari hilo kwa mkurugenzi wa Wilaya ya Longido, Bwana Christian Laizer."

  Sakata hilo limehusishwa zaidi na utendaji wa wasaidizi wa Rais Kikwete ambao wamekuwa wakilaumiwa kwa kumsabishia kiongozi huyo matatizo kadhaa kwenye kadamnasi, likiwemo tukio la hivi karibuni la kwenda kufungua hoteli ya kitalii ambayo kesho yake ilibomolewa na Tanroads kutokana na kujengwa ndani ya hifadhi ya barabara.

  Hata hivyo, taarifa hiyo ya Ikulu haijaeleza kama watendaji waliohusika na uzembe huo uliomsababishia usumbufu, kero na aibu mkurugenzi huyo wa Loliondo watachukuliwa hatua.

  Mbali na matukio hayo mawili, wasaidizi wa Kikwete wamehusishwa na uzembe wa kutomuandalia rais sehemu ya kukaa wakati alipoenda kwenye misa ya mazishi ya mbunge wa zamani wa Mbeya Vijijini, Richard Nyaulawa Novemba mwaka juzi.

  Wasaidizi hao walichukua kiti alichokuwa akitumia mchungaji, lakini Kikwete akakikataa na kwenda kukaa kwenye benchi pamoja na waombolezaji wengine.

  Oktoba mwaka huohuo, wasaidizi wake walishindwa kumuandalia gari mke wa rais wa zamani wa Madagascar, Marc Ravalomanana wakati alipowasili nchini kwa ziada fupi.

  Rais Kikwete alilazimika kuchelewa kuingia kwenye gari lake ili aelekeze wasaidizi wake jinsi ya kumpatia usafiri mke huyo wa rais mwenzake.

  Katika tukio jingine, Rais Kikwete alilazimika kubatilisha uteuzi Anatory Choya kuwa mkuu wa wilaya ya Biharamulo baada ya kubaini kuwa alikuwa na kesi ya tuhuma za rushwa. Hata hivyo, Kikwete alimteua tena Choya kuwa mkuu wa wilaya ya Mbulu baada ya mahakama kumsafisha.

  Katika sakata la juzi, Rais Kikwete alimuhoji Kayange maswali kadhaa ambayo yalionekana kumfedhehesha mkurugenzi huyo wa Ngorongoro.

  "Wewe bwana unatoka wapi," alihoji Rais Kikwete na mkurugenzi huyo alijibu kuwa anatoka wilaya ya Ngorongoro.

  "Unasema unatoka Ngorongoro,"aliendelea Rais Kikwete na kuhoji: "Hapa umefikaje; umekuja kufanya nini na nani kakualika."
  Baadaye aliwageukia wasaidizi wake na kuwauliza: "Huyu amekuja kufanya nini hapa; Nani kamwalika."

  Akamgeukia tena Kayange na kumwambia: "Hatuwezi kukupa gari hii. Hii ni kashfa kubwa, nakumbuka vizuri msaada huu niliahidi kwa wananchi wa wilaya ya Longido wakati nilipofanya ziara kijiji cha Engalinaibo kipindi cha ukame ambako nilifika Kituo cha Afya wa Engalinaibo wakaniambia hawana gari la wagonjwa na nikawaahidi nitawaletea.

  "Nakumbuka nilipofanya ziara wananchi wale waliniambia wanayo dispensary (Zahanati ) lakini, hawana gari la wagonjwa na sio nyinyi!. Hatukupi bwana, sio lako hatukupi." "Hatuwezi kukupa gari; watafuteni wanaopaswa kupewa gari hii; hii ni kashfa kubwa; document zote zimeandikwa kwa Kijiji cha Engalinaibo, iweje tuwape watu wa Ngorongoro."
   
 2. Mahai

  Mahai JF-Expert Member

  #2
  Jan 21, 2010
  Joined: Jan 14, 2010
  Messages: 351
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Huyo mwakilishi wa ngorongoro hana makosa yoyote maana asingeweza kwenda kwenye hafla IKULU bila kualikwa, nadhani JK instead of humiliating him infront of people angewahumiliate hao wafanyakazi wake waliochemsha. Ila nimefurahi wamemwomba msamaha.
   
 3. N

  Nanu JF-Expert Member

  #3
  Jan 21, 2010
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 1,224
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Nadhani Ikulu kuna tatizo kubwa la uwajibikaji na mpangilio wa kazi.
  Nadhani rais anahitaji watu wengine ambao wanajua kupanga na kuratibu mambo vizuri. Anahitaji kufanya hili sasa na siyo baadaye, otherwise atakuwa amechelewa sana na kitu kibaya zaidi kinaweza kutokea.
   
