Ikulu: Rais hajaidhinisha posho za wabunge!

Ikulu: Rais hajaidhinisha posho za wabunge!

Status
Not open for further replies.
Lakini ni nani anaye zisaini na kuzipitisha?si ni yeye sasa wabunge wapime nini wakati wao walishatoa sababu zao na JK atoe vigezo vyake kama hakubaliani na hizo posho asilete longolongo Jk

wewe mbona kutuambii posho unayopokea kwa kumshambulia JK acha longolongo hapa Jf
 
Katibu wa Bunge - posho hazijalipwa!

Spika - zimelipwa na zimeshaidhinishwa (na nani)?

Pinda - Rais amesafiri kwenda Davos ameniachia suala la posho kuwa nisaini au kutokusaini

Zitto - PInda hana mamlaka ya kusaini

Pinda na Spika - zimeshapitishwa na hela zipo tayari zimetayarishwa ili mlipwe

Wabunge - Applause!

Madaktari - mnajipendelea basi mgomo unaendelea

Wananchi - Tuandamane au tusiandamane?

Kurugenzi ya Ikulu - Rais hajasaini kamwe. Anataka wabunge watumie busara.

Kama mambo ya kusoma ramli vile.......
kweli tanzania ni zaidi ya tuijuavyo.

Kukaa kimya kwa wananchi ni sawa na kujua kuwa nyoka kaingia ndani ya nyumba yako alafu unaamua kunyamaza. Kwa hakika mwenye nyumba (sisi Watanzania) tu viumbe wa ajabu hapa kwenye sayari ya dunia!

 
Screw them! Hivi kuna vyama vingapi vinatawala Tanzania? Hivi waziri mkuu na rais wana matatizo ya mawasiliano?
Haya tunayoyashuhudia katika nchi hii ni ombwe katika utawala wakati mihimili ya dola inapofanya kazi kwa kubahatisha kwa sababu dhana ya utawala kwa chama tawala CCM imepoteza dira.KWAO hivi sasa uongozi ni kwa manuafaa yao na familia zao na sio kuwatumikia wananchi uongozi kwa CCM NI DEAL.
 
Shibuda na Selasini ni wabunge wa CCM? Ni heri ya JK ambaye hajatoa jibu kuliko wabunge hao tunaowaita watetezi wa wanyonge kuomba kwa Rais kuongezewa posho.
 
Gazeti la Mwananchi la leo, Jumanne, Januari 31, 2012 limeandika habari zenye kichwa cha habari – JK abariki posho mpya za Wabunge: Kila mmoja kulipwa sh 330,000 kwa siku.

Habari hizi siyo za kweli na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais inataka kutoa ufafanuzi ufuatao:

Maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete kuhusu suala hili yako wazi kabisa na hakuna mahali ambako Rais Kikwete amebariki posho hizi.

Maelekezo ya Mheshimiwa Rais kuhusu suala hili ni kama ifuatavyo:

Kwanza, Mheshimiwa Rais Kikwete anakubali haja ya kuangalia upya posho kwa Wabunge lakini amewataka wabunge kutumia hekima na busara katika kulitafakari suala hili.

Pili, Mheshimiwa Rais Kikwete amewataka Wabunge kutumia Kikao cha sasa cha Bunge kulizungumza upya suala hilo.


Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
31 Januari, 2012

Maelezo ya ikulu yanadhibitishisha habari ya Mwananchi. Kwa haya maelezo rais anakubali ongezeko ila anataka "busara" itumike. Haya maneno ni ya kujiondoa kwenye lawama tu!
 
Juzi juzi Pinda alidai issue ya kusign posho amekabidhiwa yeye na Rais, mbona kwenye hicho kikao Pinda amedai Rais ndo ame sign hz posho, ina maana alinyang'anywa hy kazi??"Tanzania zaidi uijuavyo"
 
Haya tunayoyashuhudia katika nchi hii ni ombwe katika utawala wakati mihimili ya dola inapofanya kazi kwa kubahatisha kwa sababu dhana ya utawala kwa chama tawala CCM imepoteza dira.KWAO hivi sasa uongozi ni kwa manuafaa yao na familia zao na sio kuwatumikia wananchi uongozi kwa CCM NI DEAL.

Ombwe la kutengenezwa na gazeti la mwananchi? Hivyo kuwaacha Shibuda na Selasini wakibishana na mwenyekiti wao Mbowe kuhusu posho nalo ni ombwe la uongozi?
 
