Ikulu: Rais hajaidhinisha posho za wabunge!

Ikulu: Rais hajaidhinisha posho za wabunge!

Status
Not open for further replies.
Screw them! Hivi kuna vyama vingapi vinatawala Tanzania? Hivi waziri mkuu na rais wana matatizo ya mawasiliano?

Nimejiuliza kitu hicho hicho lakini nimeshindwa kuelewa. Lakini swali gumu zaidi je Watanzania tutaendelea mpaka lini kuwa wapumbavu na wakimya tukiacha wachache tuliowapa dhamana ya kutuongoza wakaendelea kuwa 'busy' kuhudumia matumbo yao na kuridhia matakwa yao bila kujali Watanzania wanaoathirika.?
 
Mheshimiwa Rais Kikwete anakubali haja ya kuangalia upya posho kwa Wabunge lakini amewataka wabunge kutumia hekima na busara katika kulitafakari suala hili.

Tuanzie hapo kwenye blue: Rais anakubali posho kwa wabunge ziongezwe au la? simple yes or no.
Wabunge wameshangalia upya posho zao na wakaja na figure 200,000 extra! Na ili waweze kulipwa ni lazima (kwa taratibu za sasa) rais atie sign.

Uongozi maana yake lazima ufanye maamuzi na uwe tayari kutetea maamuzi yako hata kama wengi watakasirika. Sasa ame-sign au haja-sign? Kama haja-sign kwa nini? Na kama ame-sign kwa nini? Hizi open-ended statement hazitoi mwongozo hata kidogo sana sana zinaonena dalili ya kukwepa kufanya maamuzi.
 
Hii nchi inamatatizo gani?Au ni laana?Na kama ni laana,ni ya nani?
 
badala ya kutolea kauli la madaktari kugoma hili wamejibu haraka...hii ndio TZ ya JK

Madaktari hawana umuhimu wala faida katika nchi hii, posho za Wabunge ni kwa maslahi ya Taifa.
 
Well hapo sasa ndio tunajua nchi hii watu wapo makini kiasi gani kuokoa ngozi zao wenyewe lakini matokeo yake ni kama wanajikaanga kwa mafuta yao wenyewe.

Sasa hiyo taarifa ya Ikulu mbona inalenga zaidi kumuaibisha Rais na Utawala wake mbovu. Kweli watu wanatoa taarifa kama hiyo na kusema kwamba ni taarifa toka ofisi muhimu kuliko zote nchini? Ina maana hakuna mawasiliano kati ya Waziri Mkuu na Rais na Spika wa bunge? Ikiwa ni hivyo tunaelekea wapi kama nchi?

Dah inauma sana hii. Kuzaliwa Mtanzania sio laana ni baraka sasa kwa nini tuwaache wachache wachezee baraka tulizopewa na mwenyezi Mungu katika hii nchi yake?

Mkuu kuna makala fulani Jonhson Mbwambo alisema nchi ipo kwenye auto pilot tusubiri pilot arudi kitini na dis-engage hiyo auto pilot!
 
Screw them! Hivi kuna vyama vingapi vinatawala Tanzania? Hivi waziri mkuu na rais wana matatizo ya mawasiliano?

JK anamdharau sana pinda maana hana fikira timamu anaropopka ropoka tu..na huko ikulu ndo kama kwenye mchiriku..kila mtu na lake ...agghhhh..yaani mara mia ofisi ya katibu kata ina systems and utaratibu mwanana wa kuwasiliana lakini sio ikulu hasa ya kipindi hiki cha JK
 
Posho Tanzania ni muhimu kuliko ustawi wa maisha ya watu! Kama idiot yupo magogoni kwanini na taahira asiongoze hii nchi ya wadanganyika?
 
Sasa nakiri kwamba Tz imevamiwa na watu tusiowajua,inakuwaje Mh.Pinda anatoa taarifa zisizo na hakika na akiwa msaidizi wa karibu mno wa Mkuu wa nchi? Inakuwaje Mh.Makinda anatoa taarifa za uwongo na anatizamwa tu? Sasa ndg Pinda utuachie ofisi yetu na mama Makinda hutufai kwa kuwa hayo ni machache uliyotudanganya tumejua je ni mangapi unatudanganya na hatujui!?Maana za mwizi arobaini.CCm wamefilisika ndugu zangu!
 
