Ikulu haijampa onyo Bw Reginal Mengi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ikulu haijampa onyo Bw Reginal Mengi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Zak Malang, Jun 8, 2009.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Jun 8, 2009
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  [SIZE="3"]Ikulu haijampa onyo Bw Reginal Mengi

  • Haitoi matamko kupitia kwmye simu za mkononi
  • Ikitoa tamko huita vyombo mbali mbali vya habari
  • Taarifa katika ‘Tanzania Daima’ si tamko halali
  • Mwandishi alikurupuka bila kufuata utaratibu
  • Yeye wala si Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Ikulu

  Taarifa zilizotolewa


  Na Mwandishi Wetu, SEMA USIKIKE

  Juni 8, 2009

  TAARIFA zilizotolewa na mwandishi wa habari katika kitengo cha Mawasiliano Ikulu, Premy Kibanga, kuwa Ikulu imemuonya Mengi, si tamko la Ikulu bali ni mawazo yake mwenyewem SEMA Usikike limegundua.

  Kwa mujibu wa vyanzo vyetu vya habari kutoka ndani ya kitengo hicho, zimesema kuwa kwa kawaida Ikulu ikitoa matamko huita vyombo vya habari vyote na kutoa taarifa zake kwa kufuata utaratibu uliowekwa jambo ambalo mwandishi huyu hakulifuata.

  Vyanzo vyetu pia vimebainisha kuwa taarifa zilizoandikwa katika gazeti la ‘Tanzania Daima’ zikimnukuu mwandishi wa Ikulu Premy Kibanga zinadaiwa kuwa hilo si tamko la Ikulu.

  Katika sehemu ya tamko ambalo mwandishi huyo, Premy Kibanga alisema limetolewa na iIkulu linasema kuwa Bw Mengi ametakiwa aviheshimu vyombo vya dola na kwamba Ikulu imekanusha madai ya Mengi kuwa anaandamwa na baadhi ya viongozi wa kiserikali pamoja na taasisi zake.

  Watu waliohojiwa na gazeti hili wanasema kama kweli mwandishi huyo aliongea na gazeti hilo, alifanya kosa kubwa ambalo halijawahi kufanywa na mwandishi yeyote wa kawaida aliyewahi kufanya kazi katika kitengo huicho cha mawasiliano.

  Wamesema kuwa tokea enzi za Mwalimu, hakuna tamko la Ikulu lililowahi kutolewa kwa simu na kwa chombo kimoja kama ilivyotokea sasa, tena chombo binafsi. Kwa mfano, walisema, katika enzi za awamu ya kwanza, msemaji wa Ikulu alikuwa ni Katibu Mkuu Kiongozi Timothy Apiyo ambaye alitumia utaratibu wa kutoa taarifa kwa vyombo vya habari vyote ama kutoa tamko kupitia Idara ya Habari Maelezo ambayo ilikuwa ikisambaza habari hizi kwa wahariri wakuu.

  Utaratibu ambao Rais wa awamu ya pili, Mzee Ruksa aliutumia kwa kumteua Balozi Patrick Chokala kuwa msemaji wa Ikulu, waandishi walikuwa wanaitwa pale Ikulu na kuongea na Chokala, kuuliza maswali kisha kurudi kuandika habari. Hata siku moja mtu huwezi kutoa tamko la Ikulu kupitia chombo kimoja cha habari tena si cha serikali. Tena mtu hyo akiwa siyo msemaji wa Rais.

  Katika utawala wa awamu ya tatu, kama kawaida utaratibu wa kutoa matamko ya ofisi ya Rais ulifuatwa pia. Mheshimiwa Benjamin Mkapa naye akamteua Geoffrey Nkurlu naye akawa anatoa taarifa kwa vyombo vyote ya habari, na si kutoa tamko kupitia simu ya mkononi tena kwa jambo nyeti kama alivyofanya mwandishi huyu Premy Kibanga…………….

  ……..Habari kamili Ukurasa wa pili katika SEMA Usikike la leo
  [/SIZE]
   
 2. K

  Kyachakiche JF-Expert Member

  #2
  Jun 8, 2009
  Joined: Feb 16, 2009
  Messages: 911
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 45
  Huyu REGNAL Mengi ni yupi?
   
 3. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #3
  Jun 8, 2009
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Kumekucha! Niliposoma habari za TD nilijua tu kuna mkono wa akina RA. Aidha pia nani asiyejua mhariri wake, Absolom Kibanda kwamba alishanunuliwa na hao mafisadi? Lakini hayo yote tisa, kumi ni nani asiyejua kwamba awamu hii ya nne ni ya kishikaji tu?

  Huyu PK nani asiyejua mahusiano yake na mkuu wa kaya? Hata kama alikosea kwa kutofuata utaratibu, mkuu huyo wa kaya hawezi kufanya chochote kwa sababu zilizo wazi kabisa. Hana moral authority ya ku-take action.

