Ikiwa wafadhili watagundua CAG alionewa, basi tusali

TumainiEl

JF-Expert Member
Jan 13, 2010
6,184
11,201
Naipenda Serikali na Rais wangu ila napenda zaidi Serikali yangu kufuata Katiba ili kuepuka mambo ya Zimbabwe nchi iliokuwa na uchumi mzuri leo uchumi umeparaganyika.

Budget yetu ni tegemezi tutake ama tusitake. Ila sasa kwa mchezo unaendelea nchi wafadhili wakipunguza misaada ina maana tutabanwa zaidi ndani na tukibanwa zaidi ndani ina maana kutatokea mfumuko wa Dola kutokana na manunuzi yetu nje ya nchi hasa mafuta.

Hawa mabeberu wana akili sana na ndio maana CAG ni moja pia ya jicho lao la ndani hivyo ukimgusa unapoteza imani nao.

Well kuna mambo ni siri lakini ni lazima sote tumuombe Mungu atuepushe na jinamizi la kuharibika uchumi wetu maana uchumi ukiparaganyika ni vigumu sana kuujenga kwa mara moja.
 
Kuna wakati unajaribu kuipenda nchi yako sanaaaa lakini matendo ya waliochaguliwa kuongoza wakijizatiti kwa kujiamini kuwa wao wana uwezo mkubwa Wa kuchanganua mambo ilhali ni nafasi tu ambayo kimsingi sisi wana Wa nchi tumewapa na tunaheshimu mamlaka, hutufifiisha sana na kujiona hatuna maana katika nchi ya asili yetu.

Sisi wana Wa nchi ambao hatufungamani na siasa za mrengo wowote bali siasa za ustawi Wa nchi yetu tu tunaamini siku yaja tutaikomboa nchi yetu tukiwaacha wapiga porojo wanaoharibu nchi yetu wakistaajabu bila kuamini kinachotokea.


 
.
IMG_20191022_072648.jpeg
 
Acha ujinga wewe , tunajenga SGR, tunajenga Stieggler's, tumenunua madege, tunajenga mabarabara, tunajenga mahospitali kwa fedha zetu wenyewe... Hao mabeberu watupishe tunamadini na kilakitu wanatuogopa tunavyopanda kwa kasi na muda sio mrefu tutakuwa donor country.

Make Tanzania great again..
 
Bavicha mnahangaika bure
Yaani mabeberu waache Nazi zao washughulike na ajira ya MTU mmoja tu aliemaliza take kwa heshima?
Ivi nyie lumumba fc hamna utaratibu wa kufahamiana ama vile vichwa vya panzi mnasahau haraka

mtoa bandiko ni mboga mboga mwenzio,sema yeye akili imerudi kdg ndo maana unaona anaongea mambo ya msingi.

hata ww ikikurudia atakuja kukushangaa pia.
 
Ivi nyie lumumba fc hamna utaratibu wa kufahamiana ama vile vichwa vya panzi mnasahau haraka

mtoa bandiko ni mboga mboga mwenzio,sema yeye akili imerudi kdg ndo maana unaona anaongea mambo ya msingi.

hata ww ikikurudia atakuja kukushangaa pia.
Kwa hiyo unanipangia jinsi ya kutoaawazo yangu?
 
Mmmhhh!!!
Akiwa upande wako sifa wajaza kwake vile akosha mahitaji yako na akiwa kinyume na itikadi yako kwa jambo fulani basi kejeli matusi na yafananayo wamtunukia...

Ni wana Wa nchi wasio na mafungamano yakuimba mapambio ya kusifu na kuabudu itikadi za vyama vilivojaa hila dhidi ya utaifa tu ndio wanaoelekea kuikomboa nchi hii kutoka kwenye makucha ya wanasiasa wenye hila Wa pande zote waliojitamalakisha wakijiona wajuzi Wa utaifa ilhali ni wajuzi Wa maisha yao binafsi na familia zao.

Zidumu juhudi za awamu ya tano kwa kumuondoa CAG mchapakazi anaekubalika kimataifa
 
hapana nakukukumbusha tu mtoa bandiko ni LUMUMBA mwenzako kama kaenda kinyume na maagizo yenu ya kutukuza kwa mapambio akanywe
Mie ninaongozwa na fikra huru mkuu
Sio kama mazombi uchaguzi hakuna wapo bize na CAG,likiisha watarudi kwenye serikali za mitaa, mbowe haguswi,huko ndio kutukuza
 
Mie ninaongozwa na fikra huru mkuu
Sio kama mazombi uchaguzi hakuna wapo bize na CAG,likiisha watarudi kwenye serikali za mitaa, mbowe haguswi,huko ndio kutukuza
uchaguzi gani tena mkuu,huu ambao watendaji wanakimbia ofisi hata wakiwepo wanakataa pokea na kujaza fomu. ni uchaguzi ama vituko, na fikra huru ujaliona hilo. kuna matatizo ya izo fikra jaribu kuweka mpya

NB: mtoa bandiko ni Lumumba mwenzio, wapinzani wanaingiaje? mkuu
 
Back
Top Bottom