Ikigundulika kweli..! Je, neno Bashite kuwa visawe na neno Kihiyo?

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
6,042
10,787
Habari wakuu,

Hapa bongolala tumekuwa na misamiati isiyo rasmi ambayo imekuwa ikitokana na matukio ya watu au matendo ya watu na kupelekea kuwa msamiati.

Mfano wa maneno hayo ni

1. Kihiyo - Jinsi Ramadhan Kihiyo alivyojiuzulu baada ya kashfa ya kufoji vyeti
2. Maumba - Unakumbuka nini ukisikia jina la Maumba na Kihiyo?
3. Masaburi - Neno "Masaburi" Lina maana gani?
4. Kilaza - Mwanamuziki Juma KILAZA na asili ya neno KILAZA

Hata Rais Magufuli aliwaita wanafunzi wa UDOM vilaza, kwa mujibu wa Honi Siggala wa BAKITA (Kama sijakosea jina) alisema msamiati KILAZA sio rasmi, labda wafanye mchakato waone kama kuna uwezekano kama unaweza kuwa msamiati rasmi.

Ukisoma hizo mada tajwa utaona maneno(Misamiati) hiyo ilitokana na majina ya watu waliotenda/kunena vitu vilivyoishangaza jamii.

Tukirudi kwa jina Daudi Bashite, bila shaka kwa sasa ndio jina linalozungumzwa sana kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vya habari.

Ikiwa Daudi Bashite atatiwa hatiani kama ilivyokuwa kwa Kihiyo kwa udanganyifu wa elimu, basi ni wazi kutaibuka msamiati mpya wa Bashite ukiwa na maana sawa na Kihiyo.

Tusubiri tuone mwisho wake.
 
Kumbe elfu moja INA Bashite tatu. Looooo!
Ila nasikia maana ya Bashite kwa Kikolomije in WABANE/ WAKANDAMIZE. Nipeni ukweli mnaojua lugha hii.
 
Kama kihiyo ilivokuja kuwa msamiati wa kiswahi masna ake mjinga na kingunge nalo likawa mtu mzito
 
tupieeeni hapa audio wakuu tupunguze stress za bongoland
 
UKISTAAJABU YA MUSA YA FIRAUNI YANAKUJA, NENO BASHITE SASA LIMEKUWA NA MAANA YA 'ZERO' YAANAI SIFURI UKITAKA KUMPA MTU NAMBA YAKO YA SIMU MFANO 071.056010
utatamka BASHITE SABA MOJA . BASHITE TANO SITA BASHITE MOJA BASHITE.
WATANZANIA SIWAWEZI DUUUUUU.
bashite713
 
Nimesikiliza audio yake iliyopo mtandaoni yaani nmecheka hadi mbavu zinaniuma.....sichekagi kirasi Ila hiyo audio ya kutaja namba nimeshindwa kujibana...nikaliachia cheko
Mkuu tupia hyo audio katika mfumo wa kuweza kuidownload ikakaa kwenye file yangu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom