Magazetini
JF-Expert Member
- Aug 16, 2014
- 593
- 1,712
Habari waungwana,
Kama tukumbukavyo, Rais John Magufuli karibuni alifanya uteuzi wa kamishna mkuu wa mamlaka ya kupambana na kuzuia madawa ya kulevya ukiambatana na uteuzi wa makamishna wawili wa kumsaidia, mmoja wa upelelezi na mwingine wa intelijensia.
Huku kukiwa na vita dhidi ya madawa ya kulevya inayoendelea jijini Dar es Salaam, teuzi hizi na atachokiongea Rais Magufuli leo zimevuta hisia za watu zikiambatana na mtazamo mchanganyiko juu ya hatua zinazochukuliwa ikiwa zinafaa ama hazifai.
Tujumuike pamoja mishale ya saa tano nikuhabarishe yanayojiri kutoka jumba jeupe.
===========
Rais Magufuli amemtaka Kamishna wa Mamlaka ya kuzuia na kupambana na dawa za kulevya, Rogers Sianga kufanya kazi bila kuogopa ili kuokoa nguvu kazi ya taifa inayoteketea.
Dar es Salaam
Rais John Magufuli amemwapisha Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kupambana na Kuzuia Dawa za Kulevya, Rogers Sianga na Kamishna Mkuu wa Uhamiaji, Anna Makakala Ikulu jijiji Dar es Salaam leo.

Amesema vita ya dawa za kulevya ni ngumu kwa sababu ina faida kubwa na wafanyabiashara hao wanaweza kufanya chochote kwa fedha zao.
"They can do anything at any cost (wanaweza kufanya lolote kwa gharama yoyote). Lazima tushirikiane katika vita hii,' amesema Rais Magufuli.
Pamoja na makamishna hao, Rais pia amewaapisha mabalozi watatu ambao ni Omary Yusuph Mzee (Algeria), Joseph Sokoine (Ubelgiji) na Grace Mgovani (Uganda).

=====*WAZIRI MKUU, MAWAZIRI KUONGOZA MAPAMBANO DAWA ZA KULEVYA*
[HASHTAG]#Rais[/HASHTAG] Magufuli:Wewe Waziri Mkuu sasa ndio mwenyekiti wa mapambano haya.Ingekuwa sheria haijasema ningekuwa Mwenyekiti mimi mwenyewe;
[HASHTAG]#Rais[/HASHTAG] Magufuli: Na nyie mawaziri sasa mkafanye kazi.Msiwe wanyonge.Kafanyeni kazi bila kumuonea mtu.Tumieni sheria namba ya mwaka 2015.