 4. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #4
  Jan 21, 2010
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...dah?!

  hii kweli "Ze Komedi" show.
   
 5. Kimey

  Kimey JF-Expert Member

  #5
  Jan 21, 2010
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 4,119
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Asee Bongo ni zaidi ya Uijuavyo!!
   
 6. Che Guevara

  Che Guevara JF-Expert Member

  #6
  Jan 21, 2010
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 1,178
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 145
  Ni style yake kudhalilisha watu ili kutafuta sifa. Cheap politics ndio zake. Poor him...
   
 7. O

  Omumura JF-Expert Member

  #7
  Jan 21, 2010
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  I cant imagine usumbufu alioupata huyo DED wa ngorongoro,haitoshi tu kumwomba radhi,wampe promotion pia!
   
 8. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #8
  Jan 21, 2010
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  And a few heads should be rolling at Ikulu right about now.
   
 9. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #9
  Jan 21, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,606
  Likes Received: 6,177
  Trophy Points: 280
  JKikwete is a child molester,nothing short of it.

  Wewe kimtu kimkurugenzi cha wilaya sijui, unakikaripia namna hiyo in public, hawa watu wengine wanamsikia rais maisha yao yote hawajawahi kumuona, siku wakimuona wengine ma bush star hawa wanakuwa na awe kubwa, halafu unamkaripia hivyo, mtu anaweza kufa kwa blood pressure wakati tatizo wala hajalisababisha yeye.

  Kuna mama mmoja alikuwa anafanya kazi Ikulu enzi za Nyerere, alikuwa ananihadithia siku moja akipuyanga kwenye corridors za Ikulu huku akisoma communique zao, akafika kwenye kona akapata a near miss ya kugongana na Nyerere uso kwa uso.Alitegemea labda rais angemfokea, mama aliogopa sana, Nyerere bila shaka aliona hilo, akaanza kumpoza na kumwambia hamna tabu, hamna kilichoharibika.

  Tukio hili labda unaweza kuona lisilo na maana sana, lakini linakuonyesha mtu mwenye class anavyoweza kuwa na empathy kwa watu walio chini yake, moja ya sifa moja kubwa ya kuwa mwanasiasa mzuri.Kikwete kashasahau kwamba na yeye alikuwa a lowly mtumishi wa mkoani huko, mpaka Mzee Warioba alipomtoa huko na kuja mumu introduce kwa Mwinyi.Kikwete kashasahau kwamba huyu mtu hakupanga kuja kuchukua hilo gari, ila amepangiwa, na kama kuna wa kulaumiwa basi ni watu wake wa Ikulu na huyo aliyempangia.

  Kwa kifupi tukio hili ni "tip of the iceberg" tu inayoonyesha ni jinsi gani nchi inavyoendeshwa kiholela.Kikwete anaendesha nchi vibaya zaidi ya monitor wa darasa la nne mwenye akili.
   
 10. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #10
  Jan 21, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  yani kumwomba msamaha aitoshi ata kidogo kwa fedhea walomtwisha ivi mpaka inatokea hivi ikulu kuna tatizo gani yani lazima kuna usanii ulotaka kufanyika akuna makosa yoyote yale usanii tuu hapo
   
 11. Mponjoli

  Mponjoli JF-Expert Member

  #11
  Jan 21, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 668
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Tatizo ikulu pamejaa waganga njaa wasio na vigezo. Kama kweli watu wanajua kazi yao haiwezekani rais anaenda kugawa gari kwa mtu mwingine.

  Huu ni ubabaishaji,rais ni mtu mkubwa sana, haitakiwi awe anapewa maandalizi ya ajabu ajabu tu
   
 12. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #12
  Jan 21, 2010
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,219
  Likes Received: 2,083
  Trophy Points: 280
  Braza,
  Shida ya ikulu sio moja, ni nyingi sana (multitude) kiasi kwamba inabidi JK awajibishe timu kubwa sana pale kwake. Yaani matikiti mabovu yote yamo shambani mwa JK (Ikulu). Ndio hawahawa wanaomtwisha raisi safari zisizo na mwisho hadi anazidiwa na kudondoka majukwaani. JK alikuwa na sababu ya kuwakasirikia ile siku, ila aiishie kukasirika tu, awashikishe adabu!
   
