Ikulu haikujiandaa na ziara ya Rais wa China

Ikulu haikujiandaa na ziara ya Rais wa China

emalau

JF-Expert Member
Joined
Apr 25, 2009
Posts
2,775
Reaction score
3,109
Wadau jana nilifuatilia dhifa ya kitaifa iliyofanyika ilkulu kwa ajili ya Rais wa China, nilichoshangaa ni kwamba Rais wa China Xi Jinping aliongea kwa lugha yake ya nyumbani - kichina, ilipofika zamu ya Rais wetu aliongea kwa kutumia kiingereza, je alifanya hivyo kwa sababu gani?

Nina imani nchi hii ina watu wengi wanaoweza kutafsiri kichina pia lakini sikuona kama kulikuwa na maadalizi yoyote ya kuwapa wageni headphone ili wapate tafsiri kwa muda muafaka.

Wakuu kwa ujumla tumetia aibu mbele ya wageni achilia mbali Raisi kutoona glass yake ya maji !!

Au mnasemaje wakuu.
 
Hatuna mkurugenzi wa itifaki kwa sasa...aliyekuwepo alitaka "kukwiba peke yake" wenziye wakamporomosha kwa kutaka kuwanyima kamhogo....dhifa ya jana itakuwa iliandaliwa na housemaid wa ikulu....

mtoa mada sijui anawaza nini utazani alitanguliza miguu wakati anazaliwa fafanua aina ya aibu iliyojitokeza,tatizo lako mawazo ya kitumwa na uzandiki yanakutesa toa hoja za kujenga taifa wewe ungekuwa mke wangu ningekuacha leoleo
 
kwanza ningekuwa ni mimi ningepiga kiswahili tu;mbona yeye kapiga kichina.ah,nimesahau,kumbe bado tunatawaliwa na waingereza.am sorry.
 
Mkuu jitahidi kuwa na Tasfida kidogo hoja inajibiwa kwa hoja siyo rungu na kama kuna ushauri unatoa siyo kumtusi mtu.
 
kwanza ningekuwa ni mimi ningepiga kiswahili tu;mbona yeye kapiga kichina.ah,nimesahau,kumbe bado tunatawaliwa na waingereza.am sorry.

Au labda huyu Rais katoka HONG KONG........:A S 39::A S 39::A S 39::A S 39:
 
Aisee tena ilitakiwa iongelewe kichina kabisa badala ya kiingereza maana Rais huyu anashukuriwa kwa Mengi!!! Vinginevyo leo hii kungekuwa na historia nyingine kabisa kati ya nchi hizi mbili!!! Ile sheria ya madawa ya kulevya China nataka iletwe Tanzania ili wakikamwatwa pande zote mbili iwe hakuna majadiliano!! Khaaaaa!!
 
nilifuatilia dhifa kwa makini, wakati mkuu ya kaya kamalizia kumkaribisha Mwenyeji wake tayari kwa toss kwa ajiri ya dhifa - nilimsikia JK akaongea kwa kiswahili tena kwa mshangao "sasa iko wapi glass yangu" ni kama walisahau kuweka.

overall sikupenda sisi tuongee kingereza wakati wananchi 80% hawaijui lugha hii kwa ufasaha.
 
Mleta mada anataka kuimaliza siku kwa umbea tu tumpotezeeni, twendeleeni na mada zenye mshiko.
haina mashiko wakati mmetusainisha mikataba 17, ndani yake hatujui mmeandika nini, msije kuwa mmeshatuweka rehani sisi wenyewe.
 
Au labda huyu Rais katoka HONG KONG........:A S 39::A S 39::A S 39::A S 39:[/QUOTE

Naungana na wanaodhani ilikua muhimu Mh. Rais alitakiwa azungumze kiswahili..........hii ingekua njia moja wapo ya kuitangaza na kuikuza lugha yetu hii. Ni aibu kuona wazungu wakiithamini lugha yetu huku sisi wenyewe tukiwa hatuoni thamani yake. Mfano; Kiswahili ilikua moja ya lugha kuu TANO zilizochaguliwa na kutumika wakati wa kusimikwa kwa Papa Francis wiki iliyopita, hii inaonyesha jinsi gani kiswahili kinavyokubalika. Kwa hiyo ni dhahili kua haingii akilini JK kutotumia kiswahili ilihali mgeni wake alitumia kichina bila hata wasiwasi. Ifikie hatua tujiamni na kilichochetu kwani tutaweza kuthaminiwa na kuheshimika.
 
Mleta mada anataka kuimaliza siku kwa umbea tu tumpotezeeni, twendeleeni na mada zenye mshiko.
mh, mi sisemi lolote. wasije kusema kuwa hata haka kagirl ni kajukuu! hhd.jpg
 
Au labda huyu Rais katoka HONG KONG........:A S 39::A S 39::A S 39::A S 39:[/QUOTE

Naungana na wanaodhani ilikua muhimu Mh. Rais alitakiwa azungumze kiswahili..........hii ingekua njia moja wapo ya kuitangaza na kuikuza lugha yetu hii. Ni aibu kuona wazungu wakiithamini lugha yetu huku sisi wenyewe tukiwa hatuoni thamani yake. Mfano; Kiswahili ilikua moja ya lugha kuu TANO zilizochaguliwa na kutumika wakati wa kusimikwa kwa Papa Francis wiki iliyopita, hii inaonyesha jinsi gani kiswahili kinavyokubalika. Kwa hiyo ni dhahili kua haingii akilini JK kutotumia kiswahili ilihali mgeni wake alitumia kichina bila hata wasiwasi. Ifikie hatua tujiamni na kilichochetu kwani tutaweza kuthaminiwa na kuheshimika.

Ninakubaliana nawe kabisa. Mojawapo ya MATATIZO ya msingi ambayo yametukwamisha ni kukosa moyo wa kujiamini. Na hili linaanzia kutoka katika mitaala (kama ipo, ama iliyoandikwa au inayofikirika) yetu ya elimu. Wenzetu walioendelea ni kuanzia jinsi wanavyofundisha chekechea na nini wanachokifundisha hadi vyuo vikuu hali ya kujiamini imefunganishwa katika mfumo na mitaala ya elimu - ikiwa ni pamoja na masuala kama hayo ya matumizi ya lugha, nk. Huu mfumo wa kwet utaona kuwa ni dhahiri kuanzia viongozi wa juu hata wawe na elimu ya juu hadi wa chini hawana moyo wa kujiamini - ukiachilia shughuli za ufisadi ambazo hizo hakuna anayewashinda.
 
Katika wote nimempenda Membe, hivi kwa nini hakuchagua karia ya moddeling?
Alipoenda kusaini mara ya kwanza baada ya kukabidhiana akapose for the cameras, anakuja shtuka mchina kwshaenda kukaa anapisha wengine waje kusaini, akakimbia haraka.

Nilibaki na mshangao sana.

Anawaza ku-pose tu
 
Afu wakti wa kutost Raisi: Glass yangu iko wapi?? Jamani, ikulu kuna movie za kufa mtu inavyoelekea.
Imevamiwa, imevamiwa
 
Au labda huyu Rais katoka HONG KONG........:A S 39::A S 39::A S 39::A S 39:[/QUOTE

Naungana na wanaodhani ilikua muhimu Mh. Rais alitakiwa azungumze kiswahili..........hii ingekua njia moja wapo ya kuitangaza na kuikuza lugha yetu hii. Ni aibu kuona wazungu wakiithamini lugha yetu huku sisi wenyewe tukiwa hatuoni thamani yake. Mfano; Kiswahili ilikua moja ya lugha kuu TANO zilizochaguliwa na kutumika wakati wa kusimikwa kwa Papa Francis wiki iliyopita, hii inaonyesha jinsi gani kiswahili kinavyokubalika. Kwa hiyo ni dhahili kua haingii akilini JK kutotumia kiswahili ilihali mgeni wake alitumia kichina bila hata wasiwasi. Ifikie hatua tujiamni na kilichochetu kwani tutaweza kuthaminiwa na kuheshimika.

Anyway sijajua takwimu za watanzania wenye uwezo wa kuelewa lugha ya kiingereza(spoken english language) ni wangapi lkn kwa jana hata leo mh Jk hotuba yake angeitoa kwa kiswahili angekuwa ameienzi lugha ya nchi yake na pia ungekuwa mfano wa uzalendo pia kwa wananchi ambao walikuwa wanamtazama bila kuielewa lugha iliyotumika.Daah wenzetu wanaenzi lugha yao sana.
 
Back
Top Bottom