Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akutana na kuzungumza na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Freeman Mbowe Ikulu Mkoani Dar Es Salaam.
Rais Samia amesisitiza kuwa kuna umuhimu wa kushirikiana ili kuijenga Tanzania kwa kuaminiana na kuheshimiana kwa misingi ya haki.
Mhe. Mbowe amemshukuru Rais Samia kwa kuonesha kwake kujali huku akikubali kuwa msingi mkubwa wa kujenga taila la Tanzania ni kusimama katika haki.
Vile vile, amesema wamekubaliana kufanya siasa za kistaarabu na kiungwana na kuwa yuko tayari kushirikiana na Serikali katika kuleta maendeleo ili nao pia waweze kutekeleza majukumu yao ipasavyo.
Picha Mbalimbali zikimuonesha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na kuzungumza na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe alipowasili Ikulu Jijini Dar Es salaam leo tarehe 04 March 2022
View attachment 2139037View attachment 2139038View attachment 2139039View attachment 2139058