Ikulu blog ni aibu tupu

Joseph

JF-Expert Member
Aug 3, 2007
3,518
1,086
Leo niliamua kupitia blog ya Ikulu na kukutana na kukutana na mshangao,yaani hakuna updates zozote tangu tarehe 14 May 2013?Hivi hawa watu walioajiriwa na Ikulu kufanya kazi hii wanafanya kazi gani?Tunaposema Serikali haipo makini tunakuwa hatukosei na mifano ndio hii tunayoiona kila siku.Huu ni udhaifu wa hali ya juu.
 
Huko ikulu blog unatafuta nini mkuu?

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Hiyo ndio tz yetu,wt hawajui wajibu wao tena siku hizi yaani kila kitu ni mpaka mtu asukumwe,tunahitaji mabadiliko makubwa sana kwenye nchi hii yenye asali na maziwa
 
Wapo bize na kula bata kwa kwenda mbele!! Ishu ya Mtwara haiwahusu!?
Nimeshangaa sana kuona wameshindwa hata kuweka picha za vurugu za Mtwara,hivi huyu anayelipwa kwa kazi hii anafahamika?
 
udhaifu umeanzia kwa raisi wao hawa wa chini yake unategemea nini?
Mkuu kill umesema kweli ila angalia utashitakiwa kwa kumtukana Rais,wengine wakisikia neno dhaifu ni tusi
 
Leo niliamua kupitia blog ya Ikulu na kukutana na kukutana na mshangao,yaani hakuna updates zozote tangu tarehe 14 May 2013?Hivi hawa watu walioajiriwa na Ikulu kufanya kazi hii wanafanya kazi gani?Tunaposema Serikali haipo makini tunakuwa hatukosei na mifano ndio hii tunayoiona kila siku.Huu ni udhaifu wa hali ya juu.


Wapi link?
 


Asante sana Mkuu kwa link. Ukosefu wa umakini ambao wadau wanaoulalamikia nimeuona pia. Ni aibu kubwa kuweka jina kubwa la Taasisi ya State House halafu unapost vitu bila proof reading. It's a shame....

[Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisisitiza jambo wakati akifungua Mkutano wa kuzungumzia Mustakabali wa maendeleo ya Wakulima Barani Afrika uliofanyika katika hoteli ya White Sands jijini Dar es Salaam leo.mkutano huo umeandaliwa na asasi ya(The southern African Confederation of Agriculktural Unions(SACAU).Wapili kushoto ni Kaimu Rais wa SACAU Bwana Ishmael Sunga na Watatu kushoto ni Waziri wa Kilimo Christopher Chiza.]

Chunguza vizuri red na blu hapo. Linaweza likaonekana dogo lakini linakuwa zito linapotokea Ikulu. Ikifanya kazi na watu makini hiyo Agriculktural inatosha kabisa kuotesha kibarua majani.
 
Back
Top Bottom