  Nchi hii inatawaliwa na mafisadi na leo tunasoma kuwa wameanzisha civil war kule north. Ndiyo, ni civil war -- kwani huko nchi nyingine hizi vita huanzaje? Si hivi hivi tu, kwa kiasi kikubwa zikisukumwa na ufisadi uliokithiri?
   
 4. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #4
  Jun 8, 2009
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  "Huyu REGNAL Mengi ni yupi?"
  ___________________

  KYACHAKICHE:
  Kunradhi kwa hiyo typo error. It's supposeed to be REGINALD.
   
 5. Mchaga

  Mchaga JF-Expert Member

  #5
  Jun 8, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 1,371
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Full si hasa...
   
 6. Superman

  Superman JF-Expert Member

  #6
  Jun 8, 2009
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 5,702
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 145
  Ipo kazi!
   
 7. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #7
  Jun 8, 2009
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,795
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  ...Naona ni yale yale tu!! Hata habari hii pia ilipaswa kutolewa na Ikulu kama Taarifa Rasmi na sio kupitia vyanzo vya kuaminika vya Sema Usikike!!! Taarifa hii inaonekana kumpinga Premmy kwa ambacho yenyewe inafanya!! Tunataka taarifa rasmi kutoka Ikulu zaidi ya hivyo habari kuanzia ilikoanzia hadi sasa ni UDAKU tu!
   
 8. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #8
  Jun 8, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Mkuchika alisoma hiyo habari???
   
 9. Sophist

  Sophist JF-Expert Member

  #9
  Jun 8, 2009
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 3,087
  Likes Received: 1,733
  Trophy Points: 280
  ....samahani Baba watoto....
  Sawa lakini siyo uharibu kazi...., ...watoto watakula nini?
  Karagabaho
   
 10. J

  Jafar JF-Expert Member

  #10
  Jun 8, 2009
  Joined: Nov 3, 2006
  Messages: 1,138
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  .........you can fool some people sometimes, but you cant fool all the people all the time.
   
 11. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #11
  Jun 8, 2009
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  "Kumekucha! Niliposoma habari za TD nilijua tu kuna mkono wa akina RA. Aidha pia nani asiyejua mhariri wake, Absolom Kibanda kwamba alishanunuliwa na hao mafisadi? Lakini hayo yote tisa, kumi ni nani asiyejua kwamba awamu hii ya nne ni ya kishikaji tu?

  Huyu PK nani asiyejua mahusiano yake na mkuu wa kaya? Hata kama alikosea kwa kutofuata utaratibu, mkuu huyo wa kaya hawezi kufanya chochote kwa sababu zilizo wazi kabisa. Hana moral authority ya ku-take action.

  Nchi hii inatawaliwa na mafisadi na leo tunasoma kuwa wameanzisha civil war kule north. Ndiyo, ni civil war -- kwani huko nchi nyingine hizi vita huanzaje? Si hivi hivi tu, kwa kiasi kikubwa zikisukumwa na ufisadi uliokithiri?|
  ________________________

  COUNTERPUNCH:

  Umenena ndugu yangu. Ikulu hii ya wamau ya Nne ni uchafu mtupu kwani wanaoiendesha ni watu wengine, siyo huyo aliyeshinda kwa kishindo. Tumeshaona "kushinda kwa kishindo" ni kwamba waliiba kwa kishindo na kufanya kampeni haramu kwa kishindo kujinyakulia ushindi kwa mtu wao kwa kishindo na baadaye kumvua madaraka. Kabakia pale sanamu tu ya kuchonga.

  Hebu fikiri -- huyu mwanamke mwandishi anadiriki kutoa statement kwa niaba ya Ikulu kuhusu issue inayotokana na ufisadi? Tumefika hapo?

  Kwa mpango huu tutafika mahali ambapo hata mtunza bustani wa Ikulu anaweza kupigiwa simu na Kibanda na kutaka atoe statement ya kumkandamiza mtu fulani -- hasa iwapo huyo mtu ni kero kubwa kwa mafisadi. Na huyo Kibanda ataandika gazetini kuwa ni statement ya Ikulu! Na Mkuu wa Ikulu kimya!!!!!! kaufyata kwa woga!

  Tunakwenda pabaya ndugu zangu, heshima inapotea nchi hii, utaratibu unaoheshimika wa nyumba takatifu ya Magogoni unapotea, haki inapotea, maadili yanapotea na nakubaliana nawe Counterpunch kuwa civil war haiko mbali.

  Mungu apishie mbali -- God Bless us!
   
 12. K

  Kilamia Member

  #12
  Jun 8, 2009
  Joined: Jul 9, 2008
  Messages: 62
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Naunga mkono hoja. Inashangaza taarifa ya ajabu ya Ikulu inapingwa na taarifa ya ajabu ya Sema Usikike. Imefika mahali tukumbuke kuwa Ikulu ni Mahali `Patakatifu,' na sio pa kuchezewa chezewa. Kwa kuanzia Ikulu wakanushe taarifa inayomtaja Premmy kwa kuwa hatutegemei shutuma nzito kwa serikali na vyombo vyake zijibiwe kwa mahojiano na gazeti, tena kwa njia ya simu. Hatua nyingine zifuate baadaye.
   