Ombwe la uongozi+viongoz vilaza+viongoz wabnafsi+unafk ndilo linaloitesa tz
 
wana JF hivi ukiacha gazeti la mwananchi lenye hiyo habari je kuna source nyingine yenye nukuu ya PM akizungumzia kwamba JK ameshasaini posho? isijekuwa ni wanatunga ili wapate updates
 
Tanzania ni kikundi cha binadamu waoishi pamoja katika kipande cha ardhi kwa kuviziana na kusikiliziana, matukio yakifasili maisha ya kila siku....
Sidhani kama hii ni tafsiri ya neno NCHI......
Hamna kitu hapa hakika!
 
Gazeti la Mwananchi la leo, Jumanne, Januari 31, 2012 limeandika habari zenye kichwa cha habari – JK abariki posho mpya za Wabunge: Kila mmoja kulipwa sh 330,000 kwa siku.

Habari hizi siyo za kweli na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais inataka kutoa ufafanuzi ufuatao:

Maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete kuhusu suala hili yako wazi kabisa na hakuna mahali ambako Rais Kikwete amebariki posho hizi.

Maelekezo ya Mheshimiwa Rais kuhusu suala hili ni kama ifuatavyo:

Kwanza, Mheshimiwa Rais Kikwete anakubali haja ya kuangalia upya posho kwa Wabunge lakini amewataka wabunge kutumia hekima na busara katika kulitafakari suala hili.

Pili, Mheshimiwa Rais Kikwete amewataka Wabunge kutumia Kikao cha sasa cha Bunge kulizungumza upya suala hilo.


Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
31 Januari, 2012
Hapo pekundu means PINDA NA MAKINDA hawana Busara wala Hekima, yaani ni washenzi mana wamefanya maamuzi kishenzishenzi. Hapo c ndipo pa kuwataka wajiuzuru kwa kulidanganya Taifa???Walafi na wabinafsi, Manyang'au hao
 
Pinda kweli aliongea bungeni kuwa Rais ameidhinisha malipo hayo? kama ni kweli aliongea bungeni na Kurugenzi ya Rais inasema huo ni uongo, Pinda anachukuliwa hatua gani?

Mambo ya namna hii yanatokea Tanzania tu. Tuna laana gani sisi jamani??
 
Screw them! Hivi kuna vyama vingapi vinatawala Tanzania? Hivi waziri mkuu na rais wana matatizo ya mawasiliano?

Kama JK mawasilin yake na pm wake yana kuwa magumu hivi sasa tutaamini vipi anapooogelea Teknohama ya kina "bill gates" anatambua kile anachoeleza
 
Gazeti la Mwananchi la leo, Jumanne, Januari 31, 2012 limeandika habari zenye kichwa cha habari – JK abariki posho mpya za Wabunge: Kila mmoja kulipwa sh 330,000 kwa siku.

Habari hizi siyo za kweli na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais inataka kutoa ufafanuzi ufuatao:

Maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete kuhusu suala hili yako wazi kabisa na hakuna mahali ambako Rais Kikwete amebariki posho hizi.

Maelekezo ya Mheshimiwa Rais kuhusu suala hili ni kama ifuatavyo:

Kwanza, Mheshimiwa Rais Kikwete anakubali haja ya kuangalia upya posho kwa Wabunge lakini amewataka wabunge kutumia hekima na busara katika kulitafakari suala hili.

Pili, Mheshimiwa Rais Kikwete amewataka Wabunge kutumia Kikao cha sasa cha Bunge kulizungumza upya suala hilo.


Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
31 Januari, 2012
Wakuu, haya mawili yaliyowekwa hapo juu kama maelekezo ya rais yanatoa nafasi kubwa sana ya hicho walichofanya Wabunge na hata kusema kuwa maamuzi yao yana baraka, hayaonyeshi kukataa, na hili ndilo tatizo la viongozi wetu, hawatoi majibu ya ndiyo ama hapana wanaogopa kupoteza umaarufu na pia kupata nafasi ya kujitetea pale linaapolipuka. La maana naona sisi tuchukulie waamekubaliana katika hili!
 
kama hii taarifa ni ya kweli, then some one must go, kuiogopa chadema to this degree kumewafanya wawe na kauli za kukurupuka mno, khaa. na ndo wanazidi kuharibu jamani.

Yaani hii serikali, kama macomedians!
 
Huu ni Ushindi kwa Zitto Kabwe kwa kuwa aliwaambia ukweli kuhusu posho kutosainiwa wakabishi na kumzomea sasa hivi wanazomewa wao. wabunge wote waliozomea Hovyoooooooooooo!!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom