Ikikutokea wewe utafanyaje???

Ikikutokea wewe utafanyaje???

Sangarara

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2011
Posts
13,104
Reaction score
5,665
Umepata rafiki mtandaoni, kama hapa JF, wote mkashare mambo yenu mengi tena ya ndani kabisa ambayo inawezekena huyo rafiki ndio pekee amepata bahati ya kuyafamu.

Umemueleza kila kitu, na kweli tupu, kwa mfano, namna ambavyo mahusiano yako ya nyuma yalivyoharibika, jinsi ulivyoumia au kukiri pale ambapo wewe ndio ulikuwa sababu ya matatazo, na kwa namna ya kipekee kabisa kuelezea namna ulivyomuhitaji wa mapenzi, tena unampromise rafiki huyo kwamba Kama ni Mungu ndio ameamua kuwakutanisha mtandaoni ili kuziba upweke uliomo katika maisha yako basi unaahidi kuwa Muaminifu kwake maisha yako yote hapa duniani n.k. n.k n.k

alafu baada ya muda mrefu sana wa mahusiano hayo ya kidigital na kiroho tuuu, siku mmeamua kukutana kwa ajiri ya kuofficiate mapenzi yenu, unakuta ni mke/mme wako ambaye mlifikia hatua ya kuvunja ndoa yenu kwa sababu mlizodai kwamba hazirekebishiki ila divorce ndio the divine decision.

utafanyaje??
 
  • Thanks
Reactions: BAK
ikitokea hivyo ujue basi kuna strong bond kati yenu na bado mnapendana, hata muende wapi mtakutana tu!
 
Mungu hataki mtengane, hivyo kawarudisha tena, endeleeni kuwa pamoja!
 
rudianeni daaah thats ndoa bana alichokiunganisha mungu binadamu hawezi kutenganisha
 
Nitajua unafiki wa watu wa mtandaoni, na wala sitaendelea naye coz l know a real her/him.

Mtandaoni we give each other our best, maishani we give our real self.
 
Nampiga kibuti mara ya pili bila kuchelewa

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Ni jambo lisilo busara na la hatari kujidownload kwa mtu ambaye hamjawahi kuonana live
 
Hivi inawezekana vipi ukampenda mtu ambaye hujawahi muona!!!!
 
^^
Kwa sababu haijanitokea,,ngoja nisitamke nikaumba neno la kunigharimu baadae
^^
 
Nitajua unafiki wa watu wa mtandaoni, na wala sitaendelea naye coz l know a real her/him.

Mtandaoni we give each other our best, maishani we give our real self.

Wewe ndo umesema ukweli kabisa... bcoz....bado wanatafuta,,, so that is the first approach,,,na wengine wako kwenye mstari.....kila mmoja alieleza fikra zake akimaanisha he/she need the new one.....hakuna ndoa tena hapo....kila mmoja kivyake tena kwa amani.......Mungu kawaonyesha jinsi mlivyo muflisi wa mapenzi...
 
Nitajua unafiki wa watu wa mtandaoni, na wala sitaendelea naye coz l know a real her/him.

Mtandaoni we give each other our best, maishani we give our real self.
Kaunga
Kumbuka kwamba, wewe binafsi utakuwa umemueleza kila kitu ki ukweli, hakuna tena nafasi ya kwamba ni ule ule uongo wa mitandaoni.
 
Kikawaida si vyema kutoa mambo yako kwa mtu usiyemjua vizuri wala kuonana naye. Ila ikitokea hivyo na umekwisha kumwambia undani wako na ukweli ambao ulimficha wakati akiwa mkeo/mmeo basi kuna haja ya kukaa na kutafakari upya mahusiano yenu ya awali, kuzungumza na kuondoa tofauti zenu na kusameheana. Kama kweli ulikuwa unampenda hapo awali na sasa mtandaoni, na ukahisi kumkosa (miss) na ukafarijika baada ya kumwona tena basi binafsi nashauri kurudiana.
Katika kurudiana mnatakiwa kuwa marafiki wa karibu mno ili muweze kujua mnahitajiana kwa kiasi gani na ni kwa namna gani kila mmoja anajutia kosa lililosababisha kutengana, mmebadilika kwa kiasi gani kuweza kuishi kwa namna tofauti na mlivyokuwa awali. Mme au Mke si rahisi kuficha makucha kwani walikwisha fahamiana vizuri hivyo ni rahisi kujua kama mwenzako kabadilika ama la na hivyo kuweza kuamua.
Ni vyema wanandoa kuishi pasipo kutegemea kuachana hii itawafanya kuwa makini kulinda ndoa na kutatua tofauti zao mapema ili waendelee kufurahia tasisi hii nzuri iliyowekwa na MUNGU kwa watu wake. Mpango wa Mungu ulikuwa ndoa idumu milele lakini baada ya shetani kuingilia basi akasema kifo tu ndicho kiwatenganishe hata hivyo kutokana na uhaba wa imani na mioyo ya watu kuwa migumu Kristo akasema ndoa isiachike isipokuwa kwa sababu ya uzinzi.
 
Hii imeshawahi kutokea Zambia na ndoa yao ilikuwa haijavunjika ila ilikuwa ipo ipo tu. Baada ya kukutana kwao wakaamua kuvunja ndoa yao.

Umepata rafiki mtandaoni, kama hapa JF, wote mkashare mambo yenu mengi tena ya ndani kabisa ambayo inawezekena huyo rafiki ndio pekee amepata bahati ya kuyafamu.

Umemueleza kila kitu, na kweli tupu, kwa mfano, namna ambavyo mahusiano yako ya nyuma yalivyoharibika, jinsi ulivyoumia au kukiri pale ambapo wewe ndio ulikuwa sababu ya matatazo, na kwa namna ya kipekee kabisa kuelezea namna ulivyomuhitaji wa mapenzi, tena unampromise rafiki huyo kwamba Kama ni Mungu ndio ameamua kuwakutanisha mtandaoni ili kuziba upweke uliomo katika maisha yako basi unaahidi kuwa Muaminifu kwake maisha yako yote hapa duniani n.k. n.k n.k

alafu baada ya muda mrefu sana wa mahusiano hayo ya kidigital na kiroho tuuu, siku mmeamua kukutana kwa ajiri ya kuofficiate mapenzi yenu, unakuta ni mke/mme wako ambaye mlifikia hatua ya kuvunja ndoa yenu kwa sababu mlizodai kwamba hazirekebishiki ila divorce ndio the divine decision.

utafanyaje??
 
Hii imeshawahi kutokea Zambia na ndoa yao ilikuwa haijavunjika ila ilikuwa ipo ipo tu. Baada ya kukutana kwao wakaamua kuvunja ndoa yao.

Bad. I wish they should have taken that as an opportunity to reconcile their misunderstandings? I think the major problem with us is the physical appearances? when you are overly used to your partner we tend to seek for a difference because I have never heard relationships breaking and couple give physical reasons like she has become too fat or their are much prettier chics around than her or, he is no longer handsome or he is becoming too old for me. but i think these are the key reasons otherwise how do you feel to love someone you have never seen.
 
Mie ningeendeleza hayo mapenzi motomoto na tungefanya hannivessare. Kinachoua ndoa ni kuamua kuwa a beast. Kama tuliweza kuelewana mtandaoni, tukiendeleza hayo ya kutakiana lunch njema and dressing up for a phone call basi ndo naendelezea hapo kabisa. Its a second chance kujijua kuwa kama nikibadilisha attitude basi naweza kuishi maisha ya furaha bila mask.
 
Back
Top Bottom