Mkuu hebu vuta pumzi kwanza ............................... then tulia tena kusoma nilichoandika! punguza munkari!Sababu hizi ndiyo zinakufanya usiunge mkono move ya Rais katika hili?
Kweli hayo ni maswali ya kijinga kama ulivyo sema wewe mwenyewe.
Tatizo tangu Mwanzo umeshindwa kumuunga mkono Rais, wewe na wenzako hamjulikani mnataka nini hasa.
Look, amekuja Mwenyekiti wa ACACIA ambayo sisi hatuna hata mkataba nae sisi tuna mikataba na makampuni yake.
Amekuja kutaka kujua tatizo na kushirikiana kulitatua. Sasa ulitaka Rais amkamate na kufunga?
Hivi, watangazaji wa ITV wakikosea, Mengi akaenda Ikulu kujadili na kuona namna ya kulimaliza, unamkamata Mengi na kumuweka ndani? Au pale Mtwara kiwanda cha Dangote kikakwepa kodi, Dangote akaja kujua ukweli na nini na kujadili namna ya kulipa, unamkamata Dangote na kumuweka ndani?
Haters mnajiaibisha sana ktk hili. Hakika mmekosa uzalendo na heshma kwa nchi yetu
Endelea kuchukiaHahahahahhaha kwahyo watalipa trilion 100?? Hii nchi bwana alafu sio tena 4% ya trilion 100??? Afu mnashabikia
Na deal la kujenga smelter...bwana mkubwa tumemshtukia, anataka parcantage yake ndo apige kimya
Usiwaite wajinga, waite wehu.ccm na uvcc wanajitekenya na kucheka wenyewe mnapaka vinyesi na kuitana mashujaa wajinga kabisa
Hahahahahaaa imewauma Sana sijui wewe Na prof Palamagamba Kabudi nani anayejua Kiingereza.Sijui kama wanadanganya makusudi au ni kwamba hatujui Kiingereza cha huyo Mkanada.
HAKUNA mahala BARICK wanasema wanakubali deni, wanatubu, watalipa.
Jamani, wenzetu hawa wanatumia vichwa vyao kufikiri na kuongea. Hawafiki mwezini kwa vichwa vya panzi. Hawajitamkii tu maneno ovyo ovyo.
CEO wa ACCACIA hawezi kutamka, tena kwa maandishi, kupinga na kukemea ripoti ya Tume halafu mwingine aje nyuma yake aseme wanakiri, wanatubu, watalipa. Haiwezekani!
Yaani wewe ndio bure kabisa, hivi Watanzania akili zetu tumeweka wapi?Wakilipa mbona raha, hatutakuwa na sababu ya kulalamika sasa, kila kitu ulaya ulaya, trilion 300 si mchezo
Trillion mia inatoka wapi mkuu????? Mnapata 4% ya mrahaba pekee sasa kma 4% ni 100 trilion in maana ACACIA wanafaida ya trilion 1000?????? Kutoka kwenye makinikia pekee???Per yr almost sisi tunatumia 20 trillions.. Achsna na budget inayopitishwa bungeni sijui 31 trillions tshs. In actual, sense and real numbers roughly inatumika around 20 trillions kwa mwaka..
Sasa wakilipa 100 trillions of tshs.. Sio miaka 5 ya budget? Think it.. Sbb kamati imepata denied halisi ni 108 trillions of tshs tokea 1998 hadi March 2017.. So unafikiri mahesabu yatakuwa tofauti sana kamati? Subiri uone nakuapia utaona
Lumumba are very hopeless, mtu wamashakana kuwa zile ripoti ni uongo, leo eti atalipa. Mzungu katika clip yake hakuna aliposema atalipa! Hawezi kujikomit kijinga namna hivyo za kijinga kama hizo!Barrick wameomba mazungumzo so as wanaweza kupewa report zote mbili wakazitumie mahakamani kama ushahidi. Mark my words.
Maana previously waliomba wakanyimwa.
hizi sio press conference za ufipa, mambo makubwa haya lazima twende kwa procedure
Mkuu huyu bwana alishasema hatafukua makaburi. Kwa hiyo tusitegemee hata hao mawaziri kama kuna lolote watafanywa. Habari ndio imekwisha hivyo.Anashangaza sana huyu! Kwanini anaukimbia ukweli! Hata kuwajadili mafisadi Mkapa na Kikwete waliotufikisha hapa tulipo hataki! Ni sheria ipi inayotuzuia Watanzania kuwajadili hawa mafisadi wawili!? Kweli dikteta uchwara katika ubora wake!
hebu kuwa na Adabu wewe hivi unaijua Barrick wewe au unaisikia??? Bajeti yetu kwa mwaka huu tilion30 kwa taarifa yako wale wana uwezo wa kugharamia bajeti ya nchi hii kwa miaka20 ndo wanafilisikaNI mwehu tu ndie anaweza kuamini kwamba Barrick wamekubali kulipa matrioni yote yale!!! Hao Acacia wenyewe hata wakisema wauze mali zao zote bado hawana ubavu wa kupata angalau Trillion 100!!
Usiwe na haraka.
Win win situation umeipata? Hapo kuna mchezo unataka kuchezeka.Bado hatujavuka mto na tuzizodoane
Wanaiba sana tena ACACIA ni majizi mno hilo nakubali napongeza pia juhudi za kudai madini yetu 100% ingawa ningependa zaisi tubane dhahabu na mrahaba kuliko makinikia pekeeKwa hiyo unakubali dhahabu wanaiba kama kawa? kwanini huheshimu watu wenye data? unaweza kutoa ushahidi wa wizi wa dhahabu? Kama wewe ambaye hujafika mgodini unaamini wanaiba je wale walioenda kufanya utafiti? Dogo unajichanganya sana, badilika usiwe kama Tundu.
Barua imeshasema Mwenyekiti na Rais wamekutana kwa mazungumzo na kwamba Acacia wapo tayari kulipa fedha ambazo Tanzania imezipoteza kutokana na kampuni kampuni hiyo kuendesha shughuli zake hapa nchini!!!Hakuna kiasi kilichotajwa, hapo ni mawasiliano yatafanyika kwanza. Sasa wewe kwa akili yako, unataka nini? Ndoto yako ya usiku ni IPI?
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Kampuni ya Barrick Gold Corporation ambayo ni mmiliki mkubwa wa kampuni ya Acacia Mining Limited Prof. John L. Thornton na kukubaliana kuwa kampuni hiyo ipo tayari kufanya mazungumzo na Serikali ya Tanzania ili kulipa fedha ambazo Tanzania imezipoteza kutokana na kampuni hiyo kuendesha shughuli zake hapa nchini.
Baada ya Mazungumzo hayo Prof. John L. Thornton amesema kampuni yake ipo tayari kufanya mazungumzo na Tanzania yatakayozingatia maslahi ya pande zote mbili na pia ipo tayari kulipa fedha zote ambazo inapaswa kulipa kwa Tanzania.
Kwa upande wake Mhe. Rais Magufuli amesema Serikali inakaribisha mazungumzo hayo na itaunda jopo la wataalamu watakaofanya majadiliano na kampuni ya Barrick Gold Corporation ili kufikia makubaliano ya kulipwa fedha zinazodaiwa na namna kampuni hiyo itakavyoendesha shughuli zake nchini maslahi ya pande zote mbili.
wapumzike” amesema Mhe. Rais Magufuli.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
14 Juni, 2017