Ikulu: Rais hajaidhinisha posho za wabunge!

Status
Not open for further replies.
Hii inaonyesha Raisi, hajaweka wazi msimamo wake juu ya posho anapima joto la wananchi hapa. Lakini, Pinda wala Makinda hawana makosa maana waliambiwa watumie busara zao. Ndio hizo zimetumika sasa. Pinda na mchezo wa dolidoli - nimeachiwa maagizo nisaini ama nisisaini! kombolera likafika kwa wenyewe - ndio wawaa imeitika!
 
wameanza kujikana ee!!hadanganywi mtu hapa.ina maana wabunge watakataa posho?tunasubiri tuone.

Unaona haya kuomba radhi? jaribu kuwa muungwa kwani tumemtukana sana JK kwenye thread ya mwanzo. kudaka taarifa za udaki/mtaani na kusambaza kwa wananchi pasipo kufuatilia ukweli ni hatari kwa afya ya taifa letu kuna siku itatuletea vita.
 
Kweli nchi haitawaliki. Dr wa ukweli ebu tamka neo basi ili kutengua lile tamko baba. Naamini wamejuta sasa. Hawatachakachua tena kura.
 
MY GUDNESS! What it seems ni kua JK hamuelewi PINDA, na PINDA nae hamuelewi JK.....Basi ni vulugu tupo...kila mtu ana double standards zake.....yetu masikio na huu mwaka tutashuhudia mengi
 
Mhhh haya yetu macho
maelezo zaidi ya kujichanganya maana Waziri wake Mkuu anasema yake na Spika anasema yake na huku wabunge washaanza kulipwa na wanazitaka kwa kila njia
Wanaopinga wanaonekana wasaliti
Sasa tuelewe lipi

Umeambiwa waziri mkuu na makinda hawajasema hayo dodoma wewe vipi? kuwa upinzani ndio sababu ya kulazimisha udaku kuwa taarifa ya kweli. mwananchi halipati coverage namna wameamua kuokoteza
 
Nimesoma gazeti limedokezwa kwamba Spika na PM wamethibitisha habari za kuridhiwa kwa posho; unakuwaje hapa sasa?
 
Interesting and confusing. Rais, WM, Spika chama hicho hicho, serikali hiyo hiyo. Na leo hii wamemzotoa Zitto aliyesema kwamba Rais hajaidhinisha posho. Kwa hiyo Zitto anajua zaidi habari za ikulu kuliko WM na Spika. Pwechepweche!!

Inashangaza! Sasa Raisi si aseme na taifa sasa! maana mambo mawili nyeti haya!
 
kama hii taarifa ni ya kweli, then some one must go, kuiogopa chadema to this degree kumewafanya wawe na kauli za kukurupuka mno, khaa. na ndo wanazidi kuharibu jamani.
 
inaonyesha Kikwete hataki kabisa kupewa lawana ya hizi posho. hataki kusaini ila anashindwa kuongea ama anaangaliia upepo kwanza.


kumbuka bunge ni muhimili tofauti Jk kafanya vizuri kuwaambia wapime uzito wa ombi la nyongeza ya posho kisha waona kama ni sawa kufanya hivyo kwa sasa. Wao wabunge walikuwa wanamjaribu Rais na yeye kaamua kuwajaribu kama wana akili nzuri au hamnazo wote
 
Ni aibu pia kwa Jf tunapenda sana kujadili porojo

Lazima tujadili hata kama ni porojo kwa nini JK anakuwa kimya anamsukumizia mwenzio asiyekuwa na maamuzi yeye si alisema Pinda ndio alishughulikie? Tatizo la JK ni kigeugeu ni raisi mnafiki kwa wananchi wake hataki kuonekana kama yeye ndiye aliamua anamsakizia Pinda
 
Nilisema siku nyingi kuna jambo Kikwete anatengeneza taratibu Anna makinda na pinda wanaonekana wapumbavu na kituko mbele ya jamiii.Inakuwa mbunge wa chama cha upinzani anajua habari za Ikulu kuliko waziri mkuu na spika ???????.
 
Katibu wa Bunge - posho hazijalipwa!
Spika - zimelipwa na zimeshaidhinishwa (na nani)?
Pinda - Rais amesafiri kwenda Davos ameniachia suala la posho kuwa nisaini au kutokusaini
Zitto - PInda hana mamlaka ya kusaini
Pinda na Spika - zimeshapitishwa na hela zipo tayari zimetayarishwa ili mlipwe
Wabunge - Applause!
Madaktari - mnajipendelea basi mgomo unaendelea
Wananchi - Tuandamane au tusiandamane?
Kurugenzi ya Ikulu - Rais hajasaini kamwe. Anataka wabunge watumie busara.
Kama mambo ya kusoma ramli vile.......


Mkuu hili pia ni sakata la aina yeke hapa nchini. Kumekuwa na kugongana kwa kauli kwa muda sasa. Haijilikani nani anasema ukweli. Si waketi pamoja watuambie ukweli ni upi au wanakimbiana?
 
kumbuka bunge ni muhimili tofauti Jk kafanya vizuri kuwaambia wapime uzito wa ombi la nyongeza ya posho kisha waona kama ni sawa kufanya hivyo kwa sasa. Wao wabunge walikuwa wanamjaribu Rais na yeye kaamua kuwajaribu kama wana akili nzuri au hamnazo wote

Lakini ni nani anaye zisaini na kuzipitisha?si ni yeye sasa wabunge wapime nini wakati wao walishatoa sababu zao na JK atoe vigezo vyake kama hakubaliani na hizo posho asilete longolongo Jk
 
Screw them! Hivi kuna vyama vingapi vinatawala Tanzania? Hivi waziri mkuu na rais wana matatizo ya mawasiliano?

Wanataka kuleta whats called cheap politics. w.mkuu hawezi kutoa tamko afu wasikilizie watu rais abadili. u can fool us no more.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom