IKULU, DAR: Rais Magufuli afanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Kampuni ya Barrick Prof. John L. Thornton

Hapo kwenye wao kuleta watu wao
Na sisi kuleta watu wetu afu tuongee na watakachokubaliana ndio kitakachofanyika na watakachokubaliana kulipa ndio watalipa
Cha kwanza kabisa itakuwa ni kufanya mapitio ya ripoti afu kwenda kufanya sampling upya
Majibu ya sanpling yatashusha hizo hela
Namwisho wa siku mshindi atakuwa ni Acacia
Aminini hili
Unaota unapigwa miti ww...amia huko kwa wazungu wakutikite vizuri
 
Alichotuambia JPM na alivyotranslate kwa MZUNGU wa watu ni vitu viwili tofauti.kama nimemuelewa mzungu wa watu ni kwamba tutafika sehemu tukubaliane katika hali ya kuridhishana.taarifa ya magogoni inachumvi nyingi sana ukiisoma utafkiri jamaa kuna kosa wamekili ukweli ni kwmba hakuna sehemu wakili kunakosa wamefanya.
Alaa, Jpm aongea naye ana kwa ana tatizo lako nn
 
yote heri kama hiyo pesa italipwa kweli, na makubaliano yote yatakayofanyika yawekwe wazi kwa wananchi na ikiwezekana yawe mubashara tushuhudie kila kitu.

otherwise usaniii.
 
hebu kuwa na Adabu wewe hivi unaijua Barrick wewe au unaisikia??? Bajeti yetu kwa mwaka huu tilion30 kwa taarifa yako wale wana uwezo wa kugharamia bajeti ya nchi hii kwa miaka20 ndo wanafilisika
Inaonesha haijui wala hakuwahi kuisikia b4.
 
Kwani ile report inasema hasara ni kiasi gani? Uwe unabisha wakati unataarifa kamili
Ndio trilion 100 ila hawakusema ndio mrahaba wetu wote yaani 100 ndio 4% ambayo ndio stahiki yetu??? Acheni upotoshaji yaani wao trilion mia wametuibia maana wamekula wenyewe hawajatoa kodi na trilion 4 ya mrahaba wetu ssa wapi usoro alisema trilion 100 ni yetu??
 
Mlipokuwa mkisema TANZANIA INAKUWA ZIMBABWE VIPI!?
Toeni unafiki wenu
Mnalaana siyo bure
The Best option mliyokuwa nayo ku avoid kuwa Zimbabwe ni kulamba matapishi yenu! And that is what you have done! Negotiating with thieves? Naanza kuona waliotajwa kwenye reports za kina Ossoro walking free bila kushughulikiwa!
 
kumbe lugha ya malkia ni sheeda kweli kweli na hasa linapokuja suala zima la 'interpretation'
CEO wa Barrick kaongea short & clear, shida sasa kwenye tafsili....ohooo amekubali, ohooo ametubu,....ohoo amepiga magoti,.. ohooo Amelia .... suburi sasa hiyoo win -win situation muonee kama watu hawajajikojolea!
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Kampuni ya Barrick Gold Corporation ambayo ni mmiliki mkubwa wa kampuni ya Acacia Mining Limited Prof. John L. Thornton na kukubaliana kuwa kampuni hiyo ipo tayari kufanya mazungumzo na Serikali ya Tanzania ili kulipa fedha ambazo Tanzania imezipoteza kutokana na kampuni hiyo kuendesha shughuli zake hapa nchini.

Prof. John L. Thornton ambaye amesafiri kwa ndege binafsi kutoka nchini Canada hadi Tanzania amekutana na Mhe. Rais Magufuli leo Juni 14, 2017 Ikulu Jijini Dar es Salaam na mazungumzo yao yamehudhuriwa na Balozi wa Canada hapa nchini Mhe. Ian Myles na Waziri wa Sheria na Katiba Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi.

Baada ya Mazungumzo hayo Prof. John L. Thornton amesema kampuni yake ipo tayari kufanya mazungumzo na Tanzania yatakayozingatia maslahi ya pande zote mbili na pia ipo tayari kulipa fedha zote ambazo inapaswa kulipa kwa Tanzania.

Kwa upande wake Mhe. Rais Magufuli amesema Serikali inakaribisha mazungumzo hayo na itaunda jopo la wataalamu watakaofanya majadiliano na kampuni ya Barrick Gold Corporation ili kufikia makubaliano ya kulipwa fedha zinazodaiwa na namna kampuni hiyo itakavyoendesha shughuli zake nchini maslahi ya pande zote mbili.

Mhe. Rais Magufuli amesema pamoja na kukubali kulipa fedha zinazodaiwa Prof. John L. Thornton amekubali kushirikiana na Tanzania kujenga mtambo wa kuchenjulia dhahabu (smelter) hapa nchini.

Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amevionya vyombo vya habari vinavyowataja Marais wastaafu Mhe. Benjamin William Mkapa na Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete na kuwahusisha na taarifa za kamati mbili za uchunguzi wa madini yaliyo katika makontena yenye mchanga wa madini (Makinikia) ambao ripoti zimekabidhiwa kwake na kamati hizo.

“Nimesoma ripoti zote mbili hakuna mahali ambapo Mzee Mkapa na Mzee Kikwete wametajwa, vyombo vya habari viache kuwachafua hawa wazee, wamefanya kazi kubwa ya kulitumikia Taifa letu, viwaache wapumzike” amesema Mhe. Rais Magufuli.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
14 Juni, 2017

usanii na ujanja wa Kiccm kamwe hautasaidia nchiii nahisi harufu ya kupigwa bao na wawekezaji mapemaa.

hata wao watatoa press release kwa shareholders wao tutalinganisha na hii ya Baba Jesca.

mnaoshangilia sasa jua kuwa mambo bado ni magumu
 
Naona Raisi kaamua kuwakingia kifua Mkapa na Kikwete ameona bora yaishe maana siri zingeendelea kutoka.
 
Back
Top Bottom