 13. Gembe

  Gembe JF-Expert Member

  #13
  Jan 21, 2010
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 2,505
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  Mkulu

  alijua amekosea sana kumfokea yule jamaa baadaye sana hivyo akaona ni bora kumuomba msamaha kupitia kina salva..

  ila alikosea,hii ni picha mbaya sana kwa kiongozi..!

  tatizo mambo ya uswahili ,kushushua watu ,tabia za viongozi wa kitz
   
 14. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #14
  Jan 21, 2010
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,219
  Likes Received: 2,083
  Trophy Points: 280
  Mkuu Gembe,
  Siku nyingi ulikuwa huonekani hyapa, ulijificha wapi bro?
  Happy new year
   
 15. Gembe

  Gembe JF-Expert Member

  #15
  Jan 21, 2010
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 2,505
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135

  Mkuu IDIMI,

  Happy new year to you

  Nipo naangalia jamvi kila mara sema natumia muda mwingi kuwasiliana na watu kwa PM,nchi inakwenda kubaya sana kwa sasa mpaka naogopa.

  watu wamekata tamaa..Hivi leo nikukuuliza ni nani unaona anafaaa kama Jk asipogombea?fikiria majedwali yale ya Mzee Wangu Mwanakijiji..lile jedwali lile..

  Wananchi wanalia,watawala hawajui wafanyaje,Zanzibar moto mkubwa umeanza kuchochowa..

  tatizo Mkulu hakutusikiliza toka mwanzoni..walitudharau sana na kujidai uswahili na usaniii utasaidia.Makamba hakuna kitu na sijui kwanini Muungwana alimpa kazi ambazo inamzidi uwezo!

  tutafika na mwaka 2010 ni mwaka wa mabadiliko!
   
 16. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #16
  Jan 21, 2010
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  JK hanan watu wote hawa alitoka nao kule kijiweni na hawezi kuwabadili maana wanasema anayo taka kuyasikia . Reaction yake kwa jamaa huyu ninaye mjua vyema mtu mstaarabu sana na mchapa kazi kudhalilishwa hivi ni mwaka 2010 uchaguzi ndiyo wanaamka kwa mbwe mbwe tena .
   
 17. J

  JokaKuu Platinum Member

  #17
  Jan 21, 2010
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,734
  Likes Received: 4,958
  Trophy Points: 280
  ..JK reaction was NOT presidetial at all.

  ..he had no right to treat Ngorongoro District Director the way he did.
   
 18. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #18
  Jan 21, 2010
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Je, hawa wakurugenzi wa wilaya si ndio wasimamizi wa chaguzi mbali mbali wilayani ? Kama ni hivyo, hebu fikiria shida wanayoipata mgombea wa upinzani anaposhinda kura, hofu yao ndiyo mwanzo wa matokeo kucheleweshwa. Kama hapa tu ameweza kudhalilishwa Kayange Jacob kwa kosa lisilo lake, je inakuwaje CCM inapobwagwa kwenye uchaguzi under his watch, si ndiyo itakuwa balaa. Halafu tunategemea siku moja uchaguzi kuendeshwa kwa kuzingatia sheria, haki na usawa !
  Pole sana Kayange Jacob, Mkurugenzi wa Wilaya ya Ngorongoro.
   
 19. b

  bitimkongwe JF-Expert Member

  #19
  Jan 21, 2010
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 3,034
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 160
  Kiranga - a child molester, nani hapo mtoto?

  Punguza chumvi kijana!
   
 20. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #20
  Jan 21, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,606
  Likes Received: 6,177
  Trophy Points: 280
  Gembe,

  Hapo Mzee Colin Powell anakwambia "You break it, you own it"

  Baada ya kosa la kwanza la kumfokea mtu kiajabu ajabu, Kikwete anafanya kosa lingine kwa kutomuomba radhi yeye mwenyewe personally na kuwatuma hawa watu wa Ikulu.

  Hata kama tuseme ni kweli hawa watu wa Ikulu ndio waliochemsha na Kikwete alikuwa justified, at the end of the day Mkulu wa kaya ya Ikulu ni Kikwete, angetakiwa kumuomba radhi huyu mkuu wa wilaya kwa makosa ya watu wake wa Ikulu.

  Lakini wapi, Kikwete hajaonyesha leadership, ameonyesha kujua kutupa lawama. na kibaya zaidi, hata kama anaona kuna mtu kachemsha Ikulu huwezi kusikia mtu kawajibishwa kamwe.

  Nchi inaendeshwa kama kijiwe cha mateja.
   
Loading...