 13. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #13
  Jun 8, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,849
  Likes Received: 83,275
  Trophy Points: 280
  Ni ukweli mtupu hayo yote uliyoyaandika. Maana mafisadi wanataka kuonyesha kwamba CHADEMA ni chama cha kikabila na kabila lenyewe ni la Wachagga kumbe ni UZUSHI MTUPU na UWONGO WA HALI JUU. Hizi ni dalili za kufilisika kisiasa kwa chama cha mafisadi.
   
 14. M

  MzeePunch JF-Expert Member

  #14
  Jun 8, 2009
  Joined: Jun 8, 2009
  Messages: 1,412
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Duh inatisha! Kumbe hata Tanzania Daima limeshatwaliwa na mafisadi! Huyo Kibanda mbona alionekana kuwa mpiganaji mzuri siku za nyuma. Kulikoni? Kweli ufisadi ni janga la taifa.
  Kuhusu huyo mwanadada wa Ikulu, kwanza nashangaa alipataje hiyo kazi. Namfahamu kwama mwanamke asiye na adabu kabisa. Kwani ina maana hakuna vetting siku hizi ili watu wenye sifa zinazofaa tu ndio wafanye kazi kwenye hiyo ofisi nyeti? Kwa kweli sielewi kabisa nini kinaendelea hapa nchini. Unaweza kukuta huyo alitumwa na mtu kama RA atoe hiyo taarifa huku akijua kwamba boss wake hawezi kusema lolote. Ni aibu gani hii jamani. Hivi kweli karne hii tunaweza kuwa na ubabaishaji wa namna hii kwenye ofisi kuu ya nchi?
   
 15. Kilasara

  Kilasara JF-Expert Member

  #15
  Jun 8, 2009
  Joined: Dec 21, 2008
  Messages: 578
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Kyacha Kiche (kilukooye!). Kama haijampa onyo si uthibitisho kuwa inathibitisha mapapa wapo?
   
 16. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #16
  Jun 8, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Wameshindwa hata kupata tamko rasmi kuhusu tamko hili ilnalosemwa kuwa si msimamo rasmi wa ikulu, kitu kinachonifanya nitie shaka kuhusu hii article kwamba ikulu haikutoa tamko kumpinga Mengi, inaonekana article yao ina attack msemaji wa ikulu kusema mambo rejareja bila kufuata official channels za ikulu.

  Udhaifu wa hii criticism ni ukweli kwamba hata hii article nayo haijajiwekea uzito wa kuwa na official stand ya ikulu kutoka official channels.

  Wameshindwa kumuuliza Salva au official yeyote mwenye mamlaka ya kusema kwa niaba ya ikulu in the proper way?

  Bila ya official statement kutoka ikulu watakuwa wanafanya kile kile wanachokikataza, kuchukua vihabari habari na kuviunganisha halafu kudai kwamba ikulu imesema.
   
 17. M

  Magezi JF-Expert Member

  #17
  Jun 8, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Na ninyi wana JF munaongea mambo mengi mno na sioni hata mtu mmoja anatuelekeza tummalize vipi rostam aziz na wenzake? mbona mnazunguka mbuyu? kwani kweli anatushinda? je ni risasi ngapi zina mtosha? Kwa sababu hata tembo ukilenga vizuri ni risasi moja tu! Kwa nini huyu mburushi tumzungumze miaka na miaka? ni nani yeye hapa tanzania? Naomba maelekezo?
   
 18. t

  tk JF-Expert Member

  #18
  Jun 9, 2009
  Joined: Feb 7, 2009
  Messages: 270
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kwani kupigana vita dhidi ya ufisadi ni lazima Mengi apate support ya JK au Ikulu? Kama sivyo basi magazeti yake yana wasiwasi gani kama Ikulu inamuunga mkono au la? Why cant you guys read between the lines?? Hivi ukiangalia trend ya mambo, ni kweli serikali inamuunga mkono Mengi kuhusu vita dhidi ya ufisadi? Nauliza haya maana inaonyesha waandishi wengi wanajaribu kujipa moyo kuwa taarifa za kibanga si sahihi na serikali inamuunga mkono Mengi.
   
 19. j

  jokimbo New Member

  #19
  Jun 9, 2009
  Joined: Jun 8, 2009
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tasisi nyeti kama Ikulu ni lazima iwe na utaratibu wa kuendesha shughuli zake kwa uwazi.Haiingi akilini kwa anayejiita mwandushi wa habari wa Ikulu kutoa taarifa kwa chomo kimoja binasi tena kwa njia ya simu ya mkononi
   
 20. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #20
  Jun 9, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  that was kind my initial take; lakini nilipoisoma tena na ile ya Tanzania Daima nadhani wanataka official statement ya serikali. Kwamba serikali itachukua upande wa Tanzania Daima (walimuonya Mengi) au upande wa gazeti hilo (hawakumuonya Mengi). Kitu ambacho sidhani kama kitachukuliwa kwani ni kama catch-22
   
Loading...