Ikulu: Rais hajaidhinisha posho za wabunge!

Status
Not open for further replies.
Mbona naona kama Jk anairudisha tena bunge liamue wakati bunge ndo lililopendekeza ongezeko la posho, wameona mambo magumu aati!
 
Can't click it anyway!! Mkuu wa nchi, mwingine kiongozi wa shughuli za serikali za kila siku!!
 
Hiyo ni danganya toto tu posho zenyewe washaanza kuzitafuna ndo wanatudanganya mpaka sasa hajaidhinisha pia ili kuwapumbaza madaktari wanaoendelea kugoma
 
Kwa hiyo Pinda na Makinda wamelidanganya Bunge na nchi kwa ujumla wake,wanapaswa kuwajibika kwa hili.
 
Katibu wa Bunge - posho hazijalipwa!

Spika - zimelipwa na zimeshaidhinishwa (na nani)?

Pinda - Rais amesafiri kwenda Davos ameniachia suala la posho kuwa nisaini au kutokusaini

Zitto - PInda hana mamlaka ya kusaini

Pinda na Spika - zimeshapitishwa na hela zipo tayari zimetayarishwa ili mlipwe

Wabunge - Applause!

Madaktari - mnajipendelea basi mgomo unaendelea

Wananchi - Tuandamane au tusiandamane?

Kurugenzi ya Ikulu - Rais hajasaini kamwe. Anataka wabunge watumie busara.

Kama mambo ya kusoma ramli vile.......
 
Mhhh haya yetu macho
maelezo zaidi ya kujichanganya maana Waziri wake Mkuu anasema yake na Spika anasema yake na huku wabunge washaanza kulipwa na wanazitaka kwa kila njia
Wanaopinga wanaonekana wasaliti
Sasa tuelewe lipi

We elewa tu wanatudanganya na kutupumbaza
 
Kakalende ni kwa serikali ipi hii hii ya kikwete au? Thubutu si wangekuwa wameisha mpaka sasa? Kwani ina maana wewe ndio unaziona sarakasi kama hizi kwa mara ya kwanza? Kikwete why dont you just step down? Unatudhalilisha sana matokeo yake tunaonekana watanzania wote ni wendawazimu sasa.
Hapa kuna mtu atapoteza kibarua chake!
 
Unapoona mihimili miwili ya utawala inatofautiana katika misimamo yao kwa kiasi hiki .....tena mara kwa mara(si mara moja).....basi ujue utawala huo una matatizo makubwa sana na lengo lake si kuwahudumia raia bali ulafi wa kujaza matumbo yao.....ieleweke tu kuwa hawa ikulu wasije kuhusisha mgomo na madaktari na ongezeko la posho za wabunge.....madaktari madai yao yako pale pale...despite the fiasco between bunge and ikulu......
 
Hii ni changamoto kwa waTZ hasa kwa madokta waliopo kwenye mgomo ni wakati sasa kwa wao kuangalia sehemu inayolipa kama kwenye siasa wapate nao kuhamia huko ili wapate maslahi makubwa kama haya
 
Nini source ya taarifa hii ya Invisible na ile ya gazeti la Mwananchi? Haiwezekani kuwa mojawapo ya taarifa hizi sio ya kweli? Kwa akili ya kawaida sioni ni vipi mkanganyiko kama huu unaweza kutokea (pamoja na utendaji mbovu wa serikali uliopo!).
 
Mbona naona kama Jk anairudisha tena bunge liamue wakati bunge ndo lililopendekeza ongezeko la posho, wameona mambo magumu aati!
ukiona ivo ujue rais hajakubali anawataka waendelee kiasi cha zamani.jk ni mzalendo sana
 
Ee Mungu tujalie maisha tuzidi kuona vituko.Mbona wabunge wamemshambulia Zitto aliposema anajua Rais hajasaini?

Iliwauma sana kwa nini Zitto ajue wakati wao hawajui. Pinda uoga unamsumbua, anawaogopa wabunge maana wakimbana atalia kwa hiyo inabidi aseme suala hilo limekubaliwa
 
Screw them! Hivi kuna vyama vingapi vinatawala Tanzania? Hivi waziri mkuu na rais wana matatizo ya mawasiliano?

Interesting and confusing. Rais, WM, Spika chama hicho hicho, serikali hiyo hiyo. Na leo hii wamemzotoa Zitto aliyesema kwamba Rais hajaidhinisha posho. Kwa hiyo Zitto anajua zaidi habari za ikulu kuliko WM na Spika. Pwechepweche!!
 
Katibu wa Bunge - posho hazijalipwa!

Spika - zimelipwa na zimeshaidhinishwa (na nani)?

Pinda - Rais amesafiri kwenda Davos ameniachia suala la posho kuwa nisaini au kutokusaini

Zitto - PInda hana mamlaka ya kusaini

Pinda na Spika - zimeshapitishwa na hela zipo tayari zimetayarishwa ili mlipwe

Wabunge - Applause!

Madaktari - mnajipendelea basi mgomo unaendelea

Wananchi - Tuandamane au tusiandamane?

Kurugenzi ya Ikulu - Rais hajasaini kamwe. Anataka wabunge watumie busara.

Kama mambo ya kusoma ramli vile.......

Dah umeniacha hoi mkuu, meno thelathini na nje yote mbili!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom