IKULU, DAR: Rais Magufuli afanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Kampuni ya Barrick Prof. John L. Thornton

Hahahahahaaa imewauma Sana sijui wewe Na prof Palamagamba Kabudi nani anayejua Kiingereza.
Kama Acacia walitoa tamko sasa amekuja boss wake Katubu nyie endeleeni kupiga Kelele
Mkuu ametubu kwenye hiyo clip au ndani?
 
Sasa ni dhahiri upinzani wa Tanzania ni wa hovyo, ramli zao zote ni kuwa Raisi magufuli na Tume wakosee kiasi Barrick na kundi lake waende mahakamani halafi washinde kesi nchi ilipe fidia.

Pamoja na yote maoni ya viongozi na wafuasi wa Chadema hawajafurahishwa, mwanzo walisema tutashitakiwa, baadaye wakasema takwimu ni za uongo, sasa wanasema Barrick hawatalipa nini ajenda yao?
Barrick hawawezi kwenda mahakamani maana hawaoni wanasheria gani wa kuhonga kwenye timu itakayoundwa na serikali ya jpm. siku zote kwenye mashauri ya kimataifa kama nchi haki inakua upande wetu ila ile kitu mnyonge mnyongeni haki yake mpeni kwenye ulimwengu wa kibepari hakuna. wanasheria na timu yetu kama haikununuliwa itajiuza.
 
hebu kuwa na Adabu wewe hivi unaijua Barrick wewe au unaisikia??? Bajeti yetu kwa mwaka huu tilion30 kwa taarifa yako wale wana uwezo wa kugharamia bajeti ya nchi hii kwa miaka20 ndo wanafilisika
Hahahhahahhh trilion 100??? Wakiwalipa ndio ntaamini mko serious hivi unajia mana ya trilion 100??? Hap shareholders watakupa hasara kiasi gani????
 
Ndo kuna zuzu mmoja nilikuwa nabishana nae hapa kumbe wala hafahamu kwamba hadi kesho Acacia wanaendelea na shughuli zao kama kawaida na kilichosimamishwa ni issue ya makinikia peke yake!!!!
Na makanikia ni kama maganda ya ndizi na dhahabu ndio ndizi zenyewe. Yeye hana shida na ndizi(dhahabu) ila maganda tu(maganda)! Bila kukubaliana na wapinzani pamoja na wananchi wanaowalaumu ccm kukubali kupitisha sheria mbaya za madini na gesi na ikiwezekana kuomba radhi kwa kuwa alikuwa mmoja wa walioshiriki kuuza madini ataendelea kusemwa vibaya na kuonekana ni mnafki.
 
Vyoyvote vile lkn Muzungu mwenyewe amekuja kutufuta kinyume na huyo takataka wenu alivyokuwa anataka tufanye tumsujudie Muzungu, fvck chadema!

Aina ya wachambuzi wa Mikataba kama itaachiwa kwa watu kama wewe Mzungu ataachaje kutu fvck?
 
Hao wazungu wamekubali ki laini km wananawa vile? Cjui kwa watz lkn kimataifa mcfanye watu majuha
 
Wataalamu wa mitandao tutafutieni profile ya huyu ndugu profesa kama kweli yupo kundini kule Canada au ndio changa la macho! mzungu anayekubali kirahisi rahisi kwamba alikuwa anafanya biashara kiujanja ujanja bila kujari wala kuogopa ku tarnish image yake na kampuni achilia mbali kushitakiwa kimataifa?!
 
Lisu alikuwa anajpigia debe ili kesi zitakapokwenda mahakamani ndo awe wakili wa kutetea wanyonyaji,mnaomsujudia Lisu ndo mjue alivyo na tabia za kinyonga
 
Hamueleweki lipi mnasimamia!
Baada ya kumpigia magoti Fisadi
Mmekosa muelekeo
Mnacho kipinga na kukikubari hakijulikani
Mpo mpo tu
Sina haja ya kukuelimisha kila siku maana ya upinzani na nni tunachosimamia..... ila kwa leo mnakera kwa upotoshaji ssa wapi wamesema watalipa deni la trilion 100???
 
hebu kuwa na Adabu wewe hivi unaijua Barrick wewe au unaisikia??? Bajeti yetu kwa mwaka huu tilion30 kwa taarifa yako wale wana uwezo wa kugharamia bajeti ya nchi hii kwa miaka20 ndo wanafilisika
Pole sana kama hicho ndicho unachokiamini!!!
 
Vyoyvote vile lkn Muzungu mwenyewe amekuja kutufuta kinyume na huyo takataka wenu alivyokuwa anataka tufanye tumsujudie Muzungu, fvck chadema!
Jamaa hawana hata ubinadam Havana halafu ndo wanataka dola, labda ya kilwa kivinje.....wapuuuzi sana
 
Alichotuambia JPM na alivyotranslate kwa MZUNGU wa watu ni vitu viwili tofauti.kama nimemuelewa mzungu wa watu ni kwamba tutafika sehemu tukubaliane katika hali ya kuridhishana.taarifa ya magogoni inachumvi nyingi sana ukiisoma utafkiri jamaa kuna kosa wamekili ukweli ni kwmba hakuna sehemu wakili kunakosa wamefanya.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Kampuni ya Barrick Gold Corporation ambayo ni mmiliki mkubwa wa kampuni ya Acacia Mining Limited Prof. John L. Thornton na kukubaliana kuwa kampuni hiyo ipo tayari kufanya mazungumzo na Serikali ya Tanzania ili kulipa fedha ambazo Tanzania imezipoteza kutokana na kampuni hiyo kuendesha shughuli zake hapa nchini.

Prof. John L. Thornton ambaye amesafiri kwa ndege binafsi kutoka nchini Canada hadi Tanzania amekutana na Mhe. Rais Magufuli leo Juni 14, 2017 Ikulu Jijini Dar es Salaam na mazungumzo yao yamehudhuriwa na Balozi wa Canada hapa nchini Mhe. Ian Myles na Waziri wa Sheria na Katiba Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi.

Baada ya Mazungumzo hayo Prof. John L. Thornton amesema kampuni yake ipo tayari kufanya mazungumzo na Tanzania yatakayozingatia maslahi ya pande zote mbili na pia ipo tayari kulipa fedha zote ambazo inapaswa kulipa kwa Tanzania.

Kwa upande wake Mhe. Rais Magufuli amesema Serikali inakaribisha mazungumzo hayo na itaunda jopo la wataalamu watakaofanya majadiliano na kampuni ya Barrick Gold Corporation ili kufikia makubaliano ya kulipwa fedha zinazodaiwa na namna kampuni hiyo itakavyoendesha shughuli zake nchini maslahi ya pande zote mbili.

Mhe. Rais Magufuli amesema pamoja na kukubali kulipa fedha zinazodaiwa Prof. John L. Thornton amekubali kushirikiana na Tanzania kujenga mtambo wa kuchenjulia dhahabu (smelter) hapa nchini.

Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amevionya vyombo vya habari vinavyowataja Marais wastaafu Mhe. Benjamin William Mkapa na Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete na kuwahusisha na taarifa za kamati mbili za uchunguzi wa madini yaliyo katika makontena yenye mchanga wa madini (Makinikia) ambao ripoti zimekabidhiwa kwake na kamati hizo.

“Nimesoma ripoti zote mbili hakuna mahali ambapo Mzee Mkapa na Mzee Kikwete wametajwa, vyombo vya habari viache kuwachafua hawa wazee, wamefanya kazi kubwa ya kulitumikia Taifa letu, viwaache wapumzike” amesema Mhe. Rais Magufuli.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
14 Juni, 2017


mbwembwe zote hizo hatuendi kuwashtaki mahakamani.
 
Lisu alikuwa anajpigia debe ili kesi zitakapokwenda mahakamani ndo awe wakili wa kutetea wanyonyaji,mnaomsujudia Lisu ndo mjue alivyo na tabia za kinyonga
Katetea wapi na lini??? Mtu anayeteta wezi angeshauri muunde sheria za kuwabana??? Mbona hta CAG mstaafu ameshauri hicho icho?? Mbona usoro kashauri hiko hiko why lisu
 
Back
Top Bottom