1. Ikulu DOUBLE STANDRDS,
2. Kikwete DOUBLE STANDARDS,
3. Mizengo Pinda DOUBLE STARDARDS,

4. Wabunge DOUBLE STARDARDS,
5. Spika DOUBLE STANDARDS,
6. Hata nao baadhi ya Wabunge Vijana nao DOUBLE STANDARDS

7. Magazeti (Mwananchi)DOUBLE STANDARDS
8. Madai ya Governor kubana matumizi kurekebisha uchumi wetu (Posho-Mshahara kwa wabunge na Ukumbi Ikulu) DOUBLE STANDARDS

9. Mpango wa Serikali yetu kuhamia Dodoma huku wakizidi kuwekeza Dar es Salaam DOUBLE STANDARDS

... hivi ni nani atakayetuondolea kero hizi nchini; inauma viwango vya UNAFIKI tulikofikia na kwa mtindo huu nchi haitokaa iendelee ng'o - kazi ni kutafuna kila kitu kilichopo tu kana kwamba tumeamua kuwakomoa vizazi vijazo nchi hii!!!!!!!!!!!
 
Raisi aongee tumskie anapinga usishangae badae akisema mimi sikuwaagiza kurugenzi ya mawasiliano bada ya kusikia mziki wa wabunge mbona nilisha saini toka mwaka jana
 
Invisible et al

please, utaratibu wa mafao na malipo ya posho kwa wabunge ukoje? and which organ (who) has an authority to approve or dis-approve
 
Hivi kwa nini asiseme tu kuwa hakubaliani nalo hilo jambo?

Halafu yeye malipo yake ni shi'ngapi?

Si ndo hapo! Yaani anasema wabunge watumie busara,kwani yeye hawezi kutumia busara katika kukataa madai hayo ya wabunge?

Yaani busara zake zimemtuma kusema kwamba wabunge walijadili ilo suala bungeni? Yaani hana busara za kugundua kwamba wabunge hawawezi kujinyonga wenyewe katika ili? Ni sawa na mteja aingie dukani afu muuza duka ampe nafasi mteja huyo katika kupanga bei kitu mteja huyo anachokitaka!
 
Mi nadhani raisi nae ana hekima pia. So kwa nini ategemee ya wabunge asitumie ya kwake?
 
Hapa kuna mtu atapoteza kibarua chake!

Hakuna atakayepoteza kibarua. Wamezoea kukorogana! Hukumbuki ya Magufuli Vs Pinda Vs Kikwete! Yote heri! Duh! Mungu atupe nini tena! Hii Nchi na Viongozi wake BURE Kabisa! Nipeni fimbo!
 
Grrrrrriiii....to hell with them. Hivi hawa jamaa wanafikiri wananchi wanawafikiria vipi?
 
Kwa hiyo huu ni another ujinga ujinga?? Pinda kadanganya Bunge na Watanzania wote? Kwa hiyo Pinda Kasema Uongo?? Yaani Waziri Mkuu Anasema Uongo??? Yaani Waziri Mkuu Kadanganya?? Wabunge mnasemaje?

Waziri Mkuu amewadanganya eti, kwahiyo Kiongozi wa shgughuri za Serikali anasema uongo Bungeni?? Kama si mkweli, wabunge mnasemaje??

Ninyi wabunge wa kipindi hiki cha 2010-15, yaani mtakuja kupigwa mawe na kuchinjiwa baharini. Endeleeni kuwa kama mazezeta, tanzania ya leo 2012, siyo itakayo kuwa ya 2015. Zitapigwa kavukavu, kwa lugha ya watoto wa kijiweni.
 
Hivi nani anajua yeye huyo raisi analipwa mshahara kiasi gani na marupurupu yake ni kiasi gani na nani huwa anaamua kuyaongeza au kuyapunguza?

Au nyie wenzangu hamjali na wala hamna shauku wala sababu ya kutaka kujua compensation